Nimetoka ukweni Kigoma, ila kama hii ndiyo aina ya wazee acha wabaki na watoto wao!

Pole sana kwa kilichokukuta!!Hata Mimi ningekwazika!Ulichokosea ni kitu kimoja,ulitakiwa kabla ya kwenda uzijue mila na desturi za waha,au kwa ujumla wake tamaduni za waha!Sikushauri uoe au uache kwa sababu jambo hilo ni la kibinafsi!Mimi nimeoa muha lakini ni baada ya kuzinguliwa sana na wazazi wa mchumba wangu wa kwanza wa kinyakyusa!Sijui ungefanyaje kama yangekupata kama yaliyonikuta Mimi kwa huyo mnyakyusa!!!
 
Tamaa, mijitu ina njaa tu. Ndoa ni baraka, sasa kama mzee alileta mapingamizi ya kishoga maana yake nini? Ni suala la kuongea na kumueleza mtu pale alipokosea. Shida mijitu inatembea na mambo yao ya enzi za ujima
 
Sasa kama huyo mzee atakaza unadhani nini kinaenda kutokea? Ni kutelekeza tu. Siwezi toa hata mil.2 mimi

Sawa usitoe hata milioni lakini sio utelekeze familia, vijana mumekua lege lege sana, kisa mzee kawa mkali umeamua utupe nje mama na mtoto wake.
Haya mambo huzungumzwa, husisha wazee, kwanza kosa sana kwa kwenda kulipa mahrli umeandamana na kaka bila kuwa na wazee wa kwenu.
 
Hilo zee la binti ndio shirikina. Au ndio Zee Korofi?
 
Kwenye hizi mambo waamua kuoa kabla ya kuwa wakataa ndoa hukutana na visanga vingii mnoo.
Nilichumbia kisha nikalipa mahari na faini zoote.
Dah kumbe mama mkwe hataki binti aolewe.
Anataka abaki home amrithishe uchawi.
Nilianza kwa kupoteza kazi mara 5,biashara kufeli,mali kisha mahusiano na familia then nikamalizia na marafiki mpaka nakuja kushtuka ni baada ya miaka 10 nishaisha mbayaa.
Yaani utasikia mama anauliza tuu hivi baba mmepanga kufunga ndoa lini maana muda unaendaa eeehh kumbe nilikuwa nakosea kumjibu bhana wee muda ukikaribia tuu matatizo lukukii hakuna ndoaa.
Sasa nimeamua kumuacha ila binti hatakii,sikai nae nimekimbia na nimemuachia kila kitu na tuna watoto nimemuachia.
Wakuu sio kila mlango ni wa kuoa tuu,chunguzeni kwanza.
Kataa ndoa haiji tuu ghafla, kuna chanzo nyuma ya pazia.
 
You look smart.
Wangekutana na mwehu kama mimi ningeharibu.
Ningewaambia nafuata pesa bank mjini nikadraw.
Ndo basi tena wasingeniona tena
 
KATAA NDOA❌❌❌❌❌

KATAA NDOA❌❌❌❌❌
KATAA NDOA ❌❌❌❌❌
 
Mahali haimalizwi kwa taratibu za ki africa. We tafuta hata 1.5M peleka. Hyo nyingine unapotezea.
Usitumie hasira usije juta mbeleni kupata mke mwema kwa sasa napo ni mtihani
 
Hasira zikiisha utakuwa sawa.

Pole sana , process za mahari huwa zinaumiza sana
 
Kijana Wala hilo lisikupe wasiwasi wazee hiyo ni mikwara tu hata sisi tulikutana nayo tukakaza Sasa ivi tunaishi Kwa amani kabisa kama mke anafaa kuolewa kaanae mzee atanyoosha maelezo usifanye maamuzi unahasira.Tengeneza urafiki na mzee Kwa kumtumia viposho hiyo ml 4 hautailipa atashusha tu cha msingi kama mke yuko poa tengeneza maisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…