Nimetoka ukweni Kigoma, ila kama hii ndiyo aina ya wazee acha wabaki na watoto wao!

Mahali huwa haiishii , we mtumie mzee kidogokidogo, ukipata laki 5tuma, ikifika 1.5 m unakausha piga mimba huyo mkeo maisha yaendelee , mkeo hana hatia
 
Huyo mwanamke kama kweli mnapendana usimuache,mapenzi ya kweli huja mara moja tu ktk maisha..huwezi kumuacha mwanamke wako kwa sababu ya upuuzi wa baba yake..kama na penzi lako dogo
 
Pole best. Mke anakupenda Kwa dhati nadhani mpende pia. Wazazi wake fanya kuwasamehe lakini usiende tena kigoma. Mwisho funga ndoa harali ikibidi bila hata wazazi wake kuwepo ili likitokea la kutokea uwe on safe place
Asithubutu kufanya hivyo...kwa waha hilo ni kosa kubwa sana..ipo siku atakuja kuitolea maiti mahari na atafungishwa ndoa na maiti.
 
SI mbaya hata mama mkwe wako ni mwelewa,ila ujifunze kuishi na watu hasa wanapopatwa na shida
 
Lipa kidogo kidogo ,watu wa vijijini SI waelewa sana,kama utamwacha huyo Binti watakumaliza ndugu
 
Tulienda na gari tukaiacha mjini, kutoka mjini kwenda huko Kijijini tulikodi boda boda kwani njia ni mbaya mno!

Kuna fanana na mahali fulani hukohuko tulienda kumzika mfanyakazi mwenzetu tukiwa na Gari yetu ya ofisini ya enzi hizo (chai maharage), tulipata shida sitosahau na turiporudi Dar Ile Gari ilipelekwa gereji na haikutengenezeka Tena mpaka akauziwa Mangi
 
La maana Kama mwanamke anakupenda, waambie poa naenda kufikiria. Kaishi na mtoto Ila muwape zawa tu kidogo. Mzee akija juu nawe mjibu na wewe utawapa Nini wazazi wangu walionitunza mpaka nikaja kumchukuwa binti yako? Ila uwe ngangari, Kigoma sio mchezo.
 
Nimekutumia msg inbox..ifanyie kazi
 
Mume mtarajiwa huwa huwa haingii kwenye vikao vya mahari, huingia na kupokelewa baada ya mambo yote kuhusu mahali kuwa yameshafikiwa.
Vikao vya mahari huwa kuna mitifuano mingi hayo mambo yenu ya kisasa ndiyo yanawaponza na hatimaye mume anaingia kwenye mtafaruku na wazazi na ndugu wa mke.

Vv
 
Kwa hiyo kwa mtazamo wako sisi kutoka Dar mpaka Kigoma kwenda kuyajenga tulikuwa wapumbavu?
Ilikuwa busara kuona dhamira yetu na kuwa muungwana, ila kwa réaction aliyoonyesha atabaki n'a mtoto wake tu, siwezi kuwa n'a baba mkwe wa aina yake
Dogo lazima ukubali kuwa una matatizo. Ulifanya ujinga, umemtia binti wa watu ukaendelea kumficha kwako badala ya kujisalimisha mapema.

Badala ya kwenda mikono nyuma, kwa adabu, unyenyekevu na kuomba radhi, unajifanya kijogoo na mwenye pesa!. Milioni 4 unaiona pesa nyingi bila kuhesabu madhira uliyosababisha kwa wazazi wa huyo binti. Ulitakiwa kuwa na hekima kubwa kwa kutanguliza wajumbe kuyamaliza ndipo ukaribishwe kwa heshima kama mwana aliyekosea na kujirudi.

Kwa ujinga wako unawaza umbali, mahari na faini uliyojipangia mwenyewe, unajiaibisha. Jipange, tuma wazazi wako au wajomba/shangai ili wayaweke sawa na yataisha kilaini badala ya kuchukua mtu barabarani ati kuchukua nafasi ya wazazi. Ingekuwa wewe ungempokea mtu ambaye hata sio ndugu yako kuchukua nafasi ya wazazi? Kaka yako ni mtoto kama wewe kwa wakwe zako, kiri kukosea na utengeneze upate mke.

Vv
 
Fact!
 
Sasa hi ndo maana halisi ya ule msemo wa " Kupigwa kitu kizito kichwani".

Baba mkwe alitisha Sana kwa kweli dah 🤔
 
Ni bora uoe kwa mkopo kuliko ukitokomea Kigoma siyo kwa utani

Pamoja na yote tusisahau suala la bandari yetu kwenda kwa waarabu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…