Nimetoka ukweni Kigoma, ila kama hii ndiyo aina ya wazee acha wabaki na watoto wao!

Hivi vitisho vya kipuuzi sana, sasa wamuue mtoto kwa sababu ya wao kutaka pesa nyingi?
Kwani kuoana ni miradi mpaka ihusishe mauaji?
Kama ndivyo walivyo inaniongezea sababu ya kuwakataa tena na kutojenga undugu na watu wa aina hii!
Mkuu kule sio pa kujenga mazoea, ndio maana ndugu zako wakakwambia kabisa. Shikilia msimamo wako, hakuna atakaeishi milele. Bora kufa kuliko kujenga mahusiano na muha
 
TheMnyonge pole sana,naamini una nia nzuri ila methodology unayotumia ndo haijazaa matunda.
Pia kuna tatizo nailiona kwako,umeleta mada,acha watu wakushauri,lkn naona unabishana nao,ni kama una maamuzi yako tayari,sasa kwa nn umeileta hapa?
 
HIYO NI BUHIGWE MOJA

Yes juzi nilienda huko ni mbali Heru ushingo nikatokea huru juu aiseeh acha tu jamani hili nchi ni jitu kuuubwa sana Buhigwe ndo kwao mpango wameanza kumtengenezea barabara

Yote kwa yote ba mkwe ni \|*}%{
Maisha ya kule ni magumu kuliko jiwe ni halali binti akulilie usimuache kule hamna
 
Kama mama mkwe hana shida na mke hana shida basi achana na huyo dingi. Ni stress tu za maisha.

Tunza familia yako achana na huyo dingi.

Ma mkwe keshachukua chake shida aitoe wapi tena?

Dingi anataka kwenye mahari awanange majirani na wazee wenzie sasa matarajio wamekuwa tofauti ko lazima ajae sumu
 
Aiseeh watu hawana Shukrani yaani umeamua ujulikane na zawadi umewapelekea bado dingi anadai nani alikutuma zawadi?

Upo sahihi kujaa gas mkuu na tena kaa na binti yao hadi wao watakapoomba po!

Kikubwa ushawajua hayo mengine kwa baadae waambie mambo yamekuwa magum hata ile mahari nilokupa ukaikataa muda ule kwa sasa sina hadi yeye akuombe samahani kwa kukukwaza ugenini!
 
Hilo la kuua mtoto si kweli.Mambo huwa complicated unapozaa kabla ya kutimiza taratibu.Punguza hasira.Naturally wababa huwa overprotective kwa Binti zao. Jipe muda, baadaye utagundua huyo Mzee ni mtu poa kuliko unavyodhani. Utaratibu mzuri wa kuoa huku ni kwamba Binti stoke mbichi Nyumbani. Wee umefanya uchafuzi halafu unataka fair? Kila kabila na taratibu zake. Jipe muda utagundua. Mwenyezi Mungu awajalie Kila lililo la heri kwenye familia Yako changa.
Vijana wanaolelewa hovyo kimjinimjini ndiyo shida.Huku kwetu mikoani watu tupo kitamaduni zaidi,ukija njoo kwa nidhamu ya juu sana.
 
[emoji28]
tapatalk_1584559501930.jpg
 
Hivi vitisho vya kipuuzi sana, sasa wamuue mtoto kwa sababu ya wao kutaka pesa nyingi?
Kwani kuoana ni miradi mpaka ihusishe mauaji?
Kama ndivyo walivyo inaniongezea sababu ya kuwakataa tena na kutojenga undugu na watu wa aina hii!
Linda familia yako kijana, wewe hutakua na undugu na hao watu upande wa kikeni.

Hata mwanao ndgu zake ni wa kiumeni si kikeni ndio maana anaitwa jina lako.
 
TheMnyonge pole sana,naamini una nia nzuri ila methodology unayotumia ndo haijazaa matunda.
Pia kuna tatizo nailiona kwako,umeleta mada,acha watu wakushauri,lkn naona unabishana nao,ni kama una maamuzi yako tayari,sasa kwa nn umeileta hapa?
Nimekupata, japo nashangazwa na baadhi ya watu wanaosema sijui ningewabeba wazazi wangu na blah blah kibao!

Nimeeleza kwa kina nilimchukua Kaka yangu mkubwa (over years) kutoka Dar mpaka Kigoma, then kwa kujua kwamba kule ni ugenini, hatujui taratibu zao, tukamuomba mzee mwenyeji wa huko ili atusaidie ku-cope na mila na desturi zao, lakini yakatokea yaliyotokea pasipokujali dhamira ya sisi kufika pale!

Sijaleta mada ili watu waniamulie cha kufanya, isipokuwa nimetoa hiyo experience walau tunapozeeka tusifanye upuuzi wa namna hii, mahari si kitu cha kukomoana, kujenga undugu na linapaswa kuwa jambo la heri, sio shari!
 
Nimekuwa kwenye mahusiano na mwanamke kutoka Kigoma tangu 2020, tulikutana chuo, na penzi likakolea haswaa!

Kipindi cha Covid penzi lilinoga zaidi kwani "Working from home" ilifanya muda wote tuwe pamoja, ilikuwa mwendo wa kwenda sokoni kununua mazaga zaga pamoja, tinaweka ndani then kila baada ya mlo ni mnyanduano tu, hatimaye binti akashika mimba!

Baada ya mimba kufikisha miezi minne bibie akaniambia ni bora aende kwao kwanza kwani kubaki tukiwa wawili hatuwezijua complications za mimba, nilikubaliana nae, nikajipiga kwa kadri ya uwezo wangu nikamkatia tiketi na vizawadi kidogo vya wazee akaenda kwao!

Akiwa kwao mawasiliano yetu yalikuwa vizuri kabisa mpaka akajifungua salama salmin, na mimi niliwajibika haswa mpaka dk. ya mwisho, hatimaye tukapata mtoto wa kiume.

Bibie baada ya mtoto kufikisha miezi 6 bila mimi kwenda kujitambulisha akatoa wazo la kurudi kwangu kwani alikuwa amechoka kuishi nyumbani kwao, nikamkaribisha tukaendelea na maisha ya sogea tuishi.

Mwaka jana December, ilitokea msiba kwao akalazimika kwenda msibani, nikamfanyia maandalizi vizuri kabisa, akaondoka.

Amekaa huko tangu December, mpaka juzi nilipoamua kufuata taratibu za kwenda kwao ili tusiendelee kuishi kimya kimya (tufanye kuwa official), nikajiandaa kwa mambo kadhaa kama nilivyokuwa nimeng'atwa sikio na mpenzi wangu.

Nimeanza safari kutoka Dar kwenda Kigoma (kwao), nikiwa nimeambatana na brother wangu wa damu, aisee kwao ni mbali, maana tulitembea siku 2 njiani, tulipofika mjini, safari ya kwenda kwao ikachukua masaa mengine 8, vumbi kali hatari, tulipofika Kijijini kwao tukaambiwa Burundi ni mwendo wa kutembea nusu saa tu.

Brother akaniuliza, "Hivi dogo hukuona wanawake mikoa yote tuliyopita mpaka kuja huku?" Nikamwambia mapenzi yana nguvu bro, sikuwahi kufikiria kama kuna siku ningesafiri umbali namna hii kufuata mwanamke tu. Tulipofika mjini tulitafuta mzee mwenyeji, anayejua mila na desturi za Kiha ili mambo yasiwe magumu.

Basi bwana, tumefika pale tumepokelewa vizuri wakaandaa utaratibu wa mjadala, mshenga akatambulisha na kuanza mazungumzo rasmi, hapo nilikuwa na zawadi ya baba mkwe na mama mkwe, nilinunua tangu Dar kwa upendo kabisa.

Wakataja kiasi cha mahari kuwa wanataka mil. 4.5, hapo tukashtuka kweli, kabla hatujakaa sawa wakataja mkaja wa mama sh. laki saba, jumla wanataka 5.2 Milioni!

Yule mzee tuliyeenda naye akaomba twende nje kwa mazungumzo, akatuuliza kama tulipewa mwongozo na tuliyekwenda kumuoa, nikamjibu ndiyo (alisema mahari kwao haizidi Milioni moja) na mkaja wa mama huwa ina-range kuanzia 100k - 200k, na mimi niliandaa 200k kama mkaja wa mama! Mzee akasema hapa kuna tatizo, huku haijawahi kutokea mahari kubwa kiasi hiki, akasema tutasimamia kwenye hiyo 1M na mkaja wa mama 200k, tukarudi ndani!

Mzee (mshenga) akaanza kuzungumza, kuwa sisi tuna mahari 800k na mkaja wa mama 100k, lakini pia tuna zawadi kwa ajili ya baba na mama, ambazo si sehemu ya mahari, ni zawadi tu ya kijana wetu kwenu, mzee akatoa zile zawadi akaweka mezani.

Mshenga wao akashukuru na kuanza kuzungumzia mahari yetu kuwa angalau tufanye mahari mil.4 mkaja wa mama 500k.

Kabla hajamaliza akasimama baba mkwe, akionyesha kukasirika akasema "Sitaki mjadala wa kitoto hapa, mimi ndiye baba wa x, mkaja wa mama laki 5, mahari yangu nataka Milioni 4, Sitaki mjadala wala kusikia kupunguziana, kwanza unabeba zawadi kutuletea nani amekutuma utununulie, tumekuomba sisi utuletee zawadi zako?"

"Kwanza huyu kijana anadharau sana, tangu mtoto azaliwe hajawahi kufika hapa nyumbani, anaishia kumtumia mwenzake pesa tu, sisi hajawahi kututumia pesa hata mara moja, tumepata msiba hajawahi kuja kutupa pole zaidi ya kupiga visimu vyake tu, sasa mimi nimeshasema mkaja wa mama laki tano, mahari Milioni 4, sitaki mjadala!"

Aisee nilijikuta nimejaa hasira mpaka basi, mshenga wetu akatutaka twende nje, akasema "huyu mzee inaonekana ana lake jambo, tusiingie kwenye mtego wake, iweni wapole, tuondoke salama, watu wa huku ni hatari sana, tukiwa na hasira tunaweza tusirudi salama, hii si dalili nzuri."

Tukajadili tuvyojiandaa pale, mzee akasema muhimu tuanze na mkaja wa mama, tuwawekee hiyo 500k then tutawapa faini za mbuzi mbuzi, na vingine vidogo vidogo, baada ya hapo mahari tuwaambie kuwa tunaenda kuitafuta then mtaangalia wenyewe baada ya kufika nyumbani!

Tuliporudi ndani tukakuta mzee anaonyesha kuwa na hasira hasira tu, kiasi kwamba mshenga wao akawa ameduwaa tu, basi mshenga wetu akaanza kujitetea pale, akaweka mezani Tsh. 500k mkaja wa mama, akawaambia mbuzi watatu wa uchafuzi 300k, sijui koti la mjomba, mara blanketi ya wazee na vikolo kolo vingine kwa Kadri ya taratibu zao, ile pesa tuliyoenda nayo ikawa imekata!

Muda huo wote nina hasira vibaya mno, ila najitahidi kuificha japo mpenzi wangu aligundua kabisa kuwa nimechukia. Tukawaambia hiyo mil. 4 tunaenda kuitafuta, mzee akasema "Mkaitafute muilete hapa, au mutanitumia kwenye simu," tukawaambia sawa.

Muda wa kutoka nikakuta mpenzi wangu ameshabeba mabegi anataka tuondoke wote, nikamwambia hapana unapaswa kubaki nitakuja kuwachukua nikimalizia mahari. Akagoma, akawa analia wakati wote akiwa amenikumbatia, anaomba radhi kwa kilichotokea ila anaomba tuondoke wote, yeye hawezi kubaki kijijini tena. Nikamwambia hapana, unapaswa kubaki mpaka tumalizane na mzee, akagoma kata kata, akawa amepiga magoti huku amekumbatia miguu yangu, machozi yanamtoka tu!

Mzee wake alipotoka akaona mwanaye analia akasema "Kama mnaondoka wote nendeni tu!" Mara mama mkwe akaja na dogo (mtoto wangu), akamshusha nilipokuwa, nikambeba mtoto nikamwambia mama mtoto asimame, bro na mshenga wetu wakaniita pembeni, mshenga akasema tuondoke nao, tukimuacha na wakahisi kuwa kuna dalili za sisi kutorudi, watamuua huyu mtoto.

Basi kishingo upande, tukawakubalia kuondoka nao, mama mkwe akaleta maharage na jogoo akataka tuondoke navyo, nikakataa kuchukua, nikamwambia tutabeba wakati mwingine, akagundua bado nina hasira. Akamuita mtoto wake, akamwambia "Mwambie mumeo amsamehe bure baba yako, amekosea sana, na mimi mama naomba atusamehe tu."

Tukaondoka zetu, kichwani nikiwa nimejaa mawazo mengi mno, kiasi kwamba sikuweza kujua niamue nini. Tumefika Dar lakini moyoni nimejikuta sina tena interest ya kutengeneza undugu na familia ya mpenzi wangu, japo yeye binafsi hana shida, lakini kwa namna tulivyopokelewa na tulivyoondoka, nilijisemea moyoni kwamba sitokaa nirudi Kigoma, wala sitokaa nipeleke hiyo mahari waliyosema.

Nasubiri mwanangu akuekue kidogo nimwambie mama mtoto kwamba hakuna namna naweza kuunganisha undugu na familia yake, japo namhurumia ila ndiyo hivyo tena.

Kweli tembea uone, all the way from Dar to Kigoma, naenda kukutana na aibu tu, anyways.
Pole hapo atakayeteseka ni mtoto wako tuu huyo pole
 
Sijaona shida ya Baba mkwe hapo.
Nimekuona wewe tuu sasa hasira zimetoka wapi, unavyoonekana wewe ni mtu mwenye hasira sana.
 
mama firstborn

Daa kuna rafiki yangu mmoja wa kiume alinisimulia kuhusu hiyo.
Yeye Baba yake na mama yake walimzaa nje , baadae baba akaoa huko na mama akaolewa huko.

Daaa aliniambia jinsi alivyoishi alipata shida sana upande wa saikologia,
Akienda kwa Baba anamkuta Baba yupo na mkewe na watoto wake, mbaya zaidi watoto wake wamefanana kinoma,
Akienda kwa mama yake anamkuta mama yupo na mume mwingine na watoto wao.
Yeye yupo kati , aliniambia kuwa hawajawahi kumtesa hata kidogo ila situation kama hio daa ailimuaribu kisaikolojia kabisa,
Aliniambia tuj usijaribu kuzaa nje bro mwenye kuathirika ni mtoto sio nyie wazazi. Aliniambia yeye amepata huo uzoefu hatakuja kufanya hivyo hata siku moja, ikitokea anamuoa huyo huyo kwa gharama yoyote ile.
Ila alinkambia ata akija kuoa akichepuka condom ni lazima atumie ili asitengeneze mtoto nje.
Yeye akabaki kwenda kwa shangazi yake, na aunt yake akuwa na mume, alikuwa na mtoto mmoja wa kike tuu( single mother),
Ndo akawaanashida huko.

TheMnyonge
Pole sana , hapo mtoto wako ndo wakuteseka hujui mke utakaye muoa atakuwaje bro.
Pole sana .
 
Mkuu kwenda na bro wa 50s of age awe mhuni?
Achilia mbali hilo, mshenga tumemuomba mwenyeji wa huko huko, ili tusiharibu!
Lakini zaidi sana, kwa sisi tu nauli imekata zaidi ya 600k, tungeongezeka 2 tu (yaani shangazi na mjomba) kama unavyosema, nauli ingekuwa 1.2M

Kwa hali ya uchumi wangu na mazingira yalivyo walipaswa kuizingatia zaidi dhamira yangu kwao kuliko kuangalia makosa yangu na binti yao, (kwani makosa tulifanya wote)

Hizi tabia za kukandamiza vijana wenye nia nzuri na kuwanyanyasa ndo kunafanya wengine wakimbie kuanzia mimba, mpaka wapenzi wenyewe, na kuongeza idadi ya watoto wanaokosa malezi ya pande mbili.

Kwa mfano mimi nikiwa na roho ndogo, nikaamua kutokwenda tena na kuachana na mtoto wao, mwanangu atateseka mno, lakini pia mtoto wao atateseka pia kwa sababu ambazo hazina ulazima kabisa!

Kunitukana, kunidhalilisha kwa sababu ya eti nilizaa na mtoto wao inawaongezea nini? Inafuta makosa yetu? Kwa kunidhalilisha inafanya binti yao arejee kuwa bikra? (Obvious jibu ni hapana)

Acha hayo matusi na kunidhalilisha, wanapotaja mahari ya kunikomoa (ambayo mimi sina) wanataka nishindwe kulipa then niwaachie binti yao, wakibaki na binti yao wananufaikaje naye? wanaona bora waendelee kulea mtoto na mjukuu wao kwa kuwa tu, tulikosea? Yaani kila nikitafakari sipati majibu kabisa
Kamanda umenena vyema. Bila shaka unajua kitu cha kufanya baada ya hilo sekeseke ili kuendelea kulinda familia na mapenzi yako kwa binti.
Fanya hivyo kaka...don't lose hope. Kumbuka your present situation is not your final destination.
 
Mfano wewe mtoto wako azalishwe bila ndoa itafurahia ? Na aje kuishi na mwanaume bila kumjua na aje kwako kujitambulisha na vizawadi vya kuwadanganya kama watoto au familia yenye dhiki sana.
Daaaaa
 
Yani we jamaa umekaa na mtoto wa watu, umemzalisha, umemtuma kwao ili uje kukamilisha taratibu za kuoa, wewe umemchukua ndugu yako mmoja eti mnaenda kujadili mahari, it doesn't make any sense, ni dharau na mazoea hayo. Kwani huko kwenu taratibu za kuoa zikoje? Au ndo ukishampiga mtoto wa mtu mimba ndo unatoka na rafiki yako kwenda kwa babamkwe kuuliza ni shangapi?
Ninavyojua mimi TheMnyonge
Ukitanguliza mtu kwanza na kishika uchumba na barua ya kuomba radhi ya kumzalisha binti yao na kuishi nae.
Mambo mengine baadae.
 
Back
Top Bottom