Nimetoka ukweni Kigoma, ila kama hii ndiyo aina ya wazee acha wabaki na watoto wao!

Mbaya zaidi ntalazimika kumuacha mtoto wao kwa makosa ya baba yake
Mkuu pole sana, sidhani kama utakuwa uamuzi mzuri ukimuacha huyo binti while unajua kabisa kuwa mnapendana na yeye na mama ake hawana shida. Shida ipo kwa mzee wake na ushauri aliopewa na rafiki zake katika vilabu vya pombe za kienyeji.😫

Kama usemacho baada ya muda kafunge hata ndoa ya Bomani kuhalalisha mahusiano yenu, nakwambia huyo mzee atakuja kukuomba msamaha mwenyewe baada ya kuona anaelekea kukosa vyote.
 
Hilo la kuua mtoto si kweli.Mambo huwa complicated unapozaa kabla ya kutimiza taratibu.Punguza hasira.Naturally wababa huwa overprotective kwa Binti zao. Jipe muda, baadaye utagundua huyo Mzee ni mtu poa kuliko unavyodhani. Utaratibu mzuri wa kuoa huku ni kwamba Binti stoke mbichi Nyumbani. Wee umefanya uchafuzi halafu unataka fair? Kila kabila na taratibu zake. Jipe muda utagundua. Mwenyezi Mungu awajalie Kila lililo la heri kwenye familia Yako changa.
 
Dogo mpaka utakapoelewa umuhimu wa kushiriki maswala ya kijamii kwenye familia tarajiwa ndipo utakapo acha kuteseka. Kwa mtu anaejielewa ikishatokea mimba tu anajipeleka mwenyewe sio lazima azae na hayo mambo ya mkaja wa mama hii inatolewa kama mwanamke ni bikra mbali na hapo hakuna ujinga kama huo.

Mfano huku kwetu hela ya mama ndio sawa na utakayompa baba bahati nzuri mm ndio nilimtoa bikra wife sikuwa na kinyongo kuitoa lakini ningeleta utata kwamba sijamkuta na bikra alooo wangeishia kula mahari na blangeti la bibi kuhusu shangazi mgao wake upo kwenye hela ya mama kwahyo angekosa.

Na mahari mara nyingi ni ngombe mmoja au wawili ila mahari ya 4m alooo wanakukomoa tu kwakua hukuonyesha ushirikiano. Jitahidi kukaa na wazee wakupe busara na nini cha kufanya kwenye familia ya mke itakusaidia sana asee
 
Kuna baadhi ya Mila na desturi wazee ndio huongea hayo Mambo na kuwekana sawa, kwao n kosa kijana kwenda kuzungumza na mzee. Wenye experience na hili watalielezea zaidi.
Aliyekuwa anaongea nao ni mzee, tena mwenyeji wa huko huko Kigoma, lakini hata kama hakuridhika sisi kwenda (brother angu yupo kwenye 50's by age) kulikuwa na sababu ya kutamka maneno makali na kutaja pesa nyingi kwa command?
 
Umetoa mkaja wa mama hapo ushapata mke.

Achana na huyo baba mkwe mgaigai.
 
Aliyekuwa anaongea nao ni mzee, tena mwenyeji wa huko huko Kigoma, lakini hata kama hakuridhika sisi kwenda (brother angu yupo kwenye 50's by age) kulikuwa na sababu ya kutamka maneno makali na kutaja pesa nyingi kwa command?
Pole Sana mkuu hakuna hiyo sababu na hapo anaeumia zaidi ni binti yake, bro wako amekushaurije baada ya Hilo?
 
Shukuru umepata mtoto salama, umefika Kigoma salama na umerudi Dar salama, mengine yatajulikana mbele ya safari.
 
Easy bro, yule ni hasira za kuonekana kadharaulika kwa muda wote huo.

Achokifanya ni kukomoa.

Sio kwamba familia yake ipo pamoja nae. Ndio maana mama kakuomba radhi.

Ishi na mkeo, jengeni familia yenu. Mama yupo pamoja nanyi.

Usimfanye huyo dada akajuta kukuzalia mtoto.

Sent from my SO-01J using JamiiForums mobile app
 
Ndio mana kuna watu wanapinga mambo za mahari sababu ndio kama hizi. Kwani angepokea hyo 1M angepungukiwa kitu gani wazee wengine nuksi sana.
Mfano wewe mtoto wako azalishwe bila ndoa itafurahia ? Na aje kuishi na mwanaume bila kumjua na aje kwako kujitambulisha na vizawadi vya kuwadanganya kama watoto au familia yenye dhiki sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…