Pole sana kiongozi, umepata baba mkwe mkoloni sana.Ana tabia zote za Wazee Wa zamani.
Baba mkwe wako,kasimamia misingi ya Mila na tamaduni za kwao. Kimsingi ulikosea ulipo Anza kukaa na Binti Yao kienyeji,Hadi kufikia kumpa ujauzito , akaenda kujifungulia kwao(pasipo wewe kujurikana), akaja akafikwa na msiba(hukuoneka pia).
Matukio yote hayo uliyafanya na Binti Yao na kuwasiliana na Binti Yao tu. (hapa walitafasiri kuwa una jeuri).
Bado haitoshi ukapereka zawadi(unapereka usasa Kwa watu wenye misimamo ya kikoloni).
Sasa kwakuwa mambo yameshatokea, Haina budi kupambana, Ili muwe na mapenzi bora na salama wewe na familia yako. (Tambua mkwe ni Muha wa mipakani).
Jichange, ukipata ata 1M fanya kwanza mawasiliano na mshenga wako, Mshenga ndiyo afanye mawasiliano na baba mkwe wako! Amtaarifu kuwa "mmebahatika kupata 1M hivyo mnaomba aipokee, nyingine mtazidi kutuma mbeleni".Baada ya muda ukipata kama 500K fanya hivyo hivyo, alafu ndiyo uhanze Kutengeneza mawasiliano na mama mkwe wako. Kira Utakapo kuwa una wasiiliana nae mkumbushe amsalimie baba mkwe wako.
Baada ya muda tengeneza mazingira iyonekane mnapitia Hali ngumu sana, lakini unazuga kutuma ata pesa kidogo ya sukari na chumvi(hapa tuma Kwa mama mkwe au baba mkwe alafu mpe mwanao Simu awasalimu).Endelea kuwa Julia Hali na kushiriki mambo madogomadogo ya upande wa ukwenu.
Kuna muda atajirudi tu na anaweza kurudisha moyo nyuma, lakini pia mahali ata isipo isha siyo mbaya. Kikubwa umeonesha nia na utayari. Pia wamesha ona na Kutambua wewe ni mtu wa namna Gani.
Ndoa ni baraka toka pande zote mbili.