Nimetoka ukweni Kigoma, ila kama hii ndiyo aina ya wazee acha wabaki na watoto wao!

Nimetoka ukweni Kigoma, ila kama hii ndiyo aina ya wazee acha wabaki na watoto wao!

Yeye afuate utaratibu wa ukweni. Yeye angekuwa kaenda kuposa binti yao bila kumzalisha wala mambo yasinge kuwa makubwa, Niliwahi kuishi Zanzibar wao Tamaduni zao zina bana mambo ya hovyo kama haya, kwanza Wazanzibari hakuna tabia ya kuishi na mwanamke bila kufunga ndoa yani uishi kama muomba ushauri alivyofanya.
Huyu binti angekuwa Mzanzibari huyo leo angekuwa na kesi ya kutorosha binti chini ya uangalizi wa wazazi na angepewa kesi ya ubakaji na angekuwa mahabusu na wazazi wa mwanamke wangetaka wayamalize nje angetoa pesa nyingi sana.
Uislam ni dini safi kabisa linapokuja swala la ndoa, mahari simple kabisa, sio huku watu wanafanya kuuza watoto wao ili kujipatia kipato kikubwa!
Sidhani kama hiyo ndiyo maana halisi ya mahari!
 
Wewe ni mjinga, mtu kukuletea zawadi ni kudanganywa [emoji706] au mtaonekana mnadhiki..?

Kuna watu waliacha kuoa kisa hayo mamilioni waliaga wakenda mazima
Sijajua wewe kabila gani yani umuharibi maisha binti yangu uishi naye kama mke bila baraka ya wazazi kisha umzalishe aje nyumbani kwangu kila uje na zawadi za danganya toto.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] ndo mana matatizo kama hayo yanawakuta watu wanaoweza kutatatua tu[emoji113] siku zote hasira hasara sasa atakaeteseka ni mwanao yani damu yako ety akiamua kunitafuta atanitafuta loooh[emoji28][emoji28][emoji706] hivii kabisa unajua una mtoto wako mahali hujui anakula nini analala vp unishi kwa amani kabisa kisa wamekutajia mahali bei[emoji1787][emoji1787] pesa inatafutwa mkuu tunaishi mpaka siku tunakufa tunatafuta helaa tuu[emoji119] ila ukiwa na mawazo ya kwamba sisi wote ni binadamu na yote yanapita wala hutateseka na vitu vya kijinga kama pesa[emoji174]
Ww itakua hujasoma bandiko la mleta mada vizuri na kulielewa.
Shida sio hela aliyotajiwa, shida ni pale baba mkwe wa mchongo alivyoleta ubabe na vitisho. Sasa kuepusha yote hayo akae na mwanae na mjuu awalee.

Mbona watu wa namna hii wamekomeshwa na wengi. Binti zao wamepigwa mimba na jamaa haonekani maisha yote. Kitu gani kizuri kama jamaa kujitokeza tena kiungwana na yuko tayar kwa mahali. Kama ni hela angeiomba kistaarab. Angepokea zilizopo na wakapeana muda wa kuzilipa ili kulinda undugu na mahusiano.
 
Ulifanya Makosa kwenda Kwa kumsikiliza hiyo Mchumba wako. Hivi vibinti vya siku hizi havijui mambo ya Mila. Alisema milioni 1 ili uende.

Kama alikudhalilisha Sana na kukutokea maneno ya shombo. Piga Chini.
Sio lazima uwe na Binti Yao
 
Kwa tabia na hiyo, nakuhakikishia watoto wako watazalishwa na hutokaa uone sura za waliowazalisha, achilia mbali kuwapiga makofi...
Utalea vijukuu visivyo na baba na cha kufanya hautakuwa nacho!

Yaani mtu kuja kuyajenga ili kurekebisha makosa unaleta upumbavu wa kujifanya una hasira nyingi?
Ndio usha yakanyaga sasa
 
Huyu hajui kila jamii ina tamaduni zake, huyu angekuwa kamfanyia binti waki Zanzibar ndiyo angejua vizuri ni jambo baya la kuishi kinyumba na binti wawatu bila ndoa, kule Zanzibar angefungwa jela kwa kosa la kutorosha binti chini ya uangalizi wa wazazi na kumbaka na kuishi naye kinyumba yani mpaka leo angekuwa yupo mahabusu, yani Wazanzibari wanatushangaa sana sisi watanganyika tunaishi na wanawake bila ndoa, hii tabia ya hovyo wazanzibari hawana ya kuishi kinyumba na mtoto wa mtu.
Na wewe umekazania wazanzibari wazanzibari, kwa hiyo Zanzibar hakuna single mothers?

Na huko ukumbuke asilimia kubwa ya wakaazi wake ni waislamu, ambao mahari kwao sio kikwazo kufunga ndoa, that is why ni rahisi watu kuingia ndoani n'a kutoka pia!

Kama mtu anaweza kuoa kwa mahari ya sh. laki mbili na baada ya mwezi akamuacha mke na kuoa mwingine, unaringanishaje na hizi za kwetu?

Umesema kila jamii ina utaratibu wake, kwa hiyo unapokazania yanayotokea Zanzibar, jua kabisa nako kuna madhaifu yake!
 
Nimekuwa kwenye mahusiano na mwanamke kutoka Kigoma tangu 2020, tulikutana chuo, na penzi likakolea haswaa!

Kipindi cha Covid penzi lilinoga zaidi kwani "Working from home" ilifanya muda wote tuwe pamoja, ilikuwa mwendo wa kwenda sokoni kununua mazaga zaga pamoja, tinaweka ndani then kila baada ya mlo ni mnyanduano tu, hatimaye binti akashika mimba!

Baada ya mimba kufikisha miezi minne bibie akaniambia ni bora aende kwao kwanza kwani kubaki tukiwa wawili hatuwezijua complications za mimba, nilikubaliana nae, nikajipiga kwa kadri ya uwezo wangu nikamkatia tiketi na vizawadi kidogo vya wazee akaenda kwao!

Akiwa kwao mawasiliano yetu yalikuwa vizuri kabisa mpaka akajifungua salama salmin, na mimi niliwajibika haswa mpaka dk. ya mwisho, hatimaye tukapata mtoto wa kiume.

Bibie baada ya mtoto kufikisha miezi 6 bila mimi kwenda kujitambulisha akatoa wazo la kurudi kwangu kwani alikuwa amechoka kuishi nyumbani kwao, nikamkaribisha tukaendelea na maisha ya sogea tuishi.

Mwaka jana December, ilitokea msiba kwao akalazimika kwenda msibani, nikamfanyia maandalizi vizuri kabisa, akaondoka.

Amekaa huko tangu December, mpaka juzi nilipoamua kufuata taratibu za kwenda kwao ili tusiendelee kuishi kimya kimya (tufanye kuwa official), nikajiandaa kwa mambo kadhaa kama nilivyokuwa nimeng'atwa sikio na mpenzi wangu.

Nimeanza safari kutoka Dar kwenda Kigoma (kwao), nikiwa nimeambatana na brother wangu wa damu, aisee kwao ni mbali, maana tulitembea siku 2 njiani, tulipofika mjini, safari ya kwenda kwao ikachukua masaa mengine 8, vumbi kali hatari, tulipofika Kijijini kwao tukaambiwa Burundi ni mwendo wa kutembea nusu saa tu.

Brother akaniuliza, "Hivi dogo hukuona wanawake mikoa yote tuliyopita mpaka kuja huku?" Nikamwambia mapenzi yana nguvu bro, sikuwahi kufikiria kama kuna siku ningesafiri umbali namna hii kufuata mwanamke tu. Tulipofika mjini tulitafuta mzee mwenyeji, anayejua mila na desturi za Kiha ili mambo yasiwe magumu.

Basi bwana, tumefika pale tumepokelewa vizuri wakaandaa utaratibu wa mjadala, mshenga akatambulisha na kuanza mazungumzo rasmi, hapo nilikuwa na zawadi ya baba mkwe na mama mkwe, nilinunua tangu Dar kwa upendo kabisa.

Wakataja kiasi cha mahari kuwa wanataka mil. 4.5, hapo tukashtuka kweli, kabla hatujakaa sawa wakataja mkaja wa mama sh. laki saba, jumla wanataka 5.2 Milioni!

Yule mzee tuliyeenda naye akaomba twende nje kwa mazungumzo, akatuuliza kama tulipewa mwongozo na tuliyekwenda kumuoa, nikamjibu ndiyo (alisema mahari kwao haizidi Milioni moja) na mkaja wa mama huwa ina-range kuanzia 100k - 200k, na mimi niliandaa 200k kama mkaja wa mama! Mzee akasema hapa kuna tatizo, huku haijawahi kutokea mahari kubwa kiasi hiki, akasema tutasimamia kwenye hiyo 1M na mkaja wa mama 200k, tukarudi ndani!

Mzee (mshenga) akaanza kuzungumza, kuwa sisi tuna mahari 800k na mkaja wa mama 100k, lakini pia tuna zawadi kwa ajili ya baba na mama, ambazo si sehemu ya mahari, ni zawadi tu ya kijana wetu kwenu, mzee akatoa zile zawadi akaweka mezani.

Mshenga wao akashukuru na kuanza kuzungumzia mahari yetu kuwa angalau tufanye mahari mil.4 mkaja wa mama 500k.

Kabla hajamaliza akasimama baba mkwe, akionyesha kukasirika akasema "Sitaki mjadala wa kitoto hapa, mimi ndiye baba wa x, mkaja wa mama laki 5, mahari yangu nataka Milioni 4, Sitaki mjadala wala kusikia kupunguziana, kwanza unabeba zawadi kutuletea nani amekutuma utununulie, tumekuomba sisi utuletee zawadi zako?"

"Kwanza huyu kijana anadharau sana, tangu mtoto azaliwe hajawahi kufika hapa nyumbani, anaishia kumtumia mwenzake pesa tu, sisi hajawahi kututumia pesa hata mara moja, tumepata msiba hajawahi kuja kutupa pole zaidi ya kupiga visimu vyake tu, sasa mimi nimeshasema mkaja wa mama laki tano, mahari Milioni 4, sitaki mjadala!"

Aisee nilijikuta nimejaa hasira mpaka basi, mshenga wetu akatutaka twende nje, akasema "huyu mzee inaonekana ana lake jambo, tusiingie kwenye mtego wake, iweni wapole, tuondoke salama, watu wa huku ni hatari sana, tukiwa na hasira tunaweza tusirudi salama, hii si dalili nzuri."

Tukajadili tuvyojiandaa pale, mzee akasema muhimu tuanze na mkaja wa mama, tuwawekee hiyo 500k then tutawapa faini za mbuzi mbuzi, na vingine vidogo vidogo, baada ya hapo mahari tuwaambie kuwa tunaenda kuitafuta then mtaangalia wenyewe baada ya kufika nyumbani!

Tuliporudi ndani tukakuta mzee anaonyesha kuwa na hasira hasira tu, kiasi kwamba mshenga wao akawa ameduwaa tu, basi mshenga wetu akaanza kujitetea pale, akaweka mezani sh. 500k mkaja wa mama, akawaambia mbuzi watatu wa uchafuzi 300k sijui koti la mjomba, mara blanketi ya wazee na vikolo kolo vingine kwa Kadri ya taratibu zao, ile pesa tuliyoenda nayo ikawa imekata!

Muda huo wote Nina hasira vibaya mnooo, ila najitahidi kuificha japo mpnz wangu aligundua kabisa kuwa nimechukia!

Tukawaambia hiyo mil. 4 tunaenda kuitafuta, mzee akasema "mkaitafute muilete hapa, au mutanitumia kwenye simu" tukawaambia sawa.

Muda wa kutoka nikakuta mpnz wangu ameshabeba mabegi anataka tuondoke wote, nikamwambia hapana unapswa kubaki nitakuja kuwachukua nikimalizia mahari, akagoma akawa analia wakati wote akiwa amenikumbatia, anaomba radhi kwa kilichotokea ila anaomba tuondoke wote, yeye hawezi kubaki Kijijini tena, nikamwambia hapana, unapswa kubaki mpaka tumalizane n'a mzee, akagoma kata kata, akawa amepiga magoti huku amekumbatia miguu yangu,machozi yanamtoka tuuu

Mzee wake alipotoka akaona mwanaye analia akasema "kama mnaobdoka wote nendeni tu" Mara mama mkwe akaja na dogo (mtoto wangu) akamshusha nilipokuwa, nikambeba mtoto nikamwambia mama mtoto asimame, bro na mshenga wetu wakaniita pembeni, mshenga akasema tuondoke nao, tukimuacha na wakahisi kuwa Kuna dalili za sisi kutorudi, watamuua huyu mtoto.

Basi kiahingo upande, tukawakubalia kuondoka nao, mama mkwe akaleta maharage na jogoo akataka tuondoke navyo, nikakataa kuchukua, nikamwambia tutabeba wakati mwingine, akagundua bado nina hasira, akamuita mtoto wake, akamwambia "mwambie mumeo amsamehe bure baba yako, amekosea sana, n'a mimi mama naomba atusamehe tu)

Tukaondoka zetu, kichwani nikiwa nimejaa mawazo mengi mnoo, kiasi kwamba sikuweza kujua niamue nini, tumefika Dar lakini moyoni nimejikuta sina tena interest ya kutengeneza undugu na familia ya mpnz wangu, japo yeye binafsi hana shida, lakini kwa namna tulivyopokelewa na tulivyoondoka, nilijisemea moyoni kwamba SITOKAA NIRUDI KIGOMA, WALA SITOKAA NIPELEKE HIYO MAHARI WALIYOSEMA, nasubiri mwanangu akue kue kidogo nimwambie mama mtoto kwamba hakuna namna naweza kuunganisha undugu na familia yake, japo namhurumia ila ndiyo hivyo tena!

Kweli tembea uone, all the way from Dar to Kigoma, naenda kukutana na aibu tu, anyway!
Ilikuwa wilaya gani na kijiji gani.Nimeumia sana? Kuna jambo nataka kusaidia hapa
 
Ww itakua hujasoma bandiko la mleta mada vizuri na kulielewa.
Shida sio hela aliyotajiwa, shida ni pale baba mkwe wa mchongo alivyoleta ubabe na vitisho. Sasa kuepusha yote hayo akae na mwanae na mjuu awalee.

Mbona watu wa namna hii wamekomeshwa na wengi. Binti zao wamepigwa mimba na jamaa haonekani maisha yote. Kitu gani kizuri kama jamaa kujitokeza tena kiungwana na yuko tayar kwa mahali. Kama ni hela angeiomba kistaarab. Angepokea zilizopo na wakapeana muda wa kuzilipa ili kulinda undugu na mahusiano.

huwezi elewa uzito wa kiatu cha mtu kama hujakivaa... yule ni mzazi probably ana hasira after all jamaa kaonyesha busara piaa ila bado mtoa mada kilio chake ni mahali ukiachana na kukasirika kwa baba mkwe wake nadhan hata wewe hujamwelewa mtoa mada[emoji28][emoji28]
 
Back
Top Bottom