Nimetumia dakika nane (8) kupika na kuivisha njugumawe!

Mlolongo

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2019
Posts
3,483
Reaction score
6,257
Nimenunua njugumawe nusu kilo.
Huku Makongo Juu wanauza 1 kg = 3,400

Nikachambua, nikatia kwenye thermos flask kisha nikaweka maji ya moto (100°c), nikafunga chupa. Hapo ilikua saa tatu usiku.


Asubuhi nikafungua thermos, nikamimina njugumawe kwenye sufuria.


Zilikua hazijalainika ile kuiva kabisa. Nikabandika sufuria kwa jiko.

Nikasema wakati zinachemka, nimalizie movie ya "Kill Chain - 2019" 📺


Dakika tano tu, zishalainika kabisa, ningechelewa zingekua uji.

Nikakata kitunguu🧅 , nikaunga... Nikamalizia na tui la nazi 🥥.


Ebana eeehhh... Tamu sana.

Nilikua nimepanga kupika na wali, halafu njugu ziwe mboga, nimebadili mawazo. Wali sipiki tena.

Nakula hizi hizi njugu kama main dish 🍚. Sema zinaniga, I think nahitaji juice hivi au chai/maziwa!!



Muda niliotumia kuzibandika jikoni hadi naweka 🥥 ni dakika nane tu.
 
Hapo mkuu umepika usiku kucha 😅😅😅😅 Geto limeenea leta mdada wa Ardhi akusaidie majukumu ye anasevu kulipa chumba na wewe 'unapona' nadhani umeelewa 😎
 
Njugu na makande hapana kabisa, siwezi kula
 
Acha bangi mkuu🤣🤣
 
Hivi mfano nikiloweka maharage yanakuwa matamu kweli?kama ya kupikia kwa mkaa?
Sijawahi notice utofauti
Japo silowekagi
Ila nilishawahi kula yaliyofanywa hivyo.

Me nikiamka dk 70 kwenye electric pressure cooker napata maharage fresh.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…