Unachofanya wewe ni kutangaza vita wakati hayo mambo yanaisha kwa maongezi tu.
Hatapatikana mbabe kila mtu atavutia kwake na atakaeumia ni huyo mtoto wa kike asie na hatia kabisa.
Huyo binti unamtesa kwa makosa yasiyo yake, yeye kukusikiliza zaidi wewe usiitumie kama fimbo kumnyanyasa kwa makosa ya baba yake.
Mzee kasomesha, hujui alitegemea nini toka kwa bintiye, halafu umesema ni bush ndani ndani huko si ajabu elimu kwao ni bahati tu.
Halafu mwisho wa siku binti uliesomesha kwa tabu anakuja na mimba tu tofauti na ulivyotarajia.
Ukiielewa situation ya mzee mbona unamtuliza na anatulia, ila wewe unataka ulete ubabe na yeye hawezi kubali kuletewa ubabe.. Mwisho huyo binti kwao atatimuliwa na wewe utamtimua vilevile.
Situation ya mzee ingekuwa mbaya kama mtoto wake angekuwa alitelekezwa, lakini nimekuwa na yeye bega kwa bega, tangu ujauzito mpaka leo!
Tumechelewa kwenda kujitambulisha na kulipa mahari, (hilo nakubali ni kosa) lakini je, ni kosa linalofanya aamue kunikomoa n'a kunidhalilisha ?
Naamini baada ya watu kuoana undugu na mashirikiano huendelea, husaidiana katika huzuni na furaha, sasa ukinihuzunisha na kunisimanga kwa sababu una "hasira" kwa vitu ambavyo havina maana kabisa nitakuchukuliaje? Utegemee kuwa tutashirikiana kweli?
Lakini kilichonishangaza zaidi ni kwamba mama mtoto wangu ananiambia, dada yake alitoroshwa na jamaa wa huko huko kwao, na aliishi na mumewe kwa muda mrefuu mpaka akazlishwa watoto 2 then alipoenda "kujisalimisha" alipangiwa mahari ya sh.laki sita tu, na jamaa alilipa laki 4 na wanaishi huko Nyakanazi!
Dada yao mwingine, aliolewa na mtu wa karibu na Kijijini kwao, (huyo alikataa kwenda shule kwa ajili ya jamaa, yaani aliishia form 3) jamaa aliishia kulipishwa faini ya mbuzi 2 na mahari ya laki 6 pia!
Mama mtoto anajiuliza pia kwamba kwanini sisi anatuwekea uzibe na kuonyesha chuki ya wazi kiasi cha kutudhalilisha? Ananiambia hayupo tayari kuachana na mimi hata kama baba akimkataa (na hili naliona kabisa namna anavyokuwa upande wangu) lakini akili inaniambia, inawezekanaje kutengeneza undugu wa aina hii?
Nafika mahali naanza kuhisi pengine mzee ana chuki na watu wasio wa kabila lake tu?