Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,692
- 23,038
Kama ilivyo kwa raia wengi wa Tanzania ambao hubahatika kwenda ng'ambo, mimi pia nilipata bahati hiyo kwenye miaka ya tisini.
Nimeishi miaka mingi ughaibuni kiasi cha kuwa mwenyeji kabisa na nikiwa naishi na kufanya kazi.
Lakini kama ilivyo tabia yetu sisi waafrika huwa hatupendi kusahau nyumbani kwetu tutokako kwa kuhakikisha ndugu zetu wanapata angalau pesa ya mkate au hata soda.
Sasa hivi karibuni niliamua kuanza kutuma pesa nyumbani Tanzania kwa kutumia mtandao wangu wa benki moja kubwa tu na maarufu ughaibuni(jina nalihifadhi kwa sasa) kwenda kwenye akaunti ya ndugu yangu mmoja Tanzania katika moja ya benki maarufu pale Dar-es-Salaaam (jina nalihifadhi kwa sasa).
Lakini kwa kuwa ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kufanya hiyo transaction, nikajaribu kutuma fedha kiasi tu kama paundi 60 ambayo inatoa fedha ya madafu kama tshs 150,000 hivi.
Benki yangu ya ughaibuni wakathibitisha kwamba pesa imekwenda kwa kutumia details zote za Account name,Account number SWIFT CODE NA BIC CODE au Bank Identifier Code na IBAN.
Lakini yule ndugu yangu alipokwenda pale ofisi za benki hiyo zilizopo barabara ya Samora akaambiwa kwamba hakukuwa na ingizo la fedha yoyote kwenye akaunti yake kutoka Ughaibuni na hakuna kitu cha namna hiyo.
Mimi mwenyewe nikajaribu kuwatatuta watu wa benki hiyo pale Dar na majibu yao yalikuwa ni yake yale kwamba hakuna ingizo, pamoja na kuwapatia details zote za jinsi transfer ilivyofanywa na kwamba kwa huku kila kitu kilikuwa kimefanywa kwa asilimia 100.
Sasa najaribu kutafuta sababu za fedha kutoingizwa kwenye hiyo akaunti na utata huu kuhusiana na jambo hili ukiwemo ushauri wa watu wanaofanya kazi benki hasa wataalam wa international clearance.
Nina imani na vyombo vyetu vya fedha Tanzania isipokuwa naomba kuwa clear na hii kitu maana haieleweki kabisa.
Naombeni ushauri wenu, ahsante.