Nimetoka ukweni Kigoma, ila kama hii ndiyo aina ya wazee acha wabaki na watoto wao!

Ww usiwe na wasiwasi Mahalia waga hawamslizi ukimaliza Mahalia ni dharau ,Peleka nusu ,yaan 2M ,Oa hiyo iliyobak muwaambie mtamaliziaga.
Pesa haisuswi ,babamkwe ataipokea tuu.
 
Kuna baadhi ya Mila na desturi wazee ndio huongea hayo Mambo na kuwekana sawa, kwao ni kosa kijana kwenda kuzungumza na mzee. Wenye experience na hili watalielezea zaidi.
Uko sahihi sana. TheMnyonge ame apply u town sana sana kitu ambacho kwa wazee hasa vijijini ni ngumu kueleweka. Ndoa ni ishu za kimila sana wewe sio wa ku resolve hizo mambo hssa ukizangatia ulishamtia mimba mtoto wa watu kitu ambacho ni kosa kubwa sana ingawa kimjin mjin tumeamua kulipotezea tu ila kwakifupi ulikosea. Msafara mzima wa mahali mko masela hakuna hata mama mtu mzima wala mashangazi? Kubali tuu kuwa mlienda kihuni sana
 
Usimuogope baba mkwe Wala Nini. Ishi na mke wako swafii. Litokee na kutokea. Baba mkwe ana lake jambo.
Kwani mke wako ng'ombe?! Mke wako Hana tatizo lolote. Kila la kheri
 
Hii ishu n simplee sn..hivii hujui binadam Kuna wakat tunaongeaga maneno magumu sbb ya hasiraa?ulitakiwa hta baaad ya hapo jion ukutane nae babamkwe mkiwa wwil..myajenge..kwenye maisha Kuna moment lazim mmoja ajifanye mjinga
 
Mkuu maisha yamebadilika, basi azalishwe huyo mtoto wako ubaki nae hapo nyumbani.

Maswala ya watu kwenda kujionesha Huwa yanachangiwa na sababu nyingi Uchumi ukiwa Moja ya sababu.
 
Sijajua wewe kabila gani yani umuharibi maisha binti yangu uishi naye kama mke bila baraka ya wazazi kisha umzalishe aje nyumbani kwangu kila uje na zawadi za danganya toto.
Kabila lenu inaonekana mabinti hawazalishwi wakiwa nyumbani
 
Hiyo kawaida ila ulichokosea ni kutafuta mshenga mmoja walitakiwa angalau wawilii au watatu,wasaidiane mawazo,mmoja inakua shida,sababu wao upande wa mke wanakua wengi sana,Mitifuane hiyo hua ivyo siku zote,we tafuta hiyo milion 1,hiyo nyingine itaendelea kua deni
 

Mzee amejawa tamaa

Hii dunia kuna watu hutaka kutoka kimaisha kupitia ndoa za watoto wao.

Mwanamke anakuwa branded kama product watu wapate pesa, unyanyasaji na mateso kwa mwanamke ni vita isiyo na kikomo.

Nadhani jamii ifanye kitu kuondosha hizi sarakasi za mahari au kuweka standard ya mahari kama zawadi na sio kumuuza mwanamke kama product dukani
 
Pole best. Mke anakupenda Kwa dhati nadhani mpende pia. Wazazi wake fanya kuwasamehe lakini usiende tena kigoma. Mwisho funga ndoa harali ikibidi bila hata wazazi wake kuwepo ili likitokea la kutokea uwe on safe place
Safe place ipi ikiwa wazazi watakana kutambua hiyo ndoa?

Wale huwa wanasubiri mtoto wao afariki ili wakatae kupokea mwili na kudai uwarudishie mtoto wao akiwa hai kama ulivyomchukua

Kigoma ni hatari, narudi tena ni hatari
 
Ndugu pole nimeumia hilo zee syo muha sisi hatuko hivyo mpende mdogo wangu usimwache hilo zee nipe details nipo huku rikizo nitalinyoosha
Hahahaa, mkikaa mnaongea kilugha mwanzo mwisho yaani
 
Pole mkuu. Lakini hiyo mahari nadhani ni reasonable hasa ukizingatia ulimzalisha mtoto wao na ulichelewa kwenda kujitambulisha! Mimi sijamzalisha wa kwangu lakini nimepigwa mahari 3.8 M na wanyakyusa wa Simike wale!
Wanyakyusa ukupangiwa mil.3 basi jua ni 1.5M, huwa hawamalizi mahari, lakini kwa Kigoma nimeambiwa unatakiwa kumaliza pesa yao yote kama ilivyotajwa!
 
Hongera kwa kubeba jukumu la kumuuguza baba mkwe, angekuua sasa hivi angekuwa anatia huruma tu
 
Mbaya zaidi ntalazimika kumuacha mtoto wao kwa makosa ya baba yake
..utakuwà mjinga ,Mimi baba mkwe alinifokeaga vyakutosha ...ila nilidharqu nilijua kosa langu ..kutia mimba nje ya ndoa! Wewe kama mama watoto anakupenda ...hakuna shida! Huyo Mzee mpotezee!
 
Kuna baadhi ya Mila na desturi wazee ndio huongea hayo Mambo na kuwekana sawa, kwao ni kosa kijana kwenda kuzungumza na mzee. Wenye experience na hili watalielezea zaidi.
Hilo nalo alikosea alitakiwa atangulize msamaha mapema sana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…