Nimetumiwa pesa toka CRDB kuja Airtel money tangu jana Alhamis hadi leo Ijumaa haijaingia

Nimetumiwa pesa toka CRDB kuja Airtel money tangu jana Alhamis hadi leo Ijumaa haijaingia

Mamujay

Senior Member
Joined
Dec 24, 2022
Posts
149
Reaction score
345
Naombeni msaada Nifanyaje jana mafundi walikuwa site nusu wanipige makofi.

Pesa imetumwa kutoka CRDB kuja Airtel money tangu jana alhamis saa 12 jion hadi saiz naandika ni saa 12 asubuh pesa haijafika CRDB Wanasema pesa imeshatumwa Airtell Money wanasema hakuna muamala wowote.
 
Kuna mwamba mmoja wa CRDB keshainywea pombe kukaribisha weekend.

Hapo umeangukia kwa majambazi wawili. CRDB ni mabaradhuli na hao Airtel ndio majangili kabisa. Huwa wana majibu mepesi mno katika kila issue
 
Hilo tatizo hata mimi lilinitokea Jana jioni nilituma hella toka Airtel money kwenda tigo pessa hella haikufika Kwa mhusika lakini nilivyowapigia Airtel wakaurudisha mwamala kwangu, wakaniambia nisifanye mwamala Kwa Jana kwani mfumo Airtel money ulikuwa na hitirafu.
 
Naombeni msaada Nifanyaje jana mafundi walikuwa site nusu wanipige makofi,
Pesa imetumwa kutoka CRDB kuja Airtel money tangu jana alhamis saa 12 jion hadi saiz naandika ni saa 12 asubuh pesa haijafika CRDB Wanasema pesa imeshatumwa Airtell money wanasema hakuna muamala wowote
Mfumo wa simbank wa CRDB umekufa toka juzi.
 
Kiufupi Kuhusu Pesa za Kimtandao kwa Tanzania tuko nyuma sanaaaaaaaa. Wenzetu apo Kenya mambo ni sawa sana. Uku kwetu sijui tuna shida gani
 
airtel na Crdb bank njooni huku mtoe ufafanuzi pls!
Nami wiki jana nilihamisha kutoka Airtel money kwenda Ttcl muamala haukufika!!!

Airtel customer care walisema watarejesha pesa in 24 hrs, siku ya 4 Leo sijaona msg!
 
Hata Mpesa ilishantokea. kutoka mpesa kwenda tigopesa. nimetuma zaidi ya lak 2 ikakaa kimya. Muhuzika nimtumiaye hajapata kitu. Nikaangalia salio halijapungua. Sasa nikazema ngoja nitume tena. Pia kimya na muamala kwangu salio lile lile. Basi nikamwambia muhusika nimetuma mara mbili. Yeye hakuamini inakuaje haijaenda.
Nikawapigia voda wakajibu kutumia marobot juwa mitambo inaahughulikiwa. Kesho wakatuma miamala yote 2 badala ya kurudisha. ,Muhusika kwa kuwa tunaelewana ikabidi aniludishie muamala 1 kwa makato yangu
 
Nimetuma pesa karibia wiki sasa toka crdb kwenda airtel money, haijafika na imekatwa. Kila siku crdb wananipa majibu ya uongo.
 
Back
Top Bottom