Ahmad Abdurahman
JF-Expert Member
- Mar 5, 2016
- 3,251
- 6,299
Mwamba maamuzi ni yako. Ingekua mm ningemwachia akae na binti yake na amlee mjukuu. Na hawatokuja kuniona kigoma wala kujua naishi wapi.Kwa tabia na hiyo, nakuhakikishia watoto wako watazalishwa na hutokaa uone sura za waliowazalisha, achilia mbali kuwapiga makofi...
Utalea vijukuu visivyo na baba na cha kufanya hautakuwa nacho!
Yaani mtu kuja kuyajenga ili kurekebisha makosa unaleta upumbavu wa kujifanya una hasira nyingi?
aah basi mko vizurikusini hukoo
Ok. Nimekupata kama ni muha OG basi ongea na binti yy ndo atawatuliza wazazi wake mahari itapunguzwa. Binti wa kiha aliyepokea maadili ya Kiha asee bro umepata pipa na mfuniko wake. Nasema nikiwa na ushahidi hai. Binti wa kiha hata usafiri uende sehemu miaka 10 ukirudi utamkuta. Hata mgombane vipi upige vipi hawezi kukuacha kama kakukubali mtu wanguNi muha kabisa mkuu
Kaka mimi ni mtu wa nyanda za juu kusini, alichofanya jamaa hakwenda mikono mitupu, alibeba kiasiSijajua wewe kabila gani yani umuharibi maisha binti yangu uishi naye kama mke bila baraka ya wazazi kisha umzalishe aje nyumbani kwangu kila uje na zawadi za danganya toto.
Hili suala la mahari ni umaskini tu mm mwanangu sitataka mahali kikubwa waishi kwa amani na upendo tu basi tena nawapa makataba kabisa kua mm fulani bin fulani naozesha mtoto wangu bila mahari ninachotaka muishi kwa amani na upendo ikitokea mmeshindwa kuishi pamoja namchukua mwanangu bila masharti yoyteKigoma !? Sijawahi sikia washkaji zangu wakitaja mahali walizolipa below 2.5m mkuu.
Jipange umtumie angalau nusu ya mahali. Vita bado hujaianzisha ila ukiendelea kuishi na huyo mkeo bila mahali utakuja kujuta kwa watu type ya mkweo toka huko kgm
MkuuNimekuwa kwenye mahusiano na mwanamke kutoka Kigoma tangu 2020, tulikutana chuo, na penzi likakolea haswaa!
Kipindi cha Covid penzi lilinoga zaidi kwani "Working from home" ilifanya muda wote tuwe pamoja, ilikuwa mwendo wa kwenda sokoni kununua mazaga zaga pamoja, tinaweka ndani then kila baada ya mlo ni mnyanduano tu, hatimaye binti akashika mimba!
Baada ya mimba kufikisha miezi minne bibie akaniambia ni bora aende kwao kwanza kwani kubaki tukiwa wawili hatuwezijua complications za mimba, nilikubaliana nae, nikajipiga kwa kadri ya uwezo wangu nikamkatia tiketi na vizawadi kidogo vya wazee akaenda kwao!
Akiwa kwao mawasiliano yetu yalikuwa vizuri kabisa mpaka akajifungua salama salmin, na mimi niliwajibika haswa mpaka dk. ya mwisho, hatimaye tukapata mtoto wa kiume.
Bibie baada ya mtoto kufikisha miezi 6 bila mimi kwenda kujitambulisha akatoa wazo la kurudi kwangu kwani alikuwa amechoka kuishi nyumbani kwao, nikamkaribisha tukaendelea na maisha ya sogea tuishi.
Mwaka jana December, ilitokea msiba kwao akalazimika kwenda msibani, nikamfanyia maandalizi vizuri kabisa, akaondoka.
Amekaa huko tangu December, mpaka juzi nilipoamua kufuata taratibu za kwenda kwao ili tusiendelee kuishi kimya kimya (tufanye kuwa official), nikajiandaa kwa mambo kadhaa kama nilivyokuwa nimeng'atwa sikio na mpenzi wangu.
Nimeanza safari kutoka Dar kwenda Kigoma (kwao), nikiwa nimeambatana na brother wangu wa damu, aisee kwao ni mbali, maana tulitembea siku 2 njiani, tulipofika mjini, safari ya kwenda kwao ikachukua masaa mengine 8, vumbi kali hatari, tulipofika Kijijini kwao tukaambiwa Burundi ni mwendo wa kutembea nusu saa tu.
Brother akaniuliza, "Hivi dogo hukuona wanawake mikoa yote tuliyopita mpaka kuja huku?" Nikamwambia mapenzi yana nguvu bro, sikuwahi kufikiria kama kuna siku ningesafiri umbali namna hii kufuata mwanamke tu. Tulipofika mjini tulitafuta mzee mwenyeji, anayejua mila na desturi za Kiha ili mambo yasiwe magumu.
Basi bwana, tumefika pale tumepokelewa vizuri wakaandaa utaratibu wa mjadala, mshenga akatambulisha na kuanza mazungumzo rasmi, hapo nilikuwa na zawadi ya baba mkwe na mama mkwe, nilinunua tangu Dar kwa upendo kabisa.
Wakataja kiasi cha mahari kuwa wanataka mil. 4.5, hapo tukashtuka kweli, kabla hatujakaa sawa wakataja mkaja wa mama sh. laki saba, jumla wanataka 5.2 Milioni!
Yule mzee tuliyeenda naye akaomba twende nje kwa mazungumzo, akatuuliza kama tulipewa mwongozo na tuliyekwenda kumuoa, nikamjibu ndiyo (alisema mahari kwao haizidi Milioni moja) na mkaja wa mama huwa ina-range kuanzia 100k - 200k, na mimi niliandaa 200k kama mkaja wa mama! Mzee akasema hapa kuna tatizo, huku haijawahi kutokea mahari kubwa kiasi hiki, akasema tutasimamia kwenye hiyo 1M na mkaja wa mama 200k, tukarudi ndani!
Mzee (mshenga) akaanza kuzungumza, kuwa sisi tuna mahari 800k na mkaja wa mama 100k, lakini pia tuna zawadi kwa ajili ya baba na mama, ambazo si sehemu ya mahari, ni zawadi tu ya kijana wetu kwenu, mzee akatoa zile zawadi akaweka mezani.
Mshenga wao akashukuru na kuanza kuzungumzia mahari yetu kuwa angalau tufanye mahari mil.4 mkaja wa mama 500k.
Kabla hajamaliza akasimama baba mkwe, akionyesha kukasirika akasema "Sitaki mjadala wa kitoto hapa, mimi ndiye baba wa x, mkaja wa mama laki 5, mahari yangu nataka Milioni 4, Sitaki mjadala wala kusikia kupunguziana, kwanza unabeba zawadi kutuletea nani amekutuma utununulie, tumekuomba sisi utuletee zawadi zako?"
"Kwanza huyu kijana anadharau sana, tangu mtoto azaliwe hajawahi kufika hapa nyumbani, anaishia kumtumia mwenzake pesa tu, sisi hajawahi kututumia pesa hata mara moja, tumepata msiba hajawahi kuja kutupa pole zaidi ya kupiga visimu vyake tu, sasa mimi nimeshasema mkaja wa mama laki tano, mahari Milioni 4, sitaki mjadala!"
Aisee nilijikuta nimejaa hasira mpaka basi, mshenga wetu akatutaka twende nje, akasema "huyu mzee inaonekana ana lake jambo, tusiingie kwenye mtego wake, iweni wapole, tuondoke salama, watu wa huku ni hatari sana, tukiwa na hasira tunaweza tusirudi salama, hii si dalili nzuri."
Tukajadili tuvyojiandaa pale, mzee akasema muhimu tuanze na mkaja wa mama, tuwawekee hiyo 500k then tutawapa faini za mbuzi mbuzi, na vingine vidogo vidogo, baada ya hapo mahari tuwaambie kuwa tunaenda kuitafuta then mtaangalia wenyewe baada ya kufika nyumbani!
Tuliporudi ndani tukakuta mzee anaonyesha kuwa na hasira hasira tu, kiasi kwamba mshenga wao akawa ameduwaa tu, basi mshenga wetu akaanza kujitetea pale, akaweka mezani sh. 500k mkaja wa mama, akawaambia mbuzi watatu wa uchafuzi 300k sijui koti la mjomba, mara blanketi ya wazee na vikolo kolo vingine kwa Kadri ya taratibu zao, ile pesa tuliyoenda nayo ikawa imekata!
Muda huo wote Nina hasira vibaya mnooo, ila najitahidi kuificha japo mpnz wangu aligundua kabisa kuwa nimechukia!
Tukawaambia hiyo mil. 4 tunaenda kuitafuta, mzee akasema "mkaitafute muilete hapa, au mutanitumia kwenye simu" tukawaambia sawa.
Muda wa kutoka nikakuta mpnz wangu ameshabeba mabegi anataka tuondoke wote, nikamwambia hapana unapswa kubaki nitakuja kuwachukua nikimalizia mahari, akagoma akawa analia wakati wote akiwa amenikumbatia, anaomba radhi kwa kilichotokea ila anaomba tuondoke wote, yeye hawezi kubaki Kijijini tena, nikamwambia hapana, unapswa kubaki mpaka tumalizane n'a mzee, akagoma kata kata, akawa amepiga magoti huku amekumbatia miguu yangu,machozi yanamtoka tuuu
Mzee wake alipotoka akaona mwanaye analia akasema "kama mnaobdoka wote nendeni tu" Mara mama mkwe akaja na dogo (mtoto wangu) akamshusha nilipokuwa, nikambeba mtoto nikamwambia mama mtoto asimame, bro na mshenga wetu wakaniita pembeni, mshenga akasema tuondoke nao, tukimuacha na wakahisi kuwa Kuna dalili za sisi kutorudi, watamuua huyu mtoto.
Basi kiahingo upande, tukawakubalia kuondoka nao, mama mkwe akaleta maharage na jogoo akataka tuondoke navyo, nikakataa kuchukua, nikamwambia tutabeba wakati mwingine, akagundua bado nina hasira, akamuita mtoto wake, akamwambia "mwambie mumeo amsamehe bure baba yako, amekosea sana, n'a mimi mama naomba atusamehe tu)
Tukaondoka zetu, kichwani nikiwa nimejaa mawazo mengi mnoo, kiasi kwamba sikuweza kujua niamue nini, tumefika Dar lakini moyoni nimejikuta sina tena interest ya kutengeneza undugu na familia ya mpnz wangu, japo yeye binafsi hana shida, lakini kwa namna tulivyopokelewa na tulivyoondoka, nilijisemea moyoni kwamba SITOKAA NIRUDI KIGOMA, WALA SITOKAA NIPELEKE HIYO MAHARI WALIYOSEMA, nasubiri mwanangu akue kue kidogo nimwambie mama mtoto kwamba hakuna namna naweza kuunganisha undugu na familia yake, japo namhurumia ila ndiyo hivyo tena!
Kweli tembea uone, all the way from Dar to Kigoma, naenda kukutana na aibu tu, anyway!
Kamzalisha kvip kwani huyo mwanamke alilazimishwa kuzalishwa si alikubali kwa ridhaa yake na ni mtu mzima anajua hili ni kosa na hili si kosaKamzalisha mtoto wawatu akaishia naye bila wazazi kuruhusu, anataka wazazi wa mwanamke wafurahie vijizawadi vyake.
kwa nini vijana mnataka mahari ichezee 1m,yani mnafanya kila namna 1m ipite kama bei elekeziNimeshuhudia jamaa ametoa mahari ng'ombe 20, lakini hesabu aliyopewa ni kila ng'ombe mmoja sh.50,000/=
Dah, unaroho ngumu sana mkuuNingekua mm hata 100 nisingetoa. Kwanza nilivoona amekasirika ningejifanya kukubaliana nae kwa kika kitu. Na kusema anisamehe fidia nitatoa pia. Yaan kumuaminisha kua Niko tayar kwa lolote atakalo. Baadae sasa tukishakuabaliana nawaambia leo nimekuja kuelewana mahari na gharama zote maana sikujua gharama na mahali. Waniruhusu nirudi siku nyingine kuvilipa.
Baada ya hapo nisingerudi. Huyo binti ningeondoka nae kufika mbele kidogo ningemtelekeza kwa mshenga na kuondoka milele. Nisingerudi kigoma kamwe. Na huyo mtoto wangemsomesha wao na kumtunza baadae akiamua kunitafuta atanitafuta.
Huo ndiyo umasikini wa kufikiria, "kusomesha ili waje watusaidie baadaye"Ndiyo ya mwanamke, ndiyo maana kila siku zinatungwa sheria za kumlinda mtoto wakike.we unafikiri huyo binti wazazi wake wamejibana kiasi gani ili kumsomesha mtoto wao usikute huyo mzee kauza mashamba na mifungo ili mtoto wake aje awasaidie wadogo zake.
Utoto unamsumbua huyo.Dah, unaroho ngumu sana mkuu
Mzee kazingua sana ila jamaa alifanya vyema kutuliza hasiramzee pia atakua na zile itikadi za kwamba jamaa ana hela[emoji23][emoji23][emoji23] we kutoka dar hadi kigoma ndani ndani huko sio poa[emoji119][emoji119]
Kwanz Pole sana kwa yaliyokukuta mmi yaliwahi nitokea ila yako kiboko ....ushauri wangu wale ni wazee wana mapungufu yao kwa mawazo yangu wew jishushe jaribu kuzungumza nao Wenda hata wao kule wana jutia wakati mwingine hasira ni hasara ...... japo ni kweli wamekosea ..... fanya ivi kwa amani ya moyowako maisha mengine yaendeleeNimekuwa kwenye mahusiano na mwanamke kutoka Kigoma tangu 2020, tulikutana chuo, na penzi likakolea haswaa!
Kipindi cha Covid penzi lilinoga zaidi kwani "Working from home" ilifanya muda wote tuwe pamoja, ilikuwa mwendo wa kwenda sokoni kununua mazaga zaga pamoja, tinaweka ndani then kila baada ya mlo ni mnyanduano tu, hatimaye binti akashika mimba!
Baada ya mimba kufikisha miezi minne bibie akaniambia ni bora aende kwao kwanza kwani kubaki tukiwa wawili hatuwezijua complications za mimba, nilikubaliana nae, nikajipiga kwa kadri ya uwezo wangu nikamkatia tiketi na vizawadi kidogo vya wazee akaenda kwao!
Akiwa kwao mawasiliano yetu yalikuwa vizuri kabisa mpaka akajifungua salama salmin, na mimi niliwajibika haswa mpaka dk. ya mwisho, hatimaye tukapata mtoto wa kiume.
Bibie baada ya mtoto kufikisha miezi 6 bila mimi kwenda kujitambulisha akatoa wazo la kurudi kwangu kwani alikuwa amechoka kuishi nyumbani kwao, nikamkaribisha tukaendelea na maisha ya sogea tuishi.
Mwaka jana December, ilitokea msiba kwao akalazimika kwenda msibani, nikamfanyia maandalizi vizuri kabisa, akaondoka.
Amekaa huko tangu December, mpaka juzi nilipoamua kufuata taratibu za kwenda kwao ili tusiendelee kuishi kimya kimya (tufanye kuwa official), nikajiandaa kwa mambo kadhaa kama nilivyokuwa nimeng'atwa sikio na mpenzi wangu.
Nimeanza safari kutoka Dar kwenda Kigoma (kwao), nikiwa nimeambatana na brother wangu wa damu, aisee kwao ni mbali, maana tulitembea siku 2 njiani, tulipofika mjini, safari ya kwenda kwao ikachukua masaa mengine 8, vumbi kali hatari, tulipofika Kijijini kwao tukaambiwa Burundi ni mwendo wa kutembea nusu saa tu.
Brother akaniuliza, "Hivi dogo hukuona wanawake mikoa yote tuliyopita mpaka kuja huku?" Nikamwambia mapenzi yana nguvu bro, sikuwahi kufikiria kama kuna siku ningesafiri umbali namna hii kufuata mwanamke tu. Tulipofika mjini tulitafuta mzee mwenyeji, anayejua mila na desturi za Kiha ili mambo yasiwe magumu.
Basi bwana, tumefika pale tumepokelewa vizuri wakaandaa utaratibu wa mjadala, mshenga akatambulisha na kuanza mazungumzo rasmi, hapo nilikuwa na zawadi ya baba mkwe na mama mkwe, nilinunua tangu Dar kwa upendo kabisa.
Wakataja kiasi cha mahari kuwa wanataka mil. 4.5, hapo tukashtuka kweli, kabla hatujakaa sawa wakataja mkaja wa mama sh. laki saba, jumla wanataka 5.2 Milioni!
Yule mzee tuliyeenda naye akaomba twende nje kwa mazungumzo, akatuuliza kama tulipewa mwongozo na tuliyekwenda kumuoa, nikamjibu ndiyo (alisema mahari kwao haizidi Milioni moja) na mkaja wa mama huwa ina-range kuanzia 100k - 200k, na mimi niliandaa 200k kama mkaja wa mama! Mzee akasema hapa kuna tatizo, huku haijawahi kutokea mahari kubwa kiasi hiki, akasema tutasimamia kwenye hiyo 1M na mkaja wa mama 200k, tukarudi ndani!
Mzee (mshenga) akaanza kuzungumza, kuwa sisi tuna mahari 800k na mkaja wa mama 100k, lakini pia tuna zawadi kwa ajili ya baba na mama, ambazo si sehemu ya mahari, ni zawadi tu ya kijana wetu kwenu, mzee akatoa zile zawadi akaweka mezani.
Mshenga wao akashukuru na kuanza kuzungumzia mahari yetu kuwa angalau tufanye mahari mil.4 mkaja wa mama 500k.
Kabla hajamaliza akasimama baba mkwe, akionyesha kukasirika akasema "Sitaki mjadala wa kitoto hapa, mimi ndiye baba wa x, mkaja wa mama laki 5, mahari yangu nataka Milioni 4, Sitaki mjadala wala kusikia kupunguziana, kwanza unabeba zawadi kutuletea nani amekutuma utununulie, tumekuomba sisi utuletee zawadi zako?"
"Kwanza huyu kijana anadharau sana, tangu mtoto azaliwe hajawahi kufika hapa nyumbani, anaishia kumtumia mwenzake pesa tu, sisi hajawahi kututumia pesa hata mara moja, tumepata msiba hajawahi kuja kutupa pole zaidi ya kupiga visimu vyake tu, sasa mimi nimeshasema mkaja wa mama laki tano, mahari Milioni 4, sitaki mjadala!"
Aisee nilijikuta nimejaa hasira mpaka basi, mshenga wetu akatutaka twende nje, akasema "huyu mzee inaonekana ana lake jambo, tusiingie kwenye mtego wake, iweni wapole, tuondoke salama, watu wa huku ni hatari sana, tukiwa na hasira tunaweza tusirudi salama, hii si dalili nzuri."
Tukajadili tuvyojiandaa pale, mzee akasema muhimu tuanze na mkaja wa mama, tuwawekee hiyo 500k then tutawapa faini za mbuzi mbuzi, na vingine vidogo vidogo, baada ya hapo mahari tuwaambie kuwa tunaenda kuitafuta then mtaangalia wenyewe baada ya kufika nyumbani!
Tuliporudi ndani tukakuta mzee anaonyesha kuwa na hasira hasira tu, kiasi kwamba mshenga wao akawa ameduwaa tu, basi mshenga wetu akaanza kujitetea pale, akaweka mezani sh. 500k mkaja wa mama, akawaambia mbuzi watatu wa uchafuzi 300k sijui koti la mjomba, mara blanketi ya wazee na vikolo kolo vingine kwa Kadri ya taratibu zao, ile pesa tuliyoenda nayo ikawa imekata!
Muda huo wote Nina hasira vibaya mnooo, ila najitahidi kuificha japo mpnz wangu aligundua kabisa kuwa nimechukia!
Tukawaambia hiyo mil. 4 tunaenda kuitafuta, mzee akasema "mkaitafute muilete hapa, au mutanitumia kwenye simu" tukawaambia sawa.
Muda wa kutoka nikakuta mpnz wangu ameshabeba mabegi anataka tuondoke wote, nikamwambia hapana unapswa kubaki nitakuja kuwachukua nikimalizia mahari, akagoma akawa analia wakati wote akiwa amenikumbatia, anaomba radhi kwa kilichotokea ila anaomba tuondoke wote, yeye hawezi kubaki Kijijini tena, nikamwambia hapana, unapswa kubaki mpaka tumalizane n'a mzee, akagoma kata kata, akawa amepiga magoti huku amekumbatia miguu yangu,machozi yanamtoka tuuu
Mzee wake alipotoka akaona mwanaye analia akasema "kama mnaobdoka wote nendeni tu" Mara mama mkwe akaja na dogo (mtoto wangu) akamshusha nilipokuwa, nikambeba mtoto nikamwambia mama mtoto asimame, bro na mshenga wetu wakaniita pembeni, mshenga akasema tuondoke nao, tukimuacha na wakahisi kuwa Kuna dalili za sisi kutorudi, watamuua huyu mtoto.
Basi kiahingo upande, tukawakubalia kuondoka nao, mama mkwe akaleta maharage na jogoo akataka tuondoke navyo, nikakataa kuchukua, nikamwambia tutabeba wakati mwingine, akagundua bado nina hasira, akamuita mtoto wake, akamwambia "mwambie mumeo amsamehe bure baba yako, amekosea sana, n'a mimi mama naomba atusamehe tu)
Tukaondoka zetu, kichwani nikiwa nimejaa mawazo mengi mnoo, kiasi kwamba sikuweza kujua niamue nini, tumefika Dar lakini moyoni nimejikuta sina tena interest ya kutengeneza undugu na familia ya mpnz wangu, japo yeye binafsi hana shida, lakini kwa namna tulivyopokelewa na tulivyoondoka, nilijisemea moyoni kwamba SITOKAA NIRUDI KIGOMA, WALA SITOKAA NIPELEKE HIYO MAHARI WALIYOSEMA, nasubiri mwanangu akue kue kidogo nimwambie mama mtoto kwamba hakuna namna naweza kuunganisha undugu na familia yake, japo namhurumia ila ndiyo hivyo tena!
Kweli tembea uone, all the way from Dar to Kigoma, naenda kukutana na aibu tu, anyway!
Appreciated!Pole sana kiongozi, umepata baba mkwe mkoloni sana.Ana tabia zote za Wazee Wa zamani.
Baba mkwe wako,kasimamia misingi ya Mila na tamaduni za kwao. Kimsingi ulikosea ulipo Anza kukaa na Binti Yao kienyeji,Hadi kufikia kumpa ujauzito , akaenda kujifungulia kwao(pasipo wewe kujurikana), akaja akafikwa na msiba(hukuoneka pia).
Matukio yote hayo uliyafanya na Binti Yao na kuwasiliana na Binti Yao tu. (hapa walitafasiri kuwa una jeuri).
Bado haitoshi ukapereka zawadi(unapereka usasa Kwa watu wenye misimamo ya kikoloni).
Sasa kwakuwa mambo yameshatokea, Haina budi kupambana, Ili muwe na mapenzi bora na salama wewe na familia yako. (Tambua mkwe ni Muha wa mipakani).
Jichange, ukipata ata 1M fanya kwanza mawasiliano na mshenga wako, Mshenga ndiyo afanye mawasiliano na baba mkwe wako! Amtaarifu kuwa "mmebahatika kupata 1M hivyo mnaomba aipokee, nyingine mtazidi kutuma mbeleni".Baada ya muda ukipata kama 500K fanya hivyo hivyo, alafu ndiyo uhanze Kutengeneza mawasiliano na mama mkwe wako. Kira Utakapo kuwa una wasiiliana nae mkumbushe amsalimie baba mkwe wako.
Baada ya muda tengeneza mazingira iyonekane mnapitia Hali ngumu sana, lakini unazuga kutuma ata pesa kidogo ya sukari na chumvi(hapa tuma Kwa mama mkwe au baba mkwe alafu mpe mwanao Simu awasalimu).Endelea kuwa Julia Hali na kushiriki mambo madogomadogo ya upande wa ukwenu.
Kuna muda atajirudi tu na anaweza kurudisha moyo nyuma, lakini pia mahali ata isipo isha siyo mbaya. Kikubwa umeonesha nia na utayari. Pia wamesha ona na Kutambua wewe ni mtu wa namna Gani.
Ndoa ni baraka toka pande zote mbili.
Halafu hasara inakuwa kwa nani?Kwao ni sawa tu ndiyo maana hawaja kushobokea, watalea mjukuu wao maisha yataendelea.