Dr wa Manesi
JF-Expert Member
- Aug 19, 2024
- 997
- 1,220
Nilikuwa naongea na watoto (wanafunzi) kama 100 hivi. Basi katikati ya maongezi ikanijia chafya, nikaziba mdomo tu nilijua kuwa sina tatizo lolote na ni chafya ya kawaida tu kama zile zingine. Ajabu ni kuwa nilipopiga tu ile chafya lilitokea pande kubwa puani la kamasi mbichi na nzito sana loliloenda kumuangukia kwenye paji la uso mmoja ya wasichana waliokaa pale. Sina mafua Wala kikohozi Sasa hiki ni nini?!!! Nahisi Kuna mtu kanichezea mchezo wa kishirikina Ili niumbuke.......na kweli nimeumbuka kwani nimechekwa mno na kushindwa kuendelea tena kuongea. Mawazo yenu wadau.