Atoto
JF-Expert Member
- Jul 19, 2013
- 86,410
- 169,862
Sio kosa lako.Wewe MUHA waambie waha wenzako wapunguze upumbavu. Mnanuka shida mnatafuta magepu kiboya.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sio kosa lako.Wewe MUHA waambie waha wenzako wapunguze upumbavu. Mnanuka shida mnatafuta magepu kiboya.
Kosa ni tamaa zenu wahaSio kosa lako.
Pole sana kwa kilichokukuta!!Hata Mimi ningekwazika!Ulichokosea ni kitu kimoja,ulitakiwa kabla ya kwenda uzijue mila na desturi za waha,au kwa ujumla wake tamaduni za waha!Sikushauri uoe au uache kwa sababu jambo hilo ni la kibinafsi!Mimi nimeoa muha lakini ni baada ya kuzinguliwa sana na wazazi wa mchumba wangu wa kwanza wa kinyakyusa!Sijui ungefanyaje kama yangekupata kama yaliyonikuta Mimi kwa huyo mnyakyusa!!!yangekupataenye mahusiano na mwanamke kutoka Kigoma tangu 2020, tulikutana chuo, na penzi likakolea haswaa!
Kipindi cha Covid penzi lilinoga zaidi kwani "Working from home" ilifanya muda wote tuwe pamoja, ilikuwa mwendo wa kwenda sokoni kununua mazaga zaga pamoja, tinaweka ndani then kila baada ya mlo ni mnyanduano tu, hatimaye binti akashika mimba!
Baada ya mimba kufikisha miezi minne bibie akaniambia ni bora aende kwao kwanza kwani kubaki tukiwa wawili hatuwezijua complications za mimba, nilikubaliana nae, nikajipiga kwa kadri ya uwezo wangu nikamkatia tiketi na vizawadi kidogo vya wazee akaenda kwao!
Akiwa kwao mawasiliano yetu yalikuwa vizuri kabisa mpaka akajifungua salama salmin, na mimi niliwajibika haswa mpaka dk. ya mwisho, hatimaye tukapata mtoto wa kiume.
Bibie baada ya mtoto kufikisha miezi 6 bila mimi kwenda kujitambulisha akatoa wazo la kurudi kwangu kwani alikuwa amechoka kuishi nyumbani kwao, nikamkaribisha tukaendelea na maisha ya sogea tuishi.
Mwaka jana December, ilitokea msiba kwao akalazimika kwenda msibani, nikamfanyia maandalizi vizuri kabisa, akaondoka.
Amekaa huko tangu December, mpaka juzi nilipoamua kufuata taratibu za kwenda kwao ili tusiendelee kuishi kimya kimya (tufanye kuwa official), nikajiandaa kwa mambo kadhaa kama nilivyokuwa nimeng'atwa sikio na mpenzi wangu.
Nimeanza safari kutoka Dar kwenda Kigoma (kwao), nikiwa nimeambatana na brother wangu wa damu, aisee kwao ni mbali, maana tulitembea siku 2 njiani, tulipofika mjini, safari ya kwenda kwao ikachukua masaa mengine 8, vumbi kali hatari, tulipofika Kijijini kwao tukaambiwa Burundi ni mwendo wa kutembea nusu saa tu.
Brother akaniuliza, "Hivi dogo hukuona wanawake mikoa yote tuliyopita mpaka kuja huku?" Nikamwambia mapenzi yana nguvu bro, sikuwahi kufikiria kama kuna siku ningesafiri umbali namna hii kufuata mwanamke tu. Tulipofika mjini tulitafuta mzee mwenyeji, anayejua mila na desturi za Kiha ili mambo yasiwe magumu.
Basi bwana, tumefika pale tumepokelewa vizuri wakaandaa utaratibu wa mjadala, mshenga akatambulisha na kuanza mazungumzo rasmi, hapo nilikuwa na zawadi ya baba mkwe na mama mkwe, nilinunua tangu Dar kwa upendo kabisa.
Wakataja kiasi cha mahari kuwa wanataka mil. 4.5, hapo tukashtuka kweli, kabla hatujakaa sawa wakataja mkaja wa mama sh. laki saba, jumla wanataka 5.2 Milioni!
Yule mzee tuliyeenda naye akaomba twende nje kwa mazungumzo, akatuuliza kama tulipewa mwongozo na tuliyekwenda kumuoa, nikamjibu ndiyo (alisema mahari kwao haizidi Milioni moja) na mkaja wa mama huwa ina-range kuanzia 100k - 200k, na mimi niliandaa 200k kama mkaja wa mama! Mzee akasema hapa kuna tatizo, huku haijawahi kutokea mahari kubwa kiasi hiki, akasema tutasimamia kwenye hiyo 1M na mkaja wa mama 200k, tukarudi ndani!
Mzee (mshenga) akaanza kuzungumza, kuwa sisi tuna mahari 800k na mkaja wa mama 100k, lakini pia tuna zawadi kwa ajili ya baba na mama, ambazo si sehemu ya mahari, ni zawadi tu ya kijana wetu kwenu, mzee akatoa zile zawadi akaweka mezani.
Mshenga wao akashukuru na kuanza kuzungumzia mahari yetu kuwa angalau tufanye mahari mil.4 mkaja wa mama 500k.
Kabla hajamaliza akasimama baba mkwe, akionyesha kukasirika akasema "Sitaki mjadala wa kitoto hapa, mimi ndiye baba wa x, mkaja wa mama laki 5, mahari yangu nataka Milioni 4, Sitaki mjadala wala kusikia kupunguziana, kwanza unabeba zawadi kutuletea nani amekutuma utununulie, tumekuomba sisi utuletee zawadi zako?"
"Kwanza huyu kijana anadharau sana, tangu mtoto azaliwe hajawahi kufika hapa nyumbani, anaishia kumtumia mwenzake pesa tu, sisi hajawahi kututumia pesa hata mara moja, tumepata msiba hajawahi kuja kutupa pole zaidi ya kupiga visimu vyake tu, sasa mimi nimeshasema mkaja wa mama laki tano, mahari Milioni 4, sitaki mjadala!"
Aisee nilijikuta nimejaa hasira mpaka basi, mshenga wetu akatutaka twende nje, akasema "huyu mzee inaonekana ana lake jambo, tusiingie kwenye mtego wake, iweni wapole, tuondoke salama, watu wa huku ni hatari sana, tukiwa na hasira tunaweza tusirudi salama, hii si dalili nzuri."
Tukajadili tuvyojiandaa pale, mzee akasema muhimu tuanze na mkaja wa mama, tuwawekee hiyo 500k then tutawapa faini za mbuzi mbuzi, na vingine vidogo vidogo, baada ya hapo mahari tuwaambie kuwa tunaenda kuitafuta then mtaangalia wenyewe baada ya kufika nyumbani!
Tuliporudi ndani tukakuta mzee anaonyesha kuwa na hasira hasira tu, kiasi kwamba mshenga wao akawa ameduwaa tu, basi mshenga wetu akaanza kujitetea pale, akaweka mezani Tsh. 500k mkaja wa mama, akawaambia mbuzi watatu wa uchafuzi 300k, sijui koti la mjomba, mara blanketi ya wazee na vikolo kolo vingine kwa Kadri ya taratibu zao, ile pesa tuliyoenda nayo ikawa imekata!
Muda huo wote nina hasira vibaya mno, ila najitahidi kuificha japo mpenzi wangu aligundua kabisa kuwa nimechukia. Tukawaambia hiyo mil. 4 tunaenda kuitafuta, mzee akasema "Mkaitafute muilete hapa, au mutanitumia kwenye simu," tukawaambia sawa.
Muda wa kutoka nikakuta mpenzi wangu ameshabeba mabegi anataka tuondoke wote, nikamwambia hapana unapaswa kubaki nitakuja kuwachukua nikimalizia mahari. Akagoma, akawa analia wakati wote akiwa amenikumbatia, anaomba radhi kwa kilichotokea ila anaomba tuondoke wote, yeye hawezi kubaki kijijini tena. Nikamwambia hapana, unapaswa kubaki mpaka tumalizane na mzee, akagoma kata kata, akawa amepiga magoti huku amekumbatia miguu yangu, machozi yanamtoka tu!
Mzee wake alipotoka akaona mwanaye analia akasema "Kama mnaondoka wote nendeni tu!" Mara mama mkwe akaja na dogo (mtoto wangu), akamshusha nilipokuwa, nikambeba mtoto nikamwambia mama mtoto asimame, bro na mshenga wetu wakaniita pembeni, mshenga akasema tuondoke nao, tukimuacha na wakahisi kuwa kuna dalili za sisi kutorudi, watamuua huyu mtoto.
Basi kishingo upande, tukawakubalia kuondoka nao, mama mkwe akaleta maharage na jogoo akataka tuondoke navyo, nikakataa kuchukua, nikamwambia tutabeba wakati mwingine, akagundua bado nina hasira. Akamuita mtoto wake, akamwambia "Mwambie mumeo amsamehe bure baba yako, amekosea sana, na mimi mama naomba atusamehe tu."
Tukaondoka zetu, kichwani nikiwa nimejaa mawazo mengi mno, kiasi kwamba sikuweza kujua niamue nini. Tumefika Dar lakini moyoni nimejikuta sina tena interest ya kutengeneza undugu na familia ya mpenzi wangu, japo yeye binafsi hana shida, lakini kwa namna tulivyopokelewa na tulivyoondoka, nilijisemea moyoni kwamba sitokaa nirudi Kigoma, wala sitokaa nipeleke hiyo mahari waliyosema.
Nasubiri mwanangu akuekue kidogo nimwambie mama mtoto kwamba hakuna namna naweza kuunganisha undugu na familia yake, japo namhurumia ila ndiyo hivyo tena.
Kweli tembea uone, all the way from Dar to Kigoma, naenda kukutana na aibu tu, anyways.
Tamaa, mijitu ina njaa tu. Ndoa ni baraka, sasa kama mzee alileta mapingamizi ya kishoga maana yake nini? Ni suala la kuongea na kumueleza mtu pale alipokosea. Shida mijitu inatembea na mambo yao ya enzi za ujimaPole sana kwa kilichokukuta!!Hata Mimi ningekwazika!Ulichokosea ni kitu kimoja,ulitakiwa kabla ya kwenda uzijue mila na desturi za waha,au kwa ujumla wake tamaduni za waha!Sikushauri uoe au uache kwa sababu jambo hilo ni la kibinafsi!Mimi nimeoa muha lakini ni baada ya kuzinguliwa sana na wazazi wa mchumba wangu wa kwanza wa kinyakyusa!Sijui ungefanyaje kama yangekupata kama yaliyonikuta Mimi kwa huyo mnyakyusa!!!
Sasa kama huyo mzee atakaza unadhani nini kinaenda kutokea? Ni kutelekeza tu. Siwezi toa hata mil.2 mimi
Hilo zee la binti ndio shirikina. Au ndio Zee Korofi?Sawa usitoe hata milioni lakini sio utelekeze familia, vijana mumekua lege lege sana, kisa mzee kawa mkali umeamua utupe nje mama na mtoto wake.
Haya mambo huzungumzwa, husisha wazee, kwanza kosa sana kwa kwenda kulipa mahali umeandamana na kaka bila kuwa na wazee wa kwenu.
Ni tag nami mkuu .Haya yako malaini kabisa,mie nitakuja kuleta kisa changu humu nita kutag utaona yako cha mtoto kabisa.
Ndo mana namshangaa eti anaacha mke kwasababu ya baba yakeEbhana e, kwani anayempa utamu ni binti ama baba mkwe? 😀
KATAA NDOA❌❌❌❌❌Kwenye hizi mambo waamua kuoa kabla ya kuwa wakataa ndoa hukutana na visanga vingii mnoo.
Nilichumbia kisha nikalipa mahari na faini zoote.
Dah kumbe mama mkwe hataki binti aolewe.
Anataka abaki home amrithishe uchawi.
Nilianza kwa kupoteza kazi mara 5,biashara kufeli,mali kisha mahusiano na familia then nikamalizia na marafiki mpaka nakuja kushtuka ni baada ya miaka 10 nishaisha mbayaa.
Yaani utasikia mama anauliza tuu hivi baba mmepanga kufunga ndoa lini maana muda unaendaa eeehh kumbe nilikuwa nakosea kumjibu bhana wee muda ukikaribia tuu matatizo lukukii hakuna ndoaa.
Sasa nimeamua kumuacha ila binti hatakii,sikai nae nimekimbia na nimemuachia kila kitu na tuna watoto nimemuachia.
Wakuu sio kila mlango ni wa kuoa tuu,chunguzeni kwanza.
Kataa ndoa haiji tuu ghafla, kuna chanzo nyuma ya pazia.
wapi huko [emoji4]Mkuu huku niliko hiyo 500k(mkaja wa mama) pekee unapata mke tena ndoa kabisa na chenji inabaki ya nauli na kuanzia maisha
😅😂😆😄Kwa mimi sioni kama 4m ni tatizo, tatizo ni Baba Mkwe. Piga chini hiyo ndoa
MkuuNdoa ni utapeli !!
UMEONA SASA
Kijana Wala hilo lisikupe wasiwasi wazee hiyo ni mikwara tu hata sisi tulikutana nayo tukakaza Sasa ivi tunaishi Kwa amani kabisa kama mke anafaa kuolewa kaanae mzee atanyoosha maelezo usifanye maamuzi unahasira.Tengeneza urafiki na mzee Kwa kumtumia viposho hiyo ml 4 hautailipa atashusha tu cha msingi kama mke yuko poa tengeneza maisha.Nimekuwa kwenye mahusiano na mwanamke kutoka Kigoma tangu 2020, tulikutana chuo, na penzi likakolea haswaa!