Nimetoka ukweni Kigoma, ila kama hii ndiyo aina ya wazee acha wabaki na watoto wao!

Nimetoka ukweni Kigoma, ila kama hii ndiyo aina ya wazee acha wabaki na watoto wao!

Wewe ulikosea na ukazidi kukosa

Muulize huyo baba mkwe alimuoaje mkewe?

Kimsingi sisi wa mjini tumekiuka misingi huku tukitaka hao wazee eatupokee kisa mtoto wao aolewe hapana.

Wewe unadhani yeye hakukasirika? Mbona alikupokea
Badilika
 
Mbaya zaidi ntalazimika kumuacha mtoto wao kwa makosa ya baba yake
Kosa kubwa sana hilo Mkuu huyo mzee muhuni hachana nae mbona mama mkwe hana shida huyo mwanamke anamapenzi ya dhati kwa uzoefu wangu
 
Wewe ulikosea na ukazidi kukosa

Muulize huyo baba mkwe alimuoaje mkewe?

Kimsingi sisi wa mjini tumekiuka misingi huku tukitaka hao wazee eatupokee kisa mtoto wao aolewe hapana.

Wewe unadhani yeye hakukasirika? Mbona alikupokea
Badilika
Kwani huyo mzee alioa mwaka huu?
Mambo yanabadilika kutokana na muda na mazingira.
 
N
Pole best. Mke anakupenda Kwa dhati nadhani mpende pia. Wazazi wake fanya kuwasamehe lakini usiende tena kigoma. Mwisho funga ndoa harali ikibidi bila hata wazazi wake kuwepo ili likitokea la kutokea uwe on safe place
Unamdanganya. Ndoa atafungaje bila wazazi?. Huoni hapo ndio itakuwa balaa?
 
Pole sana.
Kwanza hongera kumpata mzee mshenga muelewa,mvumilivu na anaejua mila za huko.

Pili Maisha sio kila ukitakacho ndicho utakachokipata. Namaanisha umempata mwenza kama unampenda familia yako itaanzia hapo. Msahau baba yake kuwa na undugu nae. Wewe focus kutengeneza familia yako iliyosimama. Baba yake hata mngekuwa sawa bado InabaKi wewe na familia yako tu,wewe,mkeo na wanao.
Labda tu ni vile vijana wa siku hizi kuoa ni mtihani mwingine. Usione hiyo ikawa sababu ya kuacha familia uliyoianza.
Kumbuka Wewe unamuoa huyo binti na utatengeneza familia na huyo mkeo ,sio babaake.

Mwisho mtumie vizuri huyo mshenga wako hata kumuuliza namna ya inavyotakiwa iwe. Ksbb unaweza kuamua kuishi hivi unavyosema hapa bado ikawa tatizo kwako.

Niaonavyo hakuna namna nyingine nzuri zaidi ya kutafuta milioni 3 au 2.5. Nenda tena na yule mzee mshenga akakuwakilishe. Katoe mahali hiyo. Naamini nae mzee hasira zitakuwa zimeshuka. Hakuna namma nyingine nzuri kutafuta kuishi kwa amani zaidi ya kumalizana na ulichokianza. Katoe mahali mkuu
 
Nimekuwa kwenye mahusiano na mwanamke kutoka Kigoma tangu 2020, tulikutana chuo, na penzi likakolea haswaa!

Kipindi cha Covid penzi lilinoga zaidi kwani "Working from home" ilifanya muda wote tuwe pamoja, ilikuwa mwendo wa kwenda sokoni kununua mazaga zaga pamoja, tinaweka ndani then kila baada ya mlo ni mnyanduano tu, hatimaye binti akashika mimba!

Baada ya mimba kufikisha miezi minne bibie akaniambia ni bora aende kwao kwanza kwani kubaki tukiwa wawili hatuwezijua complications za mimba, nilikubaliana nae, nikajipiga kwa kadri ya uwezo wangu nikamkatia tiketi na vizawadi kidogo vya wazee akaenda kwao!

Akiwa kwao mawasiliano yetu yalikuwa vizuri kabisa mpaka akajifungua salama salmin, na mimi niliwajibika haswa mpaka dk. ya mwisho, hatimaye tukapata mtoto wa kiume.

Bibie baada ya mtoto kufikisha miezi 6 bila mimi kwenda kujitambulisha akatoa wazo la kurudi kwangu kwani alikuwa amechoka kuishi nyumbani kwao, nikamkaribisha tukaendelea na maisha ya sogea tuishi.

Mwaka jana December, ilitokea msiba kwao akalazimika kwenda msibani, nikamfanyia maandalizi vizuri kabisa, akaondoka.

Amekaa huko tangu December, mpaka juzi nilipoamua kufuata taratibu za kwenda kwao ili tusiendelee kuishi kimya kimya (tufanye kuwa official), nikajiandaa kwa mambo kadhaa kama nilivyokuwa nimeng'atwa sikio na mpenzi wangu.

Nimeanza safari kutoka Dar kwenda Kigoma (kwao), nikiwa nimeambatana na brother wangu wa damu, aisee kwao ni mbali, maana tulitembea siku 2 njiani, tulipofika mjini, safari ya kwenda kwao ikachukua masaa mengine 8, vumbi kali hatari, tulipofika Kijijini kwao tukaambiwa Burundi ni mwendo wa kutembea nusu saa tu.

Brother akaniuliza, "Hivi dogo hukuona wanawake mikoa yote tuliyopita mpaka kuja huku?" Nikamwambia mapenzi yana nguvu bro, sikuwahi kufikiria kama kuna siku ningesafiri umbali namna hii kufuata mwanamke tu. Tulipofika mjini tulitafuta mzee mwenyeji, anayejua mila na desturi za Kiha ili mambo yasiwe magumu.

Basi bwana, tumefika pale tumepokelewa vizuri wakaandaa utaratibu wa mjadala, mshenga akatambulisha na kuanza mazungumzo rasmi, hapo nilikuwa na zawadi ya baba mkwe na mama mkwe, nilinunua tangu Dar kwa upendo kabisa.

Wakataja kiasi cha mahari kuwa wanataka mil. 4.5, hapo tukashtuka kweli, kabla hatujakaa sawa wakataja mkaja wa mama sh. laki saba, jumla wanataka 5.2 Milioni!

Yule mzee tuliyeenda naye akaomba twende nje kwa mazungumzo, akatuuliza kama tulipewa mwongozo na tuliyekwenda kumuoa, nikamjibu ndiyo (alisema mahari kwao haizidi Milioni moja) na mkaja wa mama huwa ina-range kuanzia 100k - 200k, na mimi niliandaa 200k kama mkaja wa mama! Mzee akasema hapa kuna tatizo, huku haijawahi kutokea mahari kubwa kiasi hiki, akasema tutasimamia kwenye hiyo 1M na mkaja wa mama 200k, tukarudi ndani!

Mzee (mshenga) akaanza kuzungumza, kuwa sisi tuna mahari 800k na mkaja wa mama 100k, lakini pia tuna zawadi kwa ajili ya baba na mama, ambazo si sehemu ya mahari, ni zawadi tu ya kijana wetu kwenu, mzee akatoa zile zawadi akaweka mezani.

Mshenga wao akashukuru na kuanza kuzungumzia mahari yetu kuwa angalau tufanye mahari mil.4 mkaja wa mama 500k.

Kabla hajamaliza akasimama baba mkwe, akionyesha kukasirika akasema "Sitaki mjadala wa kitoto hapa, mimi ndiye baba wa x, mkaja wa mama laki 5, mahari yangu nataka Milioni 4, Sitaki mjadala wala kusikia kupunguziana, kwanza unabeba zawadi kutuletea nani amekutuma utununulie, tumekuomba sisi utuletee zawadi zako?"

"Kwanza huyu kijana anadharau sana, tangu mtoto azaliwe hajawahi kufika hapa nyumbani, anaishia kumtumia mwenzake pesa tu, sisi hajawahi kututumia pesa hata mara moja, tumepata msiba hajawahi kuja kutupa pole zaidi ya kupiga visimu vyake tu, sasa mimi nimeshasema mkaja wa mama laki tano, mahari Milioni 4, sitaki mjadala!"

Aisee nilijikuta nimejaa hasira mpaka basi, mshenga wetu akatutaka twende nje, akasema "huyu mzee inaonekana ana lake jambo, tusiingie kwenye mtego wake, iweni wapole, tuondoke salama, watu wa huku ni hatari sana, tukiwa na hasira tunaweza tusirudi salama, hii si dalili nzuri."

Tukajadili tuvyojiandaa pale, mzee akasema muhimu tuanze na mkaja wa mama, tuwawekee hiyo 500k then tutawapa faini za mbuzi mbuzi, na vingine vidogo vidogo, baada ya hapo mahari tuwaambie kuwa tunaenda kuitafuta then mtaangalia wenyewe baada ya kufika nyumbani!

Tuliporudi ndani tukakuta mzee anaonyesha kuwa na hasira hasira tu, kiasi kwamba mshenga wao akawa ameduwaa tu, basi mshenga wetu akaanza kujitetea pale, akaweka mezani Tsh. 500k mkaja wa mama, akawaambia mbuzi watatu wa uchafuzi 300k, sijui koti la mjomba, mara blanketi ya wazee na vikolo kolo vingine kwa Kadri ya taratibu zao, ile pesa tuliyoenda nayo ikawa imekata!

Muda huo wote nina hasira vibaya mno, ila najitahidi kuificha japo mpenzi wangu aligundua kabisa kuwa nimechukia. Tukawaambia hiyo mil. 4 tunaenda kuitafuta, mzee akasema "Mkaitafute muilete hapa, au mutanitumia kwenye simu," tukawaambia sawa.

Muda wa kutoka nikakuta mpenzi wangu ameshabeba mabegi anataka tuondoke wote, nikamwambia hapana unapaswa kubaki nitakuja kuwachukua nikimalizia mahari. Akagoma, akawa analia wakati wote akiwa amenikumbatia, anaomba radhi kwa kilichotokea ila anaomba tuondoke wote, yeye hawezi kubaki kijijini tena. Nikamwambia hapana, unapaswa kubaki mpaka tumalizane na mzee, akagoma kata kata, akawa amepiga magoti huku amekumbatia miguu yangu, machozi yanamtoka tu!

Mzee wake alipotoka akaona mwanaye analia akasema "Kama mnaondoka wote nendeni tu!" Mara mama mkwe akaja na dogo (mtoto wangu), akamshusha nilipokuwa, nikambeba mtoto nikamwambia mama mtoto asimame, bro na mshenga wetu wakaniita pembeni, mshenga akasema tuondoke nao, tukimuacha na wakahisi kuwa kuna dalili za sisi kutorudi, watamuua huyu mtoto.

Basi kishingo upande, tukawakubalia kuondoka nao, mama mkwe akaleta maharage na jogoo akataka tuondoke navyo, nikakataa kuchukua, nikamwambia tutabeba wakati mwingine, akagundua bado nina hasira. Akamuita mtoto wake, akamwambia "Mwambie mumeo amsamehe bure baba yako, amekosea sana, na mimi mama naomba atusamehe tu."

Tukaondoka zetu, kichwani nikiwa nimejaa mawazo mengi mno, kiasi kwamba sikuweza kujua niamue nini. Tumefika Dar lakini moyoni nimejikuta sina tena interest ya kutengeneza undugu na familia ya mpenzi wangu, japo yeye binafsi hana shida, lakini kwa namna tulivyopokelewa na tulivyoondoka, nilijisemea moyoni kwamba sitokaa nirudi Kigoma, wala sitokaa nipeleke hiyo mahari waliyosema.

Nasubiri mwanangu akuekue kidogo nimwambie mama mtoto kwamba hakuna namna naweza kuunganisha undugu na familia yake, japo namhurumia ila ndiyo hivyo tena.

Kweli tembea uone, all the way from Dar to Kigoma, naenda kukutana na aibu tu, anyways.
Kwanza kabisa ulikosea kwa kumfanya mwana wa watu mkeo kabla ya idhini ya wazazi wake, pili ulikosea na kuonesha dharau kama baba mkwe analivyosema, haiwezekani binti ameenda kwao tangu akiwa na miezi minne mpaka anajifungua na akzidisha miezi sita zaidi na wewe hujaenda kwao, binti karudi tena kwako mumekaa mpaka umetokea msiba kwao na bado akaenda peke yake. Umekosea sasa kamanda! Kuhusu mzee kudai mahari kubwa kuliko uhalisia hapo anakosea lakini yupo ndani ya haki yake ikiwa mila zao zinaruhusu.

Ikiwa kweli ulimpenda huyo binti acha upumbavu, tafuta milioni nne lipa funga ndoa maisha yaendelee. Na hata kama huna hiyo pesa omba kulipa nusu funga ndoa!

Hili pia ni somo kwa mabinti, ni wazi huyu kijana anaipenda milioni yake nne zaidi kuliko mzazi mwenzake. Ila yote haya angeweza kuyakabili vizuri huyu binti kama asingejikabidhi kwa kijana kama mke kabla ya muda wake. Kwanini mnarudi kwa wazee ikiwa nyie mlidhani mnajitosha kuishi kinyumba???
 
Pole best. Mke anakupenda Kwa dhati nadhani mpende pia. Wazazi wake fanya kuwasamehe lakini usiende tena kigoma. Mwisho funga ndoa harali ikibidi bila hata wazazi wake kuwepo ili likitokea la kutokea uwe on safe place
MLETA MADA ISHI HAPA.
 
Mbona Waha hatuko hivo
Namaranyingi kwetu mtu akija kama wewe hivo hua tunawapa heshima kubwa sana itakua huyo Mzee majirani walimchezea kiimani..
 
Piga chini ila kijanja.

Hapo kuna kila dalili kuwa baba mkwe ni fundi. Sasa akikutikisa dishi Je?

Ndoa ni zaidi ya mke na mme
 
K
Hilo la kuua mtoto si kweli.Mambo huwa complicated unapozaa kabla ya kutimiza taratibu.Punguza hasira.Naturally wababa huwa overprotective kwa Binti zao. Jipe muda, baadaye utagundua huyo Mzee ni mtu poa kuliko unavyodhani. Utaratibu mzuri wa kuoa huku ni kwamba Binti stoke mbichi Nyumbani. Wee umefanya uchafuzi halafu unataka fair? Kila kabila na taratibu zake. Jipe muda utagundua. Mwenyezi Mungu awajalie Kila lililo la heri kwenye familia Yako changa.
Kwa nini unamuona huyo jamaa ndiye mchafuzi na siyo binti ambaye alikuwa akizifahamu vyema taratibu na mila za nyumbani kwao?
 
Mfano wewe mtoto wako azalishwe bila ndoa itafurahia ? Na aje kuishi na mwanaume bila kumjua na aje kwako kujitambulisha na vizawadi vya kuwadanganya kama watoto au familia yenye dhiki sana.
Kama binti ndiye katoa ombi la kuzalishwa kinachokukasirisha ni nini?
Wewe wape baraka waendelee kujenga familia yao kwa kuzingatia kwamba binti siyo mwanafunzi.
 
Back
Top Bottom