Nimetoka ukweni Kigoma, ila kama hii ndiyo aina ya wazee acha wabaki na watoto wao!

Kuna namna wewe pia uliyapalilia hayo matukio, ingawa wengi hawakwambii.
 
Aseee yule Mzee namfahamu ndio kawaida yake. Mvumilie tu. Anataka kukufanya kiinua mgongo chake 😂😂
Wewe ishi tu na bintiye kikubwa anakupenda.
 
Pole mkuu. Lakini hiyo mahari nadhani ni reasonable hasa ukizingatia ulimzalisha mtoto wao na ulichelewa kwenda kujitambulisha! Mimi sijamzalisha wa kwangu lakini nimepigwa mahari 3.8 M na wanyakyusa wa Simike wale!
Ulipigwa ....mkeo alikua mmoja wapo katika mpango wa kukupiga hiyo
 
Naonaa humu mnavyo mlaumu huyo kijana ila mkae mjua kwa mitaa ambayo nimekulia na kuishi kwa jinsi single mother walivyo jaa tena wengine vitoto vidogo chini ya miaka 20.Ukimwona kijana katia mimba na kaja kujitambulisha kwako kwa nia ya kutaka kuoa shukuru sana na husimkomoe.

Kwani vijana wenye moyo kama wa huyu jamaa kwa siku hizi wako wachache, tena huyo katembea umbali mrefu zaidi ya km 1000+Wengine mkwe wake anakaa nyumba ya tatu kutoka anapokaa (mtaa mmoja) na hana time ya mtoto,kujitambulisha wala kuoa binti aliye mtia mimba.

Ndugu yangu kitendo ulicho kifanya ni kikubwa na nia yako ni nzuri, wewe kaa na huyo binti ila nina uhakika huko walipo dhamira zao zita wasuta na watakupunguzia gharama,kwani dhamira yako kwa huyo binti na mtoto ni nzuri.
 
shukuru umepata utalii wa ndani bila hao wazazi na huyo binti lini ungeenda huko, ila hapo kwenye mkaja pananiachaga hoi hadi kesho, me nilikuja kulipa vitu vinaitwa mkaja,vigingi,kinyago sijui na nini mengine nimesahau majina huko kwa wanyakyusa ila nashukuru mahari walinipunguzia tok mln 4-1.3 nikamalizana nao kiroho safi
 
Mimi najuta kuoa kigoma, hapa mda wwte naisambaratisha ndoa yenyewe.nshachoka
 
Umetomba mtoto wa watu weeeh,ukamtia mimba,akajifungua,wakakuzalishia mtoto,wakaklelea miezi sita..hujaenda hata kujitambulisha kuwa wewe ndo muhusika afu unataka wakupokee kwa matarumbeta ukweni??nyie madogo wa siku mna mawazo ya hovyo Sana!!Na una dharau kweli kwa familia ya mwanaume mwenzio. Huyo dingi hakuwa na shida ya hiyo hela ila ni hasira tu kutokana na ulivyofanya,badala ya kujishusha unajinunisha sijui ubembelezwe na nani!!
We fanya fyoko fyoko tena,soon utaanzisha uzi ukim tag MshanaJR unaomba ushauri wa kiroho. Wale wazee watakupika uive!
nb: Acheni dharau na familia za watu, mila na dsturi bado zipo.taratibu ziheshimiwe na mjifunze ku control nyege zenu!!
 
Kwenye inshu ya kubagain Mahari ndio maana wengi huwa wanamtoa Bwanaharusi mtarajiwa asiwepo kwenye haya majadiliano.

Mimi nakumbuka yalinikuta mambo kama haya ya mtoa mada ila baada ya utambulisho tu niliambiwa niondoke pale niende nikakae nje. Alibaki mshenga na wapambe wengine japo nilikuja kuona tukio zima kwenye Video.

Hadi leo nimemchukia Baba mdogo wa mke wangu kutokana na misimamo yake ya kutokubali kupunguza fedha. Nilichofanya nililipa vikolokolo vyote vidogovidogo kama mtoa mada alivyofanya, na Mahari nikatoa laki mbili tu badala ya 3,000,000 na sikurudi tena ukweni na binti yao nilikabidhiwa.
 
Umeandika kwa mihemko sanaaa, nani amesema alitaka kupokelewa kwa maturumbeta?

Kipi bora, kwenda kuyajenga n'a kuweka sawa? Au kupotelea mitini mazima wabaki na mtoto na mjukuu wao?

Halafu ukisema hawakutaka pesa, unathibitisha kwamba walitaja pesa nyingi ili nishindwe kulipa wabaki na mtoto wao?
 
Kwanza ye alienda kama nani???!!!
Baba ake na wazee wa kwao ndo wangeenda.hii ni tofauti kama angekuwa anaenda kuoa afresh
Hivi ni kila mtu ana hao wazazi?
Yaani niliyekwenda naye (Kaka yangu mkubwa) ndiyo kama baba yangu, otherwise wanataka nikamfufue baba yangu ili akajieleze huko ukweni?
 
Kwa hiyo ulilipa pungufu ya asilimia 10 ya mahari?

Ajabu sisi tumeenda na Milioni moja mzee anakataa na kudai anataka 4 Milioni,hakika sitampelekea hiyo pesa hata kwa fimbo
 
Complications zingine hazina maana kabisa, sasa wanamtoa nje mtoa mahari kwa misingi gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…