Kasanzu The Great
JF-Expert Member
- Dec 21, 2013
- 310
- 223
Mkuu kwenda na bro wa 50s of age awe mhuni?Uko sahihi sana. TheMnyonge ame apply u town sana sana kitu ambacho kwa wazee hasa vijijini ni ngumu kueleweka. Ndoa ni ishu za kimila sana wewe sio wa ku resolve hizo mambo hssa ukizangatia ulishamtia mimba mtoto wa watu kitu ambacho ni kosa kubwa sana ingawa kimjin mjin tumeamua kulipotezea tu ila kwakifupi ulikosea. Msafara mzima wa mahali mko masela hakuna hata mama mtu mzima wala mashangazi? Kubali tuu kuwa mlienda kihuni sana
Kabisa aisee, yaani kwa uchumi huu nichukue baba, mama, shangazi, mjomba, mshenga , dada ,sijui mshenga na kaka, tunaenda kujitambulisha na kulipa mahari?Mkuu maisha yamebadilika, basi azalishwe huyo mtoto wako ubaki nae hapo nyumbani.
Maswala ya watu kwenda kujionesha Huwa yanachangiwa na sababu nyingi Uchumi ukiwa Moja ya sababu.
Naogopa wasije wakamuua kweli ili tu wanikomoe, hawashindwi binadamu hawa!Safe place ipi ikiwa wazazi watakana kutambua hiyo ndoa?
Wale huwa wanasubiri mtoto wao afariki ili wakatae kupokea mwili na kudai uwarudishie mtoto wao akiwa hai kama ulivyomchukua
Kigoma ni hatari, narudi tena ni hatari
Vumilia hivyo hivyo mzee akifa ndo ufunge ndoaTulienda na gari tukaiacha mjini, kutoka mjini kwenda huko Kijijini tulikodi boda boda kwani njia ni mbaya mno!
Nakuelewa mdogo angu. Hawaja kufanyia fair kabisaaa nakubaliana na wewe na uzur hata huyo mshenga alikua na wisdom sana .Ila sasa ambacho mimi nimejaribu ku focus ni kwenye tamaduni zetu kiafrika.Na hiki ndio sabab kwel vijana wengi hukacha kuoa kwakua customs and tabboos zetu haziko friendlyMkuu kwenda na bro wa 50s of age awe mhuni?
Achilia mbali hilo, mshenga tumemuomba mwenyeji wa huko huko, ili tusiharibu!
Lakini zaidi sana, kwa sisi tu nauli imekata zaidi ya 600k, tungeongezeka 2 tu (yaani shangazi na mjomba) kama unavyosema, nauli ingekuwa 1.2M
Kwa hali ya uchumi wangu na mazingira yalivyo walipaswa kuizingatia zaidi dhamira yangu kwao kuliko kuangalia makosa yangu na binti yao, (kwani makosa tulifanya wote)
Hizi tabia za kukandamiza vijana wenye nia nzuri na kuwanyanyasa ndo kunafanya wengine wakimbie kuanzia mimba, mpaka wapenzi wenyewe, na kuongeza idadi ya watoto wanaokosa malezi ya pande mbili.
Kwa mfano mimi nikiwa na roho ndogo, nikaamua kutokwenda tena na kuachana na mtoto wao, mwanangu atateseka mno, lakini pia mtoto wao atateseka pia kwa sababu ambazo hazina ulazima kabisa!
Kunitukana, kunidhalilisha kwa sababu ya eti nilizaa na mtoto wao inawaongezea nini? Inafuta makosa yetu? Kwa kunidhalilisha inafanya binti yao arejee kuwa bikra? (Obvious jibu ni hapana)
Acha hayo matusi na kunidhalilisha, wanapotaja mahari ya kunikomoa (ambayo mimi sina) wanataka nishindwe kulipa then niwaachie binti yao, wakibaki na binti yao wananufaikaje naye? wanaona bora waendelee kulea mtoto na mjukuu wao kwa kuwa tu, tulikosea? Yaani kila nikitafakari sipati majibu kabisa
Sasa unaponitimua kwako naishije na binti yako?Kosa la huyo binti uliyemzalisha na unataka kumuacha ni lipi??
Mbona vijana hamuishiwi sababu za kuongeza singo maza mtaani??
Umemchakaza binti mpaka umemzalisha halafu unamuacha kisa baba yake aisee, unamuoa binti au baba yake.
Umtie mimba binti akiwa kwao bila ndoa halafu baba afurahie kisa umekuja na mkaja wa mama na mbuzi watatu??
Acha dharau kijana, hata mimi babu yangu angekutoa baru, eti unampangia mahari aiseee.
Ukimuacha binti nae kwa hasira akakumwagia tindikali mtaanza lawama za kusema wanawake wana roho mbaya.
Wazee wetu tunapaswa kuwashauri saba kwenye maeneo haya, angalau watambue kwamba vijana wao kwa nyakati hizi tuna changamoto nyingi mno linapokuja swala la kutengeneza familia,watuvumilie kwa madhaifu yetu na watutie moyo tunapofanya maamuzi yenye kujenga!Nakuelewa mdogo angu. Hawaja kufanyia fair kabisaaa nakubaliana na wewe na uzur hata huyo mshenga alikua na wisdom sana .Ila sasa ambacho mimi nimejaribu ku focus ni kwenye tamaduni zetu kiafrika.Na hiki ndio sabab kwel vijana wengi hukacha kuoa kwakua customs and tabboos zetu haziko friendly
Mzee wa watu hana makosa, wewe ndiye umepuyanga kwa kudhani kuwa unawamudu kwa kukaa na binti yao kumzalisha kisha kwenda kwao kwa kiburi. Unaenda kulipa mahari na bro? Huna wazee wala shangazi? Trna huyo mzee umemfanyia dharau sana.Nimekuwa kwenye mahusiano na mwanamke kutoka Kigoma tangu 2020, tulikutana chuo, na penzi likakolea haswaa!
Kipindi cha Covid penzi lilinoga zaidi kwani "Working from home" ilifanya muda wote tuwe pamoja, ilikuwa mwendo wa kwenda sokoni kununua mazaga zaga pamoja, tinaweka ndani then kila baada ya mlo ni mnyanduano tu, hatimaye binti akashika mimba!
Baada ya mimba kufikisha miezi minne bibie akaniambia ni bora aende kwao kwanza kwani kubaki tukiwa wawili hatuwezijua complications za mimba, nilikubaliana nae, nikajipiga kwa kadri ya uwezo wangu nikamkatia tiketi na vizawadi kidogo vya wazee akaenda kwao!
Akiwa kwao mawasiliano yetu yalikuwa vizuri kabisa mpaka akajifungua salama salmin, na mimi niliwajibika haswa mpaka dk. ya mwisho, hatimaye tukapata mtoto wa kiume.
Bibie baada ya mtoto kufikisha miezi 6 bila mimi kwenda kujitambulisha akatoa wazo la kurudi kwangu kwani alikuwa amechoka kuishi nyumbani kwao, nikamkaribisha tukaendelea na maisha ya sogea tuishi.
Mwaka jana December, ilitokea msiba kwao akalazimika kwenda msibani, nikamfanyia maandalizi vizuri kabisa, akaondoka.
Amekaa huko tangu December, mpaka juzi nilipoamua kufuata taratibu za kwenda kwao ili tusiendelee kuishi kimya kimya (tufanye kuwa official), nikajiandaa kwa mambo kadhaa kama nilivyokuwa nimeng'atwa sikio na mpenzi wangu.
Nimeanza safari kutoka Dar kwenda Kigoma (kwao), nikiwa nimeambatana na brother wangu wa damu, aisee kwao ni mbali, maana tulitembea siku 2 njiani, tulipofika mjini, safari ya kwenda kwao ikachukua masaa mengine 8, vumbi kali hatari, tulipofika Kijijini kwao tukaambiwa Burundi ni mwendo wa kutembea nusu saa tu.
Brother akaniuliza, "Hivi dogo hukuona wanawake mikoa yote tuliyopita mpaka kuja huku?" Nikamwambia mapenzi yana nguvu bro, sikuwahi kufikiria kama kuna siku ningesafiri umbali namna hii kufuata mwanamke tu. Tulipofika mjini tulitafuta mzee mwenyeji, anayejua mila na desturi za Kiha ili mambo yasiwe magumu.
Basi bwana, tumefika pale tumepokelewa vizuri wakaandaa utaratibu wa mjadala, mshenga akatambulisha na kuanza mazungumzo rasmi, hapo nilikuwa na zawadi ya baba mkwe na mama mkwe, nilinunua tangu Dar kwa upendo kabisa.
Wakataja kiasi cha mahari kuwa wanataka mil. 4.5, hapo tukashtuka kweli, kabla hatujakaa sawa wakataja mkaja wa mama sh. laki saba, jumla wanataka 5.2 Milioni!
Yule mzee tuliyeenda naye akaomba twende nje kwa mazungumzo, akatuuliza kama tulipewa mwongozo na tuliyekwenda kumuoa, nikamjibu ndiyo (alisema mahari kwao haizidi Milioni moja) na mkaja wa mama huwa ina-range kuanzia 100k - 200k, na mimi niliandaa 200k kama mkaja wa mama! Mzee akasema hapa kuna tatizo, huku haijawahi kutokea mahari kubwa kiasi hiki, akasema tutasimamia kwenye hiyo 1M na mkaja wa mama 200k, tukarudi ndani!
Mzee (mshenga) akaanza kuzungumza, kuwa sisi tuna mahari 800k na mkaja wa mama 100k, lakini pia tuna zawadi kwa ajili ya baba na mama, ambazo si sehemu ya mahari, ni zawadi tu ya kijana wetu kwenu, mzee akatoa zile zawadi akaweka mezani.
Mshenga wao akashukuru na kuanza kuzungumzia mahari yetu kuwa angalau tufanye mahari mil.4 mkaja wa mama 500k.
Kabla hajamaliza akasimama baba mkwe, akionyesha kukasirika akasema "Sitaki mjadala wa kitoto hapa, mimi ndiye baba wa x, mkaja wa mama laki 5, mahari yangu nataka Milioni 4, Sitaki mjadala wala kusikia kupunguziana, kwanza unabeba zawadi kutuletea nani amekutuma utununulie, tumekuomba sisi utuletee zawadi zako?"
"Kwanza huyu kijana anadharau sana, tangu mtoto azaliwe hajawahi kufika hapa nyumbani, anaishia kumtumia mwenzake pesa tu, sisi hajawahi kututumia pesa hata mara moja, tumepata msiba hajawahi kuja kutupa pole zaidi ya kupiga visimu vyake tu, sasa mimi nimeshasema mkaja wa mama laki tano, mahari Milioni 4, sitaki mjadala!"
Aisee nilijikuta nimejaa hasira mpaka basi, mshenga wetu akatutaka twende nje, akasema "huyu mzee inaonekana ana lake jambo, tusiingie kwenye mtego wake, iweni wapole, tuondoke salama, watu wa huku ni hatari sana, tukiwa na hasira tunaweza tusirudi salama, hii si dalili nzuri."
Tukajadili tuvyojiandaa pale, mzee akasema muhimu tuanze na mkaja wa mama, tuwawekee hiyo 500k then tutawapa faini za mbuzi mbuzi, na vingine vidogo vidogo, baada ya hapo mahari tuwaambie kuwa tunaenda kuitafuta then mtaangalia wenyewe baada ya kufika nyumbani!
Tuliporudi ndani tukakuta mzee anaonyesha kuwa na hasira hasira tu, kiasi kwamba mshenga wao akawa ameduwaa tu, basi mshenga wetu akaanza kujitetea pale, akaweka mezani Tsh. 500k mkaja wa mama, akawaambia mbuzi watatu wa uchafuzi 300k, sijui koti la mjomba, mara blanketi ya wazee na vikolo kolo vingine kwa Kadri ya taratibu zao, ile pesa tuliyoenda nayo ikawa imekata!
Muda huo wote nina hasira vibaya mno, ila najitahidi kuificha japo mpenzi wangu aligundua kabisa kuwa nimechukia. Tukawaambia hiyo mil. 4 tunaenda kuitafuta, mzee akasema "Mkaitafute muilete hapa, au mutanitumia kwenye simu," tukawaambia sawa.
Muda wa kutoka nikakuta mpenzi wangu ameshabeba mabegi anataka tuondoke wote, nikamwambia hapana unapaswa kubaki nitakuja kuwachukua nikimalizia mahari. Akagoma, akawa analia wakati wote akiwa amenikumbatia, anaomba radhi kwa kilichotokea ila anaomba tuondoke wote, yeye hawezi kubaki kijijini tena. Nikamwambia hapana, unapaswa kubaki mpaka tumalizane na mzee, akagoma kata kata, akawa amepiga magoti huku amekumbatia miguu yangu, machozi yanamtoka tu!
Mzee wake alipotoka akaona mwanaye analia akasema "Kama mnaondoka wote nendeni tu!" Mara mama mkwe akaja na dogo (mtoto wangu), akamshusha nilipokuwa, nikambeba mtoto nikamwambia mama mtoto asimame, bro na mshenga wetu wakaniita pembeni, mshenga akasema tuondoke nao, tukimuacha na wakahisi kuwa kuna dalili za sisi kutorudi, watamuua huyu mtoto.
Basi kishingo upande, tukawakubalia kuondoka nao, mama mkwe akaleta maharage na jogoo akataka tuondoke navyo, nikakataa kuchukua, nikamwambia tutabeba wakati mwingine, akagundua bado nina hasira. Akamuita mtoto wake, akamwambia "Mwambie mumeo amsamehe bure baba yako, amekosea sana, na mimi mama naomba atusamehe tu."
Tukaondoka zetu, kichwani nikiwa nimejaa mawazo mengi mno, kiasi kwamba sikuweza kujua niamue nini. Tumefika Dar lakini moyoni nimejikuta sina tena interest ya kutengeneza undugu na familia ya mpenzi wangu, japo yeye binafsi hana shida, lakini kwa namna tulivyopokelewa na tulivyoondoka, nilijisemea moyoni kwamba sitokaa nirudi Kigoma, wala sitokaa nipeleke hiyo mahari waliyosema.
Nasubiri mwanangu akuekue kidogo nimwambie mama mtoto kwamba hakuna namna naweza kuunganisha undugu na familia yake, japo namhurumia ila ndiyo hivyo tena.
Kweli tembea uone, all the way from Dar to Kigoma, naenda kukutana na aibu tu, anyways.
Umeokotwa tu nawewePole mkuu. Lakini hiyo mahari nadhani ni reasonable hasa ukizingatia ulimzalisha mtoto wao na ulichelewa kwenda kujitambulisha! Mimi sijamzalisha wa kwangu lakini nimepigwa mahari 3.8 M na wanyakyusa wa Simike wale!
Sema nini, usimuache huyo manzi.Usimuache kwa shida hiyo labda kama zipo au zitajitokeza zingine..Ila kwahilo hana kosa na hakupenda kilichotokea ndio maana akaamua kuondoka.Pia kitendo cha mama mkwe pia kujua walikukosea ni ishara tosha kuwa hata dingi ujumbe huo ataupata na atajua kuwa alizingua. Endelea na kuwa nae.Wazee wetu tunapaswa kuwashauri saba kwenye maeneo haya, angalau watambue kwamba vijana wao kwa nyakati hizi tuna changamoto nyingi mno linapokuja swala la kutengeneza familia,watuvumilie kwa madhaifu yetu na watutie moyo tunapofanya maamuzi yenye kujenga!
Kutudhalilisha na kutukandamiza namna hii kunafanya tujione wajinga kwenda ukweni, na kudhani kuwa ujanja ni kukimbia unapotia mimba mtoto wa mtu, kitu ambacho sio kizuri kabisa!
Tunadharau taratibu siku hizi ndio maana yanatukuta haya.Mama hana shida. Hivyo ushauri wako usijumuishe wazazi wote.
Mama yupo pamoja na bintie.
Shida ipo kwa baba.
Sent from my SO-01J using JamiiForums mobile app
Jf bhana...Aiseeh umeingia cha kike,mambo ya kuokotana nabkuanza kuishi kienyeji ndo matokeo yake hayo[emoji120]mzee anataka milion 4 yake lasivyo utakiona cha mtema kuni,ila hongera kutuongezea mrundi mwingine Tanzania kama maguful[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Acha ukoloni mzee wangu.Mwanaume gani HUNA KIFUA? Be gentlemen, hii issue ndogo sana sana sema umeikuza sana. Wewe subiri upate mtoto wa kike umsomeshe hadi Universitty atokee Bazazi kama wewe ampachike mimba, binti ajifungue then linakuja kutokea mtoto anakrbia mwaka. Aysee mimi ntakuttwanga risasi mamaaae zako. Mwanangu Chuo kikuu nilimtuma Degree siyo MIMBA yako. Huna nidhamu wewe kijana huyo mzee hajakosea.
Ukimuacha huyo binti kuna mawili laaana ya Mke imuandame au Laana ya mzee ikuandame kimila zaidi. Hupitishi round. RIP in advance
Mahari haina kiwango maalum kila koo na familia hujipangia.Sasa unaponitimua kwako naishije na binti yako?
Mahari no formality ya kimila kuunganisha koo na kubariki watoto wanapokwenda kuanza maisha yao, mahari sio biashara ya kujipatia kipato, badili hiyo mindset, otherwise utajikuta unalea watoto wako, wanazalishwa na unaanza kulea na watoto wa watoto wako!
Nani kakwambia dunia imebadilika dunia iko vilevile na ardhi ndo ileile na majira ni yaleyale kuna asubuhi, mchana, jioni na usiku na hewa tunayoivuta ni ileile na mvua ndo zilezile yaani mm ungemtia mimba mwanangu umemzini, umemzalisha alafu unaleta story za dunia kubadilika nakukodia mabaunsa wakunyandue bila mafuta acheni kuharibu watoto fateni taratibu muoe.Acha ukoloni mzee wangu.
Dunia imebadilika.
Tusitishane bhana, kama wanaona watoto wao ni mitaji acha tuwaachie tu! Siwezi kulipa 4M mimi, siwezi n'a hiyo pesa sina!Mzee wa watu hana makosa, wewe ndiye umepuyanga kwa kudhani kuwa unawamudu kwa kukaa na binti yao kumzalisha kisha kwenda kwao kwa kiburi. Unaenda kulipa mahari na bro? Huna wazee wala shangazi? Trna huyo mzee umemfanyia dharau sana.
Halafu kwani hujui mahari za waha? Mimi nilimzalisha binti wa kiha ingawa nilikuwa kwenye process. Nakumbuka nilienda kulipa mahari nikiwa tayari nina details zote kutoka kwa wazee wake na ndugu. Nilipeleka 3M casha ikijumuisha vikorombwezo vyote. Waha ukienda kulipa mahari kwao hadi bajeti ya vyakula watakavyokula ni juu yako.
Ila nashukuru binti yao ni mzuri sana, mtamu sana figa lake sasa na uzuri ana nidhamu sana. Nimekaa naye muda wa kutosha kabla sijaamua jumla na hajawahi kuonyesha dharau kwangu.
Nenda kakamilishe uliyoagizwa kwa dharau ulizoonyesha ama uanze kupata mikosi na kama huwajui waha basi nenda kigoma uone mtu anatumiwa radi inamfuata hata akiwa chini ya meza.
Mimi sikuhitaji kupokelewa kifalme mkuu, nilienda nikiwa najua kuna mahali tulikosea, lakini siwezi kukubali kulipa mahari ya kunikomoa, ukichanganya na maneno ya dharau na kunidhalilisha, kwa kufanya hivyo inawanufaisha nini?Mahari haina kiwango maalum kila koo na familia hujipangia.
Kwa story yako hakuna mahali baba wa binti kakufukuza ni wewe na hasira zako, ulitegemea upokelewe kama mfalme wakati umeidharau familia ya ukweni.
Na hapo humkomoi baba mkwe ila unamkomoa huyo mwanamke maana inaonekana hapendi kuishi kijijini, aking'ang'ania kuishi mjini ni mateso kwake kama alikua anakutegemea wewe kwa kila kitu.
Acha kukimbia majukumu lea familia yako, unaacha kuwaza maridhiano unaleta hasira na wewe. Yani huyo mkwe wako na wewe ni sawasawa kabisa hamna tofauti.