Nimetoka ukweni Kigoma, ila kama hii ndiyo aina ya wazee acha wabaki na watoto wao!

Nimetoka ukweni Kigoma, ila kama hii ndiyo aina ya wazee acha wabaki na watoto wao!

Kaka pole ila tumia busara, Lower your ego....kumuacha huyo mwanamke ni kutengeneza tatizo kubwa zaidi maana hakuna mzazi anayetaka mwanae azalishwe kisha aachwe. Nadhani hizo hasira za baba ni za muda mfupi tu hata wewe usingependa mwanao azalishwe kienyeji.
Utamuumiza sana mama na mtoto ambao hawana hatia ...ongea na washenga wako ikibidi hyo pesa uwe unalipa kidogokidogo mahari huwa haimaliziwi. Tofauti na hapo utajitafutia matatizo makubwa zaidi waha sio watu wa mchezomchezo eti..
 
Yani we jamaa umekaa na mtoto wa watu, umemzalisha, umemtuma kwao ili uje kukamilisha taratibu za kuoa, wewe umemchukua ndugu yako mmoja eti mnaenda kujadili mahari, it doesn't make any sense, ni dharau na mazoea hayo. Kwani huko kwenu taratibu za kuoa zikoje? Au ndo ukishampiga mtoto wa mtu mimba ndo unatoka na rafiki yako kwenda kwa babamkwe kuuliza ni shangapi?
Kwa maisha haya nisombe Kijiji kizima kwenda kulipa mahari, nauli n'a mahitaji mengine ya sisi kufika huko Kijijini ime-cost zaidi ya 500k (yaani nauli, kula na kulala) tungeenda 4 ingetugharimu 1M nzima, halafu kwenda wengi ndiyo kuna maana gani sasa?

Nimemchukua kaka yangu wa makamo (50's of age) nimemchukua mzee mwenyeji kama mshenga ili atusaidie ku-cope na mila na desturi zao, then wananiletea ujinga wa mahari za 4M!

Hapa ndipo uislam unaonekana kuwa smart sana kwenye eneo hili kuliko huu ujinga ujinga wetu!
 
Aisee pole Waha hao mbona wa ajab hivyo?! Lea mwanao mtafutie mzazi mwenzio mtaji muwezeshe achana nae kwa salama huyo baba mkweo ni sumu na hakuna ndoa bila baraka za wazazi,na nyie ndo mkome unaishije kinyumba na mwanamke mpaka unajaza mimba kwao hutambuliki upande flani baba ana haki ya kuwa mkali hakuna mzazi anafurahia binti yake awekwe kinyumba na akazaa hata kwenda,hapo naona mzee ana hasira hizo za kumla mwanae na kumzalisha bure kabisa ni namna yake ya kulipa kisasi.
 
Mbaya zaidi ntalazimika kumuacha mtoto wao kwa makosa ya baba yake
This is a wrong idea brother. Kikubwa, tafuta milioni moja, muombe Mshenga aipeleke kwa baba mkwe. Yeye atatafuta wazee wenye busara wakae na mzee waelewane wakiwa wao Waha peke yao. Si busara sana mtoto kulelewa na zazi mmoja.
 
Sawa nimekusoma. Unashauri nini kifanyike??
Yeye afuate utaratibu wa ukweni. Yeye angekuwa kaenda kuposa binti yao bila kumzalisha wala mambo yasinge kuwa makubwa, Niliwahi kuishi Zanzibar wao Tamaduni zao zina bana mambo ya hovyo kama haya, kwanza Wazanzibari hakuna tabia ya kuishi na mwanamke bila kufunga ndoa yani uishi kama muomba ushauri alivyofanya.
Huyu binti angekuwa Mzanzibari huyo leo angekuwa na kesi ya kutorosha binti chini ya uangalizi wa wazazi na angepewa kesi ya ubakaji na angekuwa mahabusu na wazazi wa mwanamke wangetaka wayamalize nje angetoa pesa nyingi sana.
 
Kila jamii inatamaduni zake, kama tamaduni zenu zina ruhusu Mtoto wakike azae nje ya ndoa au akipata mchumba waishi tu kiuni itakuwa sahihi, lakini kwa tamaduni zetu ukitaka kuoa lazima ufunge ndoa kisheria ya Dini , mira au Kiserikali, siyo mnakutana chuo au Dar mnaishi chumba kimoja mnazaa watoto hata familia ya mwanamke haikujui kwa utaratibu huu haikubaliki kimira wala kidini, unakuwa umeidharau familia ya upande wa mwanamke.
Kwa hiyoninsyodharaulika ni familia ya mwanamke tu, lakini ya mwanaume haidharauliki?
 
Jaribu kutafuta wazee wa kwenu wakaongee nae kiutu uzima, alichokasirika yeye ni wewe kuchelewa kwenda na ulivyoenda hukupaswa kwenda wewe Kwanza(wangeenda wazee).

mzee pia atakua na zile itikadi za kwamba jamaa ana hela[emoji23][emoji23][emoji23] we kutoka dar hadi kigoma ndani ndani huko sio poa[emoji119][emoji119]
 
Aisee mimi sio muumini sana wa Generalization. Sasa hapo kosa la mke ni lipi hadi upange kumtosa. Haya mambo ya kuishi kuogopa binadamu wenzako watasema nini au watafanya nini yamepitwa na wakati.

Kwa hiyo unamuacha mke mzuri ambae baba ake mchizi boti halafu unaenda kuoa mdangaji ambae baba ake mchungaji.

Mbona bangi ninayovuta mimi haiko hivi?!
 
Back
Top Bottom