Nimetoka ukweni Kigoma, ila kama hii ndiyo aina ya wazee acha wabaki na watoto wao!

Nimetoka ukweni Kigoma, ila kama hii ndiyo aina ya wazee acha wabaki na watoto wao!

Wewe ndie mpuuzi tena huna hata chembe ya busara. Karma is real nawewe utapata watoto wa kike naombea sana suala hili likupate siku moja. Yaani umzalishe binti yangu halafu uje kujileta baada ya mwaka? Utachezea vitasa mpaka MOI wadhani umegongwa na Treni. Be Calm umeharibu wewe na ugomvi umeauanza wewe kwa mzee.
Mikwara nyuma ya keyboard
 
Nimekuwa kwenye mahusiano na mwanamke kutoka Kigoma tangu 2020, tulikutana chuo, na penzi likakolea haswaa!

Kipindi cha Covid penzi lilinoga zaidi kwani "Working from home" ilifanya muda wote tuwe pamoja, ilikuwa mwendo wa kwenda sokoni kununua mazaga zaga pamoja, tinaweka ndani then kila baada ya mlo ni mnyanduano tu, hatimaye binti akashika mimba!

Baada ya mimba kufikisha miezi minne bibie akaniambia ni bora aende kwao kwanza kwani kubaki tukiwa wawili hatuwezijua complications za mimba, nilikubaliana nae, nikajipiga kwa kadri ya uwezo wangu nikamkatia tiketi na vizawadi kidogo vya wazee akaenda kwao!

Akiwa kwao mawasiliano yetu yalikuwa vizuri kabisa mpaka akajifungua salama salmin, na mimi niliwajibika haswa mpaka dk. ya mwisho, hatimaye tukapata mtoto wa kiume.

Bibie baada ya mtoto kufikisha miezi 6 bila mimi kwenda kujitambulisha akatoa wazo la kurudi kwangu kwani alikuwa amechoka kuishi nyumbani kwao, nikamkaribisha tukaendelea na maisha ya sogea tuishi.

Mwaka jana December, ilitokea msiba kwao akalazimika kwenda msibani, nikamfanyia maandalizi vizuri kabisa, akaondoka.

Amekaa huko tangu December, mpaka juzi nilipoamua kufuata taratibu za kwenda kwao ili tusiendelee kuishi kimya kimya (tufanye kuwa official), nikajiandaa kwa mambo kadhaa kama nilivyokuwa nimeng'atwa sikio na mpenzi wangu.

Nimeanza safari kutoka Dar kwenda Kigoma (kwao), nikiwa nimeambatana na brother wangu wa damu, aisee kwao ni mbali, maana tulitembea siku 2 njiani, tulipofika mjini, safari ya kwenda kwao ikachukua masaa mengine 8, vumbi kali hatari, tulipofika Kijijini kwao tukaambiwa Burundi ni mwendo wa kutembea nusu saa tu.

Brother akaniuliza, "Hivi dogo hukuona wanawake mikoa yote tuliyopita mpaka kuja huku?" Nikamwambia mapenzi yana nguvu bro, sikuwahi kufikiria kama kuna siku ningesafiri umbali namna hii kufuata mwanamke tu. Tulipofika mjini tulitafuta mzee mwenyeji, anayejua mila na desturi za Kiha ili mambo yasiwe magumu.

Basi bwana, tumefika pale tumepokelewa vizuri wakaandaa utaratibu wa mjadala, mshenga akatambulisha na kuanza mazungumzo rasmi, hapo nilikuwa na zawadi ya baba mkwe na mama mkwe, nilinunua tangu Dar kwa upendo kabisa.

Wakataja kiasi cha mahari kuwa wanataka mil. 4.5, hapo tukashtuka kweli, kabla hatujakaa sawa wakataja mkaja wa mama sh. laki saba, jumla wanataka 5.2 Milioni!

Yule mzee tuliyeenda naye akaomba twende nje kwa mazungumzo, akatuuliza kama tulipewa mwongozo na tuliyekwenda kumuoa, nikamjibu ndiyo (alisema mahari kwao haizidi Milioni moja) na mkaja wa mama huwa ina-range kuanzia 100k - 200k, na mimi niliandaa 200k kama mkaja wa mama! Mzee akasema hapa kuna tatizo, huku haijawahi kutokea mahari kubwa kiasi hiki, akasema tutasimamia kwenye hiyo 1M na mkaja wa mama 200k, tukarudi ndani!

Mzee (mshenga) akaanza kuzungumza, kuwa sisi tuna mahari 800k na mkaja wa mama 100k, lakini pia tuna zawadi kwa ajili ya baba na mama, ambazo si sehemu ya mahari, ni zawadi tu ya kijana wetu kwenu, mzee akatoa zile zawadi akaweka mezani.

Mshenga wao akashukuru na kuanza kuzungumzia mahari yetu kuwa angalau tufanye mahari mil.4 mkaja wa mama 500k.

Kabla hajamaliza akasimama baba mkwe, akionyesha kukasirika akasema "Sitaki mjadala wa kitoto hapa, mimi ndiye baba wa x, mkaja wa mama laki 5, mahari yangu nataka Milioni 4, Sitaki mjadala wala kusikia kupunguziana, kwanza unabeba zawadi kutuletea nani amekutuma utununulie, tumekuomba sisi utuletee zawadi zako?"

"Kwanza huyu kijana anadharau sana, tangu mtoto azaliwe hajawahi kufika hapa nyumbani, anaishia kumtumia mwenzake pesa tu, sisi hajawahi kututumia pesa hata mara moja, tumepata msiba hajawahi kuja kutupa pole zaidi ya kupiga visimu vyake tu, sasa mimi nimeshasema mkaja wa mama laki tano, mahari Milioni 4, sitaki mjadala!"

Aisee nilijikuta nimejaa hasira mpaka basi, mshenga wetu akatutaka twende nje, akasema "huyu mzee inaonekana ana lake jambo, tusiingie kwenye mtego wake, iweni wapole, tuondoke salama, watu wa huku ni hatari sana, tukiwa na hasira tunaweza tusirudi salama, hii si dalili nzuri."

Tukajadili tuvyojiandaa pale, mzee akasema muhimu tuanze na mkaja wa mama, tuwawekee hiyo 500k then tutawapa faini za mbuzi mbuzi, na vingine vidogo vidogo, baada ya hapo mahari tuwaambie kuwa tunaenda kuitafuta then mtaangalia wenyewe baada ya kufika nyumbani!

Tuliporudi ndani tukakuta mzee anaonyesha kuwa na hasira hasira tu, kiasi kwamba mshenga wao akawa ameduwaa tu, basi mshenga wetu akaanza kujitetea pale, akaweka mezani Tsh. 500k mkaja wa mama, akawaambia mbuzi watatu wa uchafuzi 300k, sijui koti la mjomba, mara blanketi ya wazee na vikolo kolo vingine kwa Kadri ya taratibu zao, ile pesa tuliyoenda nayo ikawa imekata!

Muda huo wote nina hasira vibaya mno, ila najitahidi kuificha japo mpenzi wangu aligundua kabisa kuwa nimechukia. Tukawaambia hiyo mil. 4 tunaenda kuitafuta, mzee akasema "Mkaitafute muilete hapa, au mutanitumia kwenye simu," tukawaambia sawa.

Muda wa kutoka nikakuta mpenzi wangu ameshabeba mabegi anataka tuondoke wote, nikamwambia hapana unapaswa kubaki nitakuja kuwachukua nikimalizia mahari. Akagoma, akawa analia wakati wote akiwa amenikumbatia, anaomba radhi kwa kilichotokea ila anaomba tuondoke wote, yeye hawezi kubaki kijijini tena. Nikamwambia hapana, unapaswa kubaki mpaka tumalizane na mzee, akagoma kata kata, akawa amepiga magoti huku amekumbatia miguu yangu, machozi yanamtoka tu!

Mzee wake alipotoka akaona mwanaye analia akasema "Kama mnaondoka wote nendeni tu!" Mara mama mkwe akaja na dogo (mtoto wangu), akamshusha nilipokuwa, nikambeba mtoto nikamwambia mama mtoto asimame, bro na mshenga wetu wakaniita pembeni, mshenga akasema tuondoke nao, tukimuacha na wakahisi kuwa kuna dalili za sisi kutorudi, watamuua huyu mtoto.

Basi kishingo upande, tukawakubalia kuondoka nao, mama mkwe akaleta maharage na jogoo akataka tuondoke navyo, nikakataa kuchukua, nikamwambia tutabeba wakati mwingine, akagundua bado nina hasira. Akamuita mtoto wake, akamwambia "Mwambie mumeo amsamehe bure baba yako, amekosea sana, na mimi mama naomba atusamehe tu."

Tukaondoka zetu, kichwani nikiwa nimejaa mawazo mengi mno, kiasi kwamba sikuweza kujua niamue nini. Tumefika Dar lakini moyoni nimejikuta sina tena interest ya kutengeneza undugu na familia ya mpenzi wangu, japo yeye binafsi hana shida, lakini kwa namna tulivyopokelewa na tulivyoondoka, nilijisemea moyoni kwamba sitokaa nirudi Kigoma, wala sitokaa nipeleke hiyo mahari waliyosema.

Nasubiri mwanangu akuekue kidogo nimwambie mama mtoto kwamba hakuna namna naweza kuunganisha undugu na familia yake, japo namhurumia ila ndiyo hivyo tena.

Kweli tembea uone, all the way from Dar to Kigoma, naenda kukutana na aibu tu, anyways.

Mimi namuunga mkono bro robert heriel sitakuja pokea mahali ya mtoto wangu wa kike kama nitampata. Haya mavitu ya ovyo mno hayana hata mantiki
 
Umemaliza mkuu...wewe ndio mwenye kuamua maisha yako,huyu mzee njaa yake ndio imekufanya usanuke...mimi nlikaa 8yrz bila kufika kwao ila baadhi ya ndgu zake walinijua,baba mkwe aliniambia mahari nilipe ya kimila tu...kuona familia maskini ni kujiongezea matatizo
Usinitishe bhanaaa, kwani nilibaka?
Mimba ni matokeo ya nyege zetu, haina lawama hiyo!
 
Huyu hajui kila jamii ina tamaduni zake, huyu angekuwa kamfanyia binti waki Zanzibar ndiyo angejua vizuri ni jambo baya la kuishi kinyumba na binti wawatu bila ndoa, kule Zanzibar angefungwa jela kwa kosa la kutorosha binti chini ya uangalizi wa wazazi na kumbaka na kuishi naye kinyumba yani mpaka leo angekuwa yupo mahabusu, yani Wazanzibari wanatushangaa sana sisi watanganyika tunaishi na wanawake bila ndoa, hii tabia ya hovyo wazanzibari hawana ya kuishi kinyumba na mtoto wa mtu.
Hao wazenji kesi za kulawiti wanamalizana kimyakimya...hawana lolote
 
Kwenye hizi mambo waamua kuoa kabla ya kuwa wakataa ndoa hukutana na visanga vingii mnoo.
Nilichumbia kisha nikalipa mahari na faini zoote.
Dah kumbe mama mkwe hataki binti aolewe.
Anataka abaki home amrithishe uchawi.
Nilianza kwa kupoteza kazi mara 5,biashara kufeli,mali kisha mahusiano na familia then nikamalizia na marafiki mpaka nakuja kushtuka ni baada ya miaka 10 nishaisha mbayaa.
Yaani utasikia mama anauliza tuu hivi baba mmepanga kufunga ndoa lini maana muda unaendaa eeehh kumbe nilikuwa nakosea kumjibu bhana wee muda ukikaribia tuu matatizo lukukii hakuna ndoaa.
Sasa nimeamua kumuacha ila binti hatakii,sikai nae nimekimbia na nimemuachia kila kitu na tuna watoto nimemuachia.
Wakuu sio kila mlango ni wa kuoa tuu,chunguzeni kwanza.
Kataa ndoa haiji tuu ghafla, kuna chanzo nyuma ya pazia.
Hili balaa
 
Mkuu hakuna namna hapo. Sasa ni aidha umuache mke ili mtoto ateseke kuwafurahisha wazazi na kufurahisha nafsi yako lakini pia kunuumiza mkeo au ishi na mke ili uwaumize wazazi wake.

Mwisho na Kwa umuhimu kupanga ni kuchagua. Hapa tutakushauri mengi Ila siku yakikupata ya kukupata hutotuona kwenye shida yako mkuu
Waha ni wanga haratariiii nyie mnamshaurii kwa mlengo wa macho ya nyama
Hawa watu wasikienii
 
Wazee wengine huwafanya watoto wao wa kike ni mtaji
Nalog off
 
Mimi namuunga mkono bro robert heriel sitakuja pokea mahali ya mtoto wangu wa kike kama nitampata. Haya mavitu ya ovyo mno hayana hata mantiki
Hakuna tusi baya ambalo binti yako atatukanwa likamuumiza yeye na wewe pamoja kama kumuozesha bure au kumuozesha kwa mahari sawa na bei ya kununua changudoa. Mzazi taja mahari reasonable kwa kulingana na uchumi wa mkweo.
 
Ishawah nikuta hii ,siku nzima ilivurugika aisee siku ya kutoa mahari haitakiw muende watu wenye hasira maana wazaz wa bint wanakela case yangu nilimpa bint mimba ina 8 month ndo naenda kujitambulisha wabena noma kunamjomba wake wife alikuwa anakiherehere balaaa niliondoka kwa hasira mshenga alifanya kaz ya ziada kuja kuniomba nisitumie hasira bint akawa analia tu
 
Wewe ndo unawajua waha sasa ,hao watu wanaubaguz Sana kwa kabila lingine naandika haya nikiwa na experience ya kuish nao
Umaskini taabu sana na ubaguzi wa waha kwa makabila mengine ndio shida hapo, una huruma sana, ningekuwa mimi hakika ningewaacha wote mtoto na mama ndio basi tena, sipendi dharau na huyo mzee ningemueleza mila za kabila langu ili aone utofauti, sipendi ujinga kabisa, mi nikichukia nakuonesha waziwazi sitaki ujinga
 
Hilo lizee Ni Li ujinga la karne

Tuna mzee mingi mipuuzi tu huku mitaani

Mpaka unajiuliza huyu haoni uzee Ni busara

Huyo mzee hana busara hana stara hana ubinadamu yaani Ni mjinga tu

Pole
 
Haya mambo huwa siyapend ila kuna mmoja kajiingiza kinguvu wakat mimi huwa sinaga ratiba ya haya mambo,watakubal tu yeye na familia yake,bahat nzur baba mkwe hayupo
Hili kama langu tu nna binti ananielewa na anaforce nimuoe an kanibana na ana mama ila hana baba lakin pia mm nasom chuo na sina mpango wa kuoa kaja gheto naishi nae ila wao wanajuh mtoto wao yuko mjini kikazi hàpa nasubl nione nini ni nini
 
Hili kama langu tu nna binti ananielewa na anaforce nimuoe an kanibana na ana mama ila hana baba lakin pia mm nasom chuo na sina mpango wa kuoa kaja gheto naishi nae ila wao wanajuh mtoto wao yuko mjini kikazi hàpa nasubl nione nini ni nini
Kwanza kabisa hakikisha humpi mimba kama ni kumeza p2 mmezeshe kila siku au akachome sindano za uzazi wa mpango maana akipata mimba atakuletea shida

Sahv mimi naishi nje ya malengo
 
KWAni
Hakuna tusi baya ambalo binti yako atatukanwa likamuumiza yeye na wewe pamoja kama kumuozesha bure au kumuozesha kwa mahari sawa na bei ya kununua changudoa. Mzazi taja mahari reasonable kwa kulingana na uchumi wa mkweo.



Kwanini upokee pesa KWA ajili ya binti YAKO hujanipa sababu.
 
Back
Top Bottom