Nimetoka ukweni Kigoma, ila kama hii ndiyo aina ya wazee acha wabaki na watoto wao!

Nimetoka ukweni Kigoma, ila kama hii ndiyo aina ya wazee acha wabaki na watoto wao!

Na hapa ndipo penye mkwamo, nakosa namna yoyote ya kufanya isipokuwa kumuacha kabisa mtoto wao, japo ni kweli nampenda ila sina namna!
Ukimuacha huyo mwanamke utakuwa umeonyesha madhaifu makubwa na pia unaweza sababisha matatizo upande wako. Kina Yemga wanaweza kukuwangia.

Kama ni mahari lipia kidogo kidogo mkuu kwani shida iko wapi na mkeo ushampenda.
 
Pole sana Kiongozi.

Duuuh kweli Mapenzi sio Mchezo Dar to Kigoma tena ndani ndani.

Iko hivi, hapo usitumie hisia utaumia.
Logic ipo hivi huwezi kuoa mwanamke halafu huelewani na mzazi mmojawapo au wote, wewe ndio utaumia mwisho wa siku Kama litamtokea jambo lolote huyo binti Kwa bahati mbaya au makusudi au wewe mwenyewe linaweza kukutokea jambo baya.

Na kumbuka eneo unalooa sina hakika asili ya ukoo wa mkeo mtarajiwa sababu kama asili ni nchi ile jirani hao jamaa ni kisanga Kwa kutunza ubaya ili kuja kulipa kisasi.

Usipoelewana na wazazi wa huyo mwanamke hasa baba yake aisee usimuoe huyo mwanamke.

Weka hisia pembeni kabisa. Maana hisia ndio zinatetea mwanamke huyo kwamba hana kosa, mara mmezaa sa itakuaje ila Situation inagoma kabisa.

Oa tu huyo dada endapo umesawazisha mambo na Baba yake.
 
Kazaa na mrundi huyo na ni wachawi balaa🤔ajipange
 
Na hapa ndipo penye mkwamo, nakosa namna yoyote ya kufanya isipokuwa kumuacha kabisa mtoto wao, japo ni kweli nampenda ila sina namna!
Mwanaume gani HUNA KIFUA? Be gentlemen, hii issue ndogo sana sana sema umeikuza sana. Wewe subiri upate mtoto wa kike umsomeshe hadi Universitty atokee Bazazi kama wewe ampachike mimba, binti ajifungue then linakuja kutokea mtoto anakrbia mwaka. Aysee mimi ntakuttwanga risasi mamaaae zako. Mwanangu Chuo kikuu nilimtuma Degree siyo MIMBA yako. Huna nidhamu wewe kijana huyo mzee hajakosea.
Ukimuacha huyo binti kuna mawili laaana ya Mke imuandame au Laana ya mzee ikuandame kimila zaidi. Hupitishi round. RIP in advance
 
Mfano wewe mtoto wako azalishwe bila ndoa itafurahia ? Na aje kuishi na mwanaume bila kumjua na aje kwako kujitambulisha na vizawadi vya kuwadanganya kama watoto au familia yenye dhiki sana.
Kwa hiyo kwa mtazamo wako sisi kutoka Dar mpaka Kigoma kwenda kuyajenga tulikuwa wapumbavu?
Ilikuwa busara kuona dhamira yetu na kuwa muungwana, ila kwa réaction aliyoonyesha atabaki n'a mtoto wake tu, siwezi kuwa n'a baba mkwe wa aina yake
 
Siwezi kufurahi lkn angalau mwanaume kaenda kujionesha wengine huwa wanakula kona moja kwa moja. Wapunguze mahari mtoto wao aolewe jamaa akizira hasara kwa binti yao.
Kaenda kujionyesha baada ya kuishi kinyumba mpaka mtoto kuzaliwa sasa hapo uoni dharau hizo? Wewe usikie binti yako yupo Dar anaishi na mwanaume kama mke na kazalishwa je kama familia ya binti mtajisikiaje na jamii ya iliyowazunguka si itakuwa fedheha ? Maana maisha ya vijijini yanajulikana utasikia mtoto wa furahi kazalishwa na anaishi na mwanaume bila kuolewa na wazazi wake watakuwa wanaishi bila furaha.
 
Sawa nimekusoma. Unashauri nini kifanyike??
 
Dogo mpaka utakapoelewa umuhimu wa kushiriki maswala ya kijamii kwenye familia tarajiwa ndipo utakapo acha kuteseka. Kwa mtu anaejielewa ikishatokea mimba tu anajipeleka mwenyewe sio lazima azae na hayo mambo ya mkaja wa mama hii inatolewa kama mwanamke ni bikra mbali na hapo hakuna ujinga kama huo. Mfano huku kwetu hela ya mama ndio sawa na utakayompa baba bahati nzuri mm ndio nilimtoa bikra wife sikua na kinyongo kuitoa lakini ningeleta utata kwamba sijamkuta na bikra alooo wangeishia kula mahari na blangeti la bibi kuhusu shangazi mgao wake upo kwenye hela ya mama kwahyo angekosa. Na mahari mara nyingi ni ngombe mmoja au wawili ila mahari ya 4m alooo wanakukomoa tu kwakua hukuonyesha ushirikiano. Jitahidi kukaa na wazee wakupe busara na nn cha kufanya kwenye familia ya mke itakusaidia sana asee
Aisee!
 
Kwa hiyo kwa mtazamo wako sisi kutoka Dar mpaka Kigoma kwenda kuyajenga tulikuwa wapumbavu?
Ilikuwa busara kuona dhamira yetu na kuwa muungwana, ila kwa réaction aliyoonyesha atabaki n'a mtoto wake tu, siwezi kuwa n'a baba mkwe wa aina yake
Sasa mkuu ulitakiwa familia ya mwanamke ikujue kabla ya mimba au mtoto kuzaliwa, sasa wewe unaishi na mtoto wa mtu kabla ya kumpa ujauzito mpaka anajifungua upo kimya na mpaka anaenda kwao anakaa miezi mingi kazi yako ni kupiga simu na kumtumia pesa we unavyoona ulikuwa sahihi?, je mimba ingetoka mpaka leo ungekuwa unaishi naye bila kujulikana kwao, wewe ulienda kuweni kwaajili ya mtoto bila kuwepo na mtoto safari ya Kigoma hakuna .
 
Wewe jamaa huna ajili, au uwezo wako wa kufikiria ni mdogo sana!
Wewe ndie mpuuzi tena huna hata chembe ya busara. Karma is real nawewe utapata watoto wa kike naombea sana suala hili likupate siku moja. Yaani umzalishe binti yangu halafu uje kujileta baada ya mwaka? Utachezea vitasa mpaka MOI wadhani umegongwa na Treni. Be Calm umeharibu wewe na ugomvi umeauanza wewe kwa mzee.
 
Back
Top Bottom