Nimetoka ukweni Kigoma, ila kama hii ndiyo aina ya wazee acha wabaki na watoto wao!

Mkuu huku niliko hiyo 500k(mkaja wa mama) pekee unapata mke tena ndoa kabisa na chenji inabaki ya nauli na kuanzia maisha
 
Wewe unajifanya kuwa na hasira wakati ndiye mwenye makosa tangu mwanzo, umeishi na binti wa watu mpaka unamtia mimba na hadi anazaa hujajua kwao au kuwasiliana na watu wao.
Vijana wa kisasa mna ujinga sana, muneharibu mabinti wa watu kwa mtindo huu, halafu mbaya zaidi unataka umtelekeze kisa babake alikemea tabia mbovu zako hizo.
Omba radhi, anza kulipa mahari, kawaida mahari unaweza ukalipa taratibu kidogo kidogo ila tafuta kusamehewa wewe kosa ulilolifanya tangu mwanzo.
Kuna siku utakua na binti kisha utaelewa nini maana ya mwanao kutiwa mimba mjini huko na limtu ambalo haliwasiliani na wewe.
 
Alijua unampenda sana maringo kibao. Na hivi ndio inatakiwa unampenda mtu nyodo kama zote siku ukiamsha unaamsha kimoja.
Na nilimpenda haswa sio masihara..
Yote kwa yote only time healed me, i got a lesson and nothing bothers me anymore. It's been 4 years, im living my life
 
Sawa kakosea hapo, ila Million 4 unaijua mkuu? Hapo ni nje na mambo mengine ya kusindikizia.. hata kama aisee, haitokaa itokee kwangu. Labda kwa mleta uzi
 
Mahari ni biashara ya utumwa tu, mwanamke anauzwa.
 
Ulienda na kanzu ya rangi gani? Ndevu ulipakaa rangi?
Kigoma unaendeleaje kama huwezi kubishana?
 
Kwa hiyo unataka binti yako atiwe mimba na lijitu unalowasiliana nalo, ili likwambie kwamba sasa namtia mimba binti yako?
 
Pole mkuu,

Lakini unadhan ukimuacha huyo mwanamke kisa huwezi kuunganisha undugu ataenda wapi!?
Huoni kama utamuanzishia safari ya majonzi na ngumu kiukweli.

Kama unampenda jaribu kumfeel namna atavyojiskia yeye,
Hapo kikubwa ni kwenda nae tu,
Maisha yako wewe yanapaswa kuundwa na mme(Me) na mke (Ke). Wazazi (W) ningekushauri tu uende nao hivyo hivyo maybe mtapatana huko mbele.
assume tu kuwa W ni constant

Life = WKeMe
 
Ndio maana kuna watu wanapinga mambo za mahari sababu ndio kama hizi. Kwani angepokea hyo 1M angepungukiwa kitu gani?? wazee wengine nuksi sana.
Kuna wazee ni watata.
Utata ni sifa zao za kinasaba kabisa
 
Nikiwa unampenda mwanamke,nakushaur tafuta mahar iliyo ndani ya uwezo wako mpatie huyo baba mkwe then muahid nyingine utaendelea kumpa kadirisiku zinavyoekwenda baada ya hapo the rest is history
 
Kaka huwezi kuacha mke na mtoto kwasababu ya baba yake, kwani anaekupa utamu ni mke au baba yake? Mpuuze huyo mzee maisha yako na mwanae yaendelee huku yeye akizidi kuzeeka akisubiri mahari
Ebhana e, kwani anayempa utamu ni binti ama baba mkwe? 😀
 
Huu ndiyo ushauri wa maana
 
tumepata msiba hajawahi kuja kutupa pole zaidi ya kupiga visimu vyake tu,
Kwa kifupi hawa wakwe walikuwa wamekukataa, walijua kuwa wewe siyo binadamu wa kawaida. Hata angekuwa mtu mwingine tofauti na hao, naye pia vile vile angekukataa
Waha wana maadili sana ukiwaendea vingine wanakushangaa
 
Sawa kakosea hapo, ila Million 4 unaijua mkuu? Hapo ni nje na mambo mengine ya kusindikizia.. hata kama aisee, haitokaa itokee kwangu. Labda kwa mleta uzi

Hapa issue sio kiasi cha hela, hata kama baba kaagiza milioni kumi, hayo ni mambo ambayo huzungumzwa na kuwekana sawa, ila mwanzo dogo alipaswa kurekebisha kosa alilolifanya.
Sasa anataka kutelekeza familia, mama na mwanaye kisa babake binti alimfokea kwa alichokifanya? Huyu dogo awajibike, hata kama hatoitoa hiyo mahari haipaswi atelekeze familia, ahusishe wazee wa kwao wamsaidie kurekebisha.
 
Pole anayeolewa ni dada wala sio baba yake,mkatae shetani,we ishi na mkeo funga ndoa hukohuko mengine achana nayo
Usimlaumu mzee wale wakisikia mtu anatoka dar wanajua tyari hela ipo ya kumwaga,nakusihi punguza hasira

Sent from my HUAWEI MLA-AL10 using JamiiForums mobile app
 
Sawa kakosea hapo, ila Million 4 unaijua mkuu? Hapo ni nje na mambo mengine ya kusindikizia.. hata kama aisee, haitokaa itokee kwangu. Labda kwa mleta uzi
Kweli hiyo pesa ni nyingi kwakuwa kafanya makosa na dharau ukweni , ila angekuwa haja fanya makosa naamini ata laki 8 ange pewa mke, hiyo milioni 4 kuna adhabu ndani yake.
 
Kweli hiyo pesa ni nyingi kwakuwa kafanya makosa na dharau ukweni , ila angekuwa haja fanya makosa naamini ata laki 8 ange pewa mke, hiyo milioni 4 kuna adhabu ndani yake.
Yaani kwangu haiwezi. Siwezi toa milioni 4 hata kama na adhabu humo. Hata mil.2 sitoi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…