Nimeumia kisa mapenzi

Nimeumia kisa mapenzi

Hatuwezi kusoma vitu vigumu kila wakati tunahitaji vitu vizuri tupumzishe akili.
Akili nani anakuambia kuwa inachoka kisa tu inapenda Raha ndio mana inajitetea , akili haichoku nikuambie ni sawa na jicho ,moyo,sikio,mdomo havichoki kufanya kazi zao.
Utasikiliza mziki,ukachoka tunacheki movie mara unapiga stori mara unaongea ni kazi ya akili iyo
 
SEHEMU YA TATU

“Ndiyo Desmond! Uchunguzi unaendelea hivyo ni lazima tutoe taarifa kila hatua” Alieleza askari huyo kwa njia ya simu, Desmond alitamani kumwambia Askari huyo asirushe chochote lakini alishindwa sababu angeulizwa kwanini anataka taarifa zisiruke alafu angekosa jibu la kumpa, alikata simu akairudisha kwenye mfuko wake.

Siku zilienda, Desmond na Noela walipanga kuvishana pete ya uchumba ili mahusiano yao yatambulike, japo Desmond alikuwa na Mke tena aliyefunga naye ndoa kanisani ila hakutaka kusema chochote kile, akili yake ilizidi kumwambia kuwa Mandy atakufa muda wowote ule, walipanga siku ya tukio hilo, hofu ya Desmond ikawa kwa Lucia kama atapewa hiyo taarifa alafu akahudhuria sherehe hiyo fupi ya kuvishana pete na kama unavyojuwa Lucia alikuwa akifahamu kuwa Desmond ana Mke tena yupo Hoi Hospitalini.

Miongoni mwa Watu ambao Noela aliwaarika alikuwa ni Lucia sababu alikuwa ni rafki yake wa zamani, Desmond alimwambia Noela hana sababu ya kuarika Watu wengi hivyo sababu ni sherehe fupi ambayo inawahusu wao na baadhi ya ndugu.

“Sijawahi kuvishwa pete katika Maisha yangu Joshua, wewe ndiye Mwanaume wangu wa kwanza kunipeleka kwenye ulimwengu huu hivyo ni fahari kwangu kuona marafiki zangu wanakuja hapa” Alisema Noela siku moja baada ya Desmond kulalamika kuwa anaarika Watu wengi.

“Najuwa Mpenzi wangu lakini tukio hili ni la kushuhudiwa na Watu wachache sana, Aaah…” Alisema Desmond huku bado akitafunwa na hofu ya Lucia kuarikwa

“Joshua nimearika marafiki wachache sana, usiwe na wasiwasi kuhusu hilo. Nakuelewa Mume wangu mtarajiwa” Alisema Noela kisha alisema

“Naenda chooni mara moja” Aliaga kisha aliondoka lakini aliacha Kitabu chenye majina ya Watu walioarikwa kwenye shughuli hiyo, haraka Desmond alikifunua, kama alivyofikiria ndivyo ilivyokuwa, Lucia aliarikwa kwemye shughuli hiyo, jina lake lilikuwa la tatu kutoka juu akimaanisha kuwa ni miongoni mwa Watu muhimu zaidi kwake, kijasho kilimtoka Desmond, alifikiria haraka haraka afanye nini ili kumzuia Lucia asiende kwenye tukio hilo la kuvishana pete maana kama Lucia ataenda basi mambo mawili yatajulikana, kwanza ni jina lake halisi ambalo siyo Joshua na pili ni kwamba ana Mke hivyo haruhusiwi kuowa Mke mwingine kwa mujibu wa sheria za dini ya Kikristo.

Walikuwa kwenye moja ya Bustani nzuri wakizungumza, Desmond alikaa kwenye kiti akiwa amechoka mwili na akili, akakumbuka Maswali aliyoulizwa na Lucia juu ya jaribio la kutaka kuuawa kwa Mandy, moja kwa moja alijuwa mambo mengi yanaenda kujulikana kama ataruhusu Lucia kuwepo kwenye Shughuli hiyo, akiwa anaendelea na tafakari Noela alirudi akamkuta Desmond akiwa katika hali ya mawazo sana

“Kulikoni Bebe?” Alihoji, kijasho kilikuwa kikimtoka Desmond, Noela alimpa kitambaa Desmond ili ajifute jasho

“Unaumwa?” Aliuliza tena Noela

“Ndiyo ghafla tu sijisikii vizuri, usijali nitakuwa sawa” Alisema Desmond kisha alijifuta jasho alafu akashushia maji ya baridi, Noela aliketi, aliona kitabu kimefunguliwa

“Au kwasababu umeona nimearika idadi kubwa ya Watu Joshua?” Aliuliza Noela akiwa mwenye wasiwasi huwenda Desmond ana hasira

“Hapana Noela ni tofauti na ufikiriavyo, ni ghafla tu najisikia vibaya” Alisema Desmond, Noela alisema

“Ngoja nimpigie rafiki yangu ni nesi”

“Rafiki yako nesi?” Alihoji Desmond akiwa katika hali tofauti kabisa hata Noela alishangaa maana Mtu ambaye alionekana kuwa na hali mbaya

“Mbona umeshtuka sana niliposema nampigia rafiki yangu nesi? Si wewe ulikuwa katika hali ya homa?” Kiukweli Noela alizidi kumshangaa Desmond

“Hukuwahi kuniambia kama una rafiki yako Nesi” Alisema Desmond, Noela alitabasamu akagundua ni kweli hakuwahi

kumwambia Desmond istoshe alikutana na rafiki yake huyo siku chache zilizopita

“Oooh ni kweli, ni rafiki niliyesoma naye. Tulipotezana muda mrefu sana ni majuzi tu ndiyo tumeonana. Hata hivyo nimemuarika kwenye shughuli yetu lakini nakumbuka kama niliwahi kukwambia, atakuja utamuona anaitwa Lucia” Alieleza Noela kisha alimpigia Lucia lakini kabla hata simu haijaita Desmond alimkatisha Noela

“Huna haja ya kumsumbua nitakuwa sawa tu” Alisema Desmond huku akitafakari kuhusu Lucia, aliona wazi vita kubwa inaenda kupigwana mbeleni

“Hivi unajua Joshua sikuelewi, unatokwa jasho namna hiyo lafu hutaki nimuite Lucia?” Aliuliza Noela

“Nimesema nitakuwa sawa, tunaweza ondoka hapa” Alisema Desmond kisha alisimama, Noela naye alisimama japo kwa kuchukia kisha waliongozana hadi kwenye gari ya Desmond, walianza safari ya kuondoka pale kuelekea nyumbani anakoishi Noela, baada ya kumaliza mizunguko yote alirudi kwenye nyumba aliyokuwa akiishi na Mandy.

Kuna dokumenti alizihitaji akaenda kufungua kabati la Mandy ambalo alikuwa akiweka baadhi ya vitu vyake muhimu kisha alitoa Mkataba wenye umiliki wa Mali za Mandy yakiwemo Mashamba, kampuni ya Kuuza Vipuri vya Magari na Mgodi mmoja.

Alipozipata nyaraka hizo muhimu alizipitia, alithibitisha ndizo alizokuwa akizihitaji kwa wakati huo, kisha alimpigia Mtu mmoja simu akasema

“Joel ninazo, nakuja ofisini kwako” Alisema Desmond kisha alikata simu, aliingia kwenye gari akaelekea kwa Joel ambaye alikuwa ni Mwanasheria wa Mandy.

Alifika ofisini kwa Mwanasheria huyo aliyeitwa Joel, alikuwa ni Mtu makini aliyefahamu kilichotokea kati ya Mandy na Mume wake Desmond, walitazmana huku nafsi zao zikizungumza, walionesha kujuwa hasa walichodhamiria kufanya. Haraka Desmond alizama kwenye mkoba wake akatoa zile nyaraka muhimu za Mandy.

Joel aliketi akazipitia kisha akamwambia Desmond baada ya dakika kadhaa za ukimya kupita

“Ni zenyewe” Alisema hivyo huku akizidi kutafakari jambo, Desmond aligundua kisha akamuuliza

“Unafikiria nini Joel?” Alimuuliza Mwanaume huyo mweupe mwenye mvi kiasi ambaye umri wake ulienda kidogo

“Nafikiria kuhusu Mandy, tunachofanya ni kumzika akiwa hai, nakumbuka mengi ya zamani” Alisema Joel huku akifuta chozi jicho moja

“Wewe ni mshamba sana Joel, hukuzaliwa kuwa masikini. Huoni aibu? Huhisi haya machoni pako? Mwaga wino hatukuanza leo” Alisistiza Desmond huku akizidi kumshangaa Joel, basi Joel alichukua peni akaiweka juu ya nyaraka hizo akamwambia Desmond

“Hiki ninachokifanya kinaenda kubadili kila kitu katika Maisha yangu, uadilifu na uaminifu wangu kwa Mandy unazikwa baada ya kutia saini nyaraka hizi Desmond. Natamani kurudi nyuma na kuzuia hili lisitokee” Alisema Joel huku akizidi kujilaumu

“Mandy ni wa leo wa kesho, unataka afe ili nihangaike na familia yake si ndiyo?” Alisema Desmond kisha alimlazimisha Joel kutia saini ya makubaliano kuwa Mandy amempa mali hizo Mume wake Desmond, kwa Mamlaka aliyonayo Joel alitia saini

“Ooooh!! Sasa umefanya kwa upande wako, kilichobakia ni kule Hospitali, twende tukamalize mchezo” Alisema Desmond kisha alisimama

“Desmond una uhakika kuwa Mandy atakufa?” Joel aliuliza

“Asipokufa atakuwa na mapungufu kwenye ubongo wake, ni lazima atapoteza kumbukumbu tu” Alisema Desmond kwa kujiamini

“Baada ya hapa nitakupatia kiasi kikubwa cha pesa kisha utakuwa na jukumu la kuitunza siri hii” Alisema Desmond kisha walitoka wakaelekea kule Hospitalini.

Walipofika walimkuta Lucia akiendelea kumuangalia Mandy maana ndiyo jukumu lake kuu alilopewa, Lucia aliwatazama Desmond na Joel Mwanasheria.

“Samahani Lucia kuna jambo Mwanasheria wa Mandy amekuja kufanya” Alisema Desmond, Lucia alishtuka akamuuliza Desmond

“Unahisi Mandy hatoweza kuamka?” Alihoji akiwa kama muuguzi namba moja wa Mandy, alihisi kuna jambo lisilo la kawaida ndiyo maana Mwanasheria huyo alienda Hospitalini. Desmond alimvuta pembeni Lucia akamwambia

“Siyo kila jambo linaendeshwa kimihemko Lucia, mambo mengine unapaswa kuyaangalia tu. Wewe ni nesi na utabakia kuwa nesi” Alisema Desmond kwa sauti iliyojaa ukomavu huku akiwa amemshika mkono kwa nguvu Lucia

“Hata kama Desmond, nimemungalia Mke wako kwa kipindi kirefu. Lipo tumaini ndani yake, kuwa na subra” Alijibu Lucia

“Unajuwa nini wewe Lucia? Unajuwa nini kuhusu familia yangu!? Kumuuguza Mandy ni jukumu lako sababu unalipwa msharaha hufamyi bure hapa” Alisema Desmond kwa sauti ile ile

“Desmond! Desmond vuta subra Mkeo ataamka tena” Alisema Lucia akionesha kuumizwa sana, mara nyingi Mtu anapokuwa mgonjwa sana alafu Mwanasheria akaja basi kunakuwa na uwezekano Mkubwa sana kuwa kuna mjadala wa mali za mgonjwa, Lucia aliligundua hilo

Basi Desmond na Lucia walirudi huku Lucia akitaka kusema kitu lakini Desmond hakutaka kumsikiliza Lucia, Mwanasheria Joel alitoa wino kisha alipakaza kwenye kidole cha Mandy. Akaweka saini kwenye zile karatasi, Desmond alikabidhiwa karatasi hizo kisha alizisoma tena, Lucia alichungulia kuona kulikuwa kumeandikwa kitu gani kwenye karatasi hizo.

Aliona maandishi yaliyosomeka

“MAKABIDHIANO YA MALI KATOKA KWA MANDY KWENDA KWA DESMOND”

Alishtuka sana Lucia, alimtazama mara mbili mbili Desmond, jinsi alivyokuwa amemchukulia Mwanzo aliona kabisa alimchukulia tofauti kabisa kwa jinsi alivyo sasa, alimuona Desmond kuwa ni mkatili na jambo ambalo alikuwa analifanya pale lilijaa tamaa za kutosha, alishindwa hata aseme nini. Baada ya kumaliza Desmond na Mwanasheria Joel waliondoka Wodini, Lucia alichoka roho na mwili huku akihisi kabisa viungo havifanyi kazi tena.

Alijikutana akikaa chini taratibu huku akijawa na mshangao mno, aliona kabisa kitendo kile kilifanywa bila ridhaa ya Mandy. Alifuta chozi lake lililoanza kumdondoka kisha alijishangaa ni kwanini alikuwa akilia, alinyanyuka kisha alimtazama sana Mandy, alimuonea huruma. Alitamani aamke ili ashuhudie kilichokuwa kinafanywa na Mume wake, akili ya Lucia ikamwambia

“Basi Desmond anaeeza akamuuwa Mke wake kama ameweza kumsainisha akiwa hoi kitandani basi anaweza akaondoa uhai wake” Akili ya Lucia ilifika ukomo wa kutafakari jambo hilo.

Usiku Lucia aliondoka Hospitalini akiwa hoi Bin taabani, alipitia baa akaagiza pombe akanywa maana jambo lile halikuwa la kawaida hasa kwa Mawanaume ambaye alimpenda ila hakuwahi kumwambia, aliona moyo wake ulikosea njia kisha alijicheka akiwa anaendelea kupata pombe taratibu, kisha baadaye alikodi Pikipiki ikamrejesha nyumbani kwao.

Mama yake alishangaaa sana kumuona Lucia akiwa amelewa kiasi kile, alikuwa amelewa kupita maelezo hata dereva wa pikipiki alimpa tahadhari Mama Lucia kuwa Binti huyo alikuwa amekunywa sana hivyo awe naye makini wakati anampeleka ndani.
 
“Lucia kwanini umekunywa hivi Mwanangu jamani” alisema Mama Lucia akiwa anamuingiza Lucia ndani, alimpeleka hadi chumbani Kwake, alimuweka kitandani

“Lucia umepatwa na nini leo? Sijapata kukuona ukiwa umekunywa kiasi hiki” Alisema Mama yake Lucia huku Lucia akiangua kicheko kisha alisema kwa ulevi

“Ukiwa mzima kila Mtu atakupenda lakini kosa lako uumwe au ufe, kila Mtu atakuwa adui wa Maisha yako Mama” Alisema Lucia kisha alibeuwa kidogo, Mama yake alitamani kufahamu ni kwanini Lucia alisema hivyo

“Kwanini unasema hivyo?” Alihoji Mama Lucia

“Mama sisi Binadamu ni wabaya sana, tunacheka mbele kisha nyuma tunanuna ha!ha!ha!” Alisema kisha alicheka lakini Mama Lucia alihisi Mtoto wake pengine amekutana na jambo zito sana, ni kweli Lucia alikutana na janbo zito mno

“Pumzika Lucia tutaongea kesho” Alisema Mama Lucia kisha alitoka chumbani humo, baada ya Mama kutoka Lucia alichukua simu yake akampigia Noela, alihitaji msaada kutoka kwa Noela

Wakati simu hii inapigwa usiku huo, Noela alikuwa amelala na Desmond, Mara moja Noela alishtuka akaipokea huku akiwa mwingi wa Usingizi

“Hello?” Alisema Noela kwa sauti ya Usingizi, Desmond alikuwa amelala

“Noela nahitaji msaada wako” Alisema Lucia

“Msaada gani huo?” Aliuliza Noela huku akinyanyuka kitandani na kwenda dirishani ili tu asimpigie kelele Desmond

“Nataka msaada wa kisheria kwa mgonjwa wangu…ipo hivi….” Lucia alimuelezea Noela alichotaka kusaidiwa

“Hivi una uhakika na unachokisema? Unaonekana umelewa sana kwanini tusiongee kesho hili jambo?” Aliuliza Noela, Lucia alikubali kuzungumza na Noela kesho yake.

Simu ilikatika, kwa Mshituko Noela alipogeuka alimuona Desmond

“Eeeeh Joshua umeamka?” Alihoji Noela kwa mshtuko maana hakutegemea kama angemkuta akiwa amemsimamia nyuma

“Ulikuwa unaongea na nani?” Aliuliza Desmond

“Aaah ni mteja wangu alikuwa anahitaji msaada wa kisheria, usijali Mpenzi twende tukalale” Alisema Noela, hakujuwa kama msaada alioombwa na Lucia ulimuhusu Mtu aliyekuwa naye Usiku huo, Ndiyo!! Lucia alihitaji msaada wa kisheria kwa Mandy maana alichokiona pale kilimtisha sana.

Asubuhi mapema sana Lucia alienda Hospitalini kama kawaida yake, safari hii alikuwa makini zaidi na Mandy maana alijuwa kuna jambo linachezwa nyuma ya ufahamu wake, alitembea taratibu akizunguka kitanda cha Mandy huku akijiuliza afanye nini kuzuia jambo hilo kutokea au kuwa baya zaidi. Alipata wazo fulani, alimfuata Daktari Mkuu wa Hospitali akamuomba Mandy aongezewe Huduma zaidi ili kuharakisha afya yake irejee kama mwanzo maana ilionekana kuwa na uwezekano wa Mandy kupona japo haikujulikana atapona lini licha ya wasiwasi kuwa hata kama kiamka hatoweza kukumbuka chochote au anaweza kukumbuka lakini akawa hawezi kuzungumza wala kufanya chochote kile.

“Kwanini umekuja kuniomba kuhusu hilo jambo?” Aliuliza daktari Mkuu wa Hospitali

“Ni jukumu langu Kuhakikisha Mandy anakaa sawa haraka kuliko ilivyo dhaniwa, naomba sana” Alizidi kuomba Lucia

“Aah Lucia hilo jambo ni lazima tumshirikishe Mume wake, kama unavyojuwa yeye ndiye msimamizi wa kwanza wa Mandy” Alisema Daktari huyo

“Hakuna haja ya kumuleza Desmond kuhusu hili jambo, naomba asijuwe chochote kile” Alisema Lucia na kumfanya Daktari ashangae, akamuuliza

“Kwanini hutaki ajuwe?” Nani atazilipa hizo gharama za ziada?” Aliuliza

“Kumbuka Mandy ni mfanyabiashara mkubwa sana hivyo akiamka atalipia hizo gharama” Alisema Lucia katika hali ya kuendelea kumuomba daktari akubali.

“Asipoamka?” Aliuliza Daktari

“Jukumu letu namba moja ni kuhakikisha wagonjwa wanapona, ni lazima tufanye juu chini kuhakikisha tunasaidia Maisha yake” Alisema Lucia akiwa anamtazama Daktari huyo ambaye alionekana kuanza kumuelewa kidogo Lucia

“Nakuamini Lucia usiniangushe katika hili, nitafanya kama unavyosema” Alisema Daktari huyo, Lucia aliweka mikono mdomoni kwa furaha kisha akasema

“Asante sana Mkuu! Umenipa thamani kubwa sana” Alisema Lucia kisha alimuaga Daktari akaondoka zake, daktari huyo alikuwa Mzee na ilionesha ndiye mmiliki wa Hospitali hiyo

“Aaah” Alisema Daktari kisha alipiga simu alipopajua yeye akatoa maelekezo ya Mandy kupelekwa hatua ya pili ya matibabu.

•••••••

Baada ya siku kama tatu kupita ilipatikana taarifa kutoka kwa Askari polisi aliyekuwa akifuatilia kifo cha Mama Mandy, polisi huyo alimpigia simu Desmond akamwambia kuwa kuna gari iliyopatikana kwenye Bahari, gari hiyo ilikutwa na maiti ya Mtu. Desmond alichanganikiwa, alikuwa ofisini kwake akamuuliza polisi huyo

“Gari! Maiti! Imefahamika gari ni ya nani na maiti ya Nani?” Alihoji Desmond akiwa amesimama huku macho yakiwa yamemtoka pima, alijuwa tu ni ile gari yake aliyomuulia Sanga, haraka akiwa anasubiria jibu la Polisi huyo alijiuliza kama gari ile ikitambulika kuwa ni yake itakuwaje?

“Bado maiti imechukuliwa lakini kimekutwa kitambulisho cha yule mfanyakazi wako ambaye alikuwa ni mhisiwa namba moja wa Tukio la Mke wako ila mwili ulikuwa umeharibika hivyo imekuwa ngumu kumtambuwa kwa macho. Mwili unafanyiwa vipimo kubaini ni Nani” Alisema Polisi huyo

“Vipi kuhusu gari imejulikana kuwa ni ya Nani?” Aliuliza Desmond kama Mtu mwenye haraka ya kutaka kujuwa, polisi hakutia shaka sababu aliamini Desmond alihitaji kufahamu sababu Mandy ni Mke wake pasipo kujuwa Desmond ndiye aliyesababisha kila jambo na alikuwa akiwapiga changa askari ili wasijuwe chochote kile, hata huyo Sanga aliyekuwa akitafutwa ni yeye ndiye aliyemuuwa Hapo Baharini kwa kutumia gari yake.

“Kazi hiyo inafanywa na kitengo husika ili kubaini gari hiyo ilikuwa ni ya nani, ndani ya dakika kumi zijazo tutajuwa gari ni ya Nani pia tutapata taarifa juu ya mwili ule kama ni Wa Sanga au ni wa Mtu mwingine tu” Alisema Polisi huyo kisha alikata simu baada ya kuhakikisha kuwa alizifikisha taarifa muhimu kwa Desmond akiamini ni Mtu mzuri anayepaswa kujuwa kinachoendelea.

Ofisini kwa Desmond hapakukalika mchana huo kila alichofikiria hakikumpa jibu la moja kwa moja, alijuwa ni lazima gari itajulikana kuwa ni ya kwake na polisi watamuhisi kwa namna moja au nyingine jambo ambalo litasababisha aanze kuchunguzwa kuhusu matukio taliyotokea, alizunguka ofisini hapo huku akifikiria afanye nini.

“Oooshit itakuwaje?” Alijiuliza sana Desmond, aliketi akaamka akaketi tena huku akitazama saa ya ukutani, alihesabu hadi dakika kumi alizoambiwa na yule polisi mpelelezi zilipokatika kisha alishika simu yake huku akisubiria simu hiyo iite, punde simu iliita na mpigaji alikuwa ni yule polisi, muda aliosema kuwa atampa taarifa juu ya ule mwili pamoja na gari uliwadia, taratibu aliipokea kisha aliiweka sikioni akiwa amefumba macho yake

“Desmond! Mwili ni wa Sanga mshukiwa namba moja, kesi inazidi kuwa ngumu na kuhusu gari kuna fumbo zito sana hapa ambalo linahitaji umakini hasa ukizingatia gari ile…” alisema Polisi kisha Desmond alidakia

“Ni ya Nani?” Alihoji kwa hofu kubwa sana, ukimya ulitawala huku Desmond akisubiria neno kutoka kwa Polisi huyo, alisema

“Haijulikani, mfumo hauitambui gari hiyo” Alisema Polisi huyo kitu ambacho kilimshangaza sana Desmond, itakuwaje gari yake isitambulike? Kibaya zaidi alikumbuka kuwa hakutoa chochote kwenye ile gari ikiwemo kadi ya Gari kitu ambacho kingekuwa rahisi sana kufahamika, pia alipokuwa akifanya hivyo alijuwa wazi kina kile kirefu hivyo gari haiwezi kuonekana

“Gari haitambuliki?” Alihoji Desmond akiwa na presha
 
SEHEMU YA TANO

“Ndiyo, ngoja nitakupa taarifa zaidi” Alisema Polisi kisha alikata simu hiyo. Desmond alishusha pumzi zake kisha akajiuliza

“Gari yangu haitambuliki? Polisi walijuwaje kuwa kuna gari eneo lile wakati kina chake ni kirefu sana?…” alijiwazia bila kupata majibu huku kichwa kikizidi kumuuma, aliona hawezi kuendelea kuwepo ofisini badala yake alionelea aelekee nyumbani kwake.

Alichukua koti lake la Suti kisha alitoka, akaenda eneo la maegesho ya Magari ya kampuni hiyo, wakati anaingia kwenye gari aliona kitu kilichomchanganya zaidi, aliiyona ile gari yake ambayo alimuulia Sanga kule Baharini tena ikiwa kavu kabisa, alishuka akaenda kuiangalia kwa ukaribu zaidi! Ndiyo ilikuwa ndiyo gari yake ileile aliyoitosa Baharini

“Gari hii imefikaje hapa?” Alijiuliza Desmond kwa mshituko mkubwa, moja kwa moja akatambua kuwa kuna Mtu anayejuwa kila kitu kuhusu Mauwaji yote yaliyofanyika, Desmond alichoka mwili hadi roho

“Nani ni Mtu wa tatu?” Alijiuliza maana katika matukio yale alikuwepo yeye na Mwanasheria wa Mandy aliyeitwa Joel, sasa huyo Mtu wa Tatu ambaye anafuatilia na kujuwa kila kitu ni Nani? Desmond alijikuta akiwa katika rundo zito la Mawazo katika akili yake, aliegemea gari iliyo pembeni.

Mara alikuja Mwanaume mmoja ambaye alikuwa amevalia miwani ya macho, akamwambia Desmond

“Samahani nahitaji kuondoka na hii gari hapa” Alisema Mwanaume huyo akiionesha ni mmiliki wa gari ambayo Deamond alikuwa ameiegemea, Basi Desmond alimpisha Mwanaume huyo akawa ameondoka zake na hiyo gari, Bado Desmond alijawa na mawazo sana kuhusu huyo Mtu wa tatu

Alimpigia simu Mwanasheria Joel akamwambia waonane mara moja, walikutana ufukweni ambako mara nyingi walikuwa wakikutana, Desmond alimsimulia Joel kilichotokea, sasa huyo Joel alikuwa muoga sana tofauti na Desmond akaanza kumlaumu Desmond

“Kwanini uliniingiza huku Desmond, ona sasa siri hii inaenda kuvuja, tutaishia jela nakwambia” Alilaumu Mwanasheria Joel huku akizunguka zunguka nje ya gari walipokuwa wanesimama

“Acha kubweka kama Mbwa koko, huu siyo muda wa kulaumiana ni lazima tumtafute Mtu wa Tatu ambaye anajuwa kuhusu sisi” alisema Desmond kwa hasira sana

“Unafikiri ni rahisi kumuwinda Mtu anayejuwa kuwa anawindwa? Usikute hata hapa tulipo anatuona” alisema Joel, ni kweli mita kadhaa kutoka walipo kulikuwa na Hoteli iliyojaza wazungu kadhaa, kulikuwa na Mtu mmoja ambaye alikuwa amevalia Mask alikuwa akiwapiga picha Joel na Desmond. Mtu huyo alikuwa ni Mwanaume, hakujulikana alikuwa ni Nani, alipopata picha kadhaa aliondoka zake, huwenda ndiye ambaye alikuwa akifuatilia jambo hilo

“Hebu tuliza akili yake Joel, haya maji tumeshayavulia nguo ni lazima tuyaoge, huyo Mtu hana nia ya kutukamatisha mikononi mwa polisi bali kipo anachokitaka, naamni atakuja kukisema hicho anachotaka ndipo tutakapomjuwa na kummaliza ili hii siri ibakie kwetu tu” Alisema Desmond, maongezi yao yalichukua muda mrefu hapo Ufukweni, hawakufikia makubaliano ya nini wafanye ili kujiweka mbali na mikono ya sheria maana tayari walikuwa na kesi ya Mauwaji.

Desmond alijikuta akiwa kwenye matatizo mazito sana, jioni alirudi nyumbani kwake, alipokelewa na shangwe za Watu waliokuwa wakimsubiria huku wakimuimbia, Naam ilikuwa ni siku yake ya kuzaliwa, alishasahu kutokana na msongo wa mawazo, miongoni mwao alikuwepo mpenzi wake Noela.

“Mpenzi umesahau leo ni siku yako muhimu sana eeeh?” Alisema Noela akiwa anatabasamu mbele ya Desmond, aliangaza huku na kule akaona ni bora ajifanye hakumbuki

“Oooh nilisahau kabisa jamani, asanteni sana sana hakika nyie ni Watu wangu wa nguvu sana” Alisema Desmond huku akiachia tabasamu lililobeba mengi mazito, walikata keki, walikula na kunywa, baadaye wengine waliondoka akabakia Noela na Desmond.

Walikunywa pombe kwa pamoja, Noela alionekana kunywa zaidi, sasa huyu Noela alikuwa na tatizo moja, akinywa pombe anaropoka siri nyingi anazozijuwa, Desmond alikuwa akilifahamu hilo ila hakuwa na shaka na Noela, waliendelea kugida unywaji wakiwa kwenye jumba hilo la hadhi ya juu sana ambalo Desmond alilinunua ili kumfanya Noela awe anaenda hapo na siyo kule ambako alikuwa akiishi na Mke wake Mandy hivyo ilikuwa rahisi kwa Noela kutokufahamu kama Desmond ana Mke.

Usiku ulikuwa mwingi sana, Desmond alishangaa ni kwanini Noela haropoki chochote wakati siyo kawaida ya mpenzi wake huyo, alikunywa sana kisha alijikuta akipitiwa na Usingizi akiwa amelala hapo kwenye kiti. Desmond hakulewa, alinyanyuka ili amsaidie Noela kumuingiza ndani.

Wakati anajaribu kutaka kumbeba alimsikia akisema

“Lucia tutalifanya hilo baada ya tukio la kuveshwa pete, sitaki kuchanganya mambo kwa sasa…..Lucia hiyo ni kesi nzito inahitaji utulivu sana” Alisema Kisha alikoroma, sasa kutajwa kwa Lucia kulimfanya Desmond afikirie jambo fulani.

“Lucia ana kesi gani aliyompa Noela? Au amemwambia kuhusu Mandy?” Alijiuliza Desmond kisha alikumbuka tukio la yeye na Mwanasheria Joel kwenda wodini kwa Mandy na kumsainisha mafaili kwa alama za kidole, akafikiria sana mwisho akasema

“Huwenda Mtu wa tatu akawa Lucia, inawezekana ananifuatilia” Alisema Desmond, kisha alimbeba Noela akampeleka chumbani. Aliwasha kompyuta yake akaanza kufuatilia taarifa za Lucia, akajuwa hadi mtaa anaoishi.

Siku iliyofuata, Desmond alianza kumfuatilia sana Lucia kuanzia alipotoka nyumbani kwake asubuhi. Lucia alionekana kuwa mwenye jambo fulani kichwani pake, alimfuatilia kwa karibu ili ajuwe ana fahamu nini kuhusu Yeye, siku hiyo Lucia hakwenda kule Hospitali sababu alikuwa na uhakika na usalama wa Mandy sababu aliwekwa kwenye chumba chenye uangalizi wa daraja la pili, chumba ambacho hata yeye kwa daraja lake la elimu hakupaswa kwenda huko kufanya kazi.

Desmond alijuliza ni kwanini Lucia haendi Hospitalini siku hiyo badala yake alipanda taxi akaelekea Mjini, safari ya Lucia iliishia kwenye moja ya Hoteli maarufu sana mjini hapo, yote haya Desmond alikuwa akiyashuhudia kwa kutumia jicho lake la udadisi, Lucia aliketi kwenye kiti mithiri ya Mtu ambaye alikuwa Hotelini hapo kumsubiria Mtu.

Lucia aliketi hapo kwa kutambo kidogo baadaye Noela aliingia Hotelini hapo, akaangaza huku na kule ndipo alipomuona Lucia, ilionesha walikuwa na miadi ya kukutana hapo, Desmond alizidi kujawa na mshangao huku akifikiria watakuwa wanazungumza kuhusu nini, alikuwa amejificha nje ya Hoteli hiyo ila sehemu ambayo alikuwa na uwezo wa kuwaona Lucia na Noela.

“Lucia hilo jambo ni zito sana ndiyo maana nimekwambia subiria nivishwe pete kwasasa akili yangu inawaza pete tu, sitoweza kuifanya hiyo kazi ngumu” Alisema Noela

“Najuwa Noela lakini hapa nazungumzia uhai wa Mtu, nakuomba uchunguze kuhusu hili jambo ili ifahamike kuna jambo gani lililo jificha” Alisema Lucia kisha akasisitza

“Tafadhali chukua hii Bahasha ina kila kitu, kuna picha za huyo Mwanaume anaitwa Desmond, na baadhi ya taarifa nilizoziandika humo, tafadhali sana Noela” Alisema Lucia

“Ooooh Lucia haya nipe lakini hii kazi nitaifanya baada ya kuvishwa pete” Alisema Noela bila kujuwa kuwa ndani ya bahasha hiyo kulikuwa na picha ya Mwanaume wake ambaye yeye alikuwa akimjuwa kama Joshua wakati jina halisi ni Desmond na Mwanaume huyo alikuwa Muuwaji

Lucia alimpatia Noela bahasha hiyo yenye taarifa muhimu za kesi, Desmond aliona makabidhiano hayo ya Bahasha kisha wawili hao waliagana kila mmoja akashika barabara yake. Desmond aliona ni bora amfuatilie Mpenzi wake Noela ili kujuwa Bahasha hiyo ilikuwa na nini. Basi, baada ya kutoka hapo Noela alielekea moja kwa moja nyumbani kwao, alipoingia ndani aliiweka Bahasha hiyo kwenye Shefu maalum ya kuhifahdhia nyaraka zake, alifunga kwa namba maalum kisha alijipumzisha kitandani.

Akiwa hapo nje Desmond alipokea simu ya Polisi mpelelezi akaambiwa anahitajika haraka kituoni, mara moja aliwasha gari bila kumwambia Noela kuwa alikuwa nje ya nyumba yao, akaelekea kituoni. Huko alioneshwa gari ambayo maiti ilikutwa, gari hiyo ilikuwa ni Landlover ya zamani ambayo ilidaiwa kuwa usajili wake haukujulikana.
 
SEHEMU YA SITA

“Hii ndiyo gari yenyewe ambayo ilikutwa ndani ya Bahari ikiwa na mwili wa Sanga, hadi kufikia sasa tumempoteza mshukiwa namba moja ambaye angetusaidia kujuwa mambo mengi yaliyojificha kuhusu kesi ya Mkeo” Alisema Polisi huyo wakiwa wamesimama kando ya gari hilo, Desmond alilitazama sana gari hilo alafu akakumbuka siku ya tukio kuwa gari aliyoitumia ilikuwa ni Audi A4 na siyo Landlover hiyo chakavu.

Bado aliendelea kujiuliza Mtu wa tatu ni nani?

“Kwa maana hiyo uchunguzi wa kesi utaanza upya ili kumpata mshukiwa mwingine wa matukio haya, inaonesha Sanga alifungiwa ndani ya gari kisha akatupwa Baharini ili afe, yupo Muuwaji nyuma ya hili” Alisema tena Polisi huyo huku Desmond akijiambia

“Muuwaji ni Mimi lakini hamtokuja mnijuwe” alisema ndani ya nafsi yake, basi baada ya kumaliza kufanya mazungumzo hapo Kituoni aliondoka zake, alimfikiria sana huyo Mtu wa tatu kisha akili yake ikawa inamwambia kuwa Mtu wa tatu ni Lucia

Akapata wazo la kutaka kujuwa Noela alipokea bahasha ya nini, alimpigia Noela akamuuliza yuko wapi, Noela alimwambia kuwa yupo Mjini anaangalia gauni la kuvaa siku ya kuvishwa pete, basi Desmond aliutumia mwanya huo kwenda nyumbani anakoishia Noela na Mama yake.

Alisalimiana kwa Bashasha na Mama Noela, Mama huyo alikuwa akimpenda sana Desmond amuowe Mwanaye hivyo kumuona hapo ilikuwa ni jambo la furaha sana, Mama Noela aliingia jikoni kumpikia Mkwe wake mtarajiwa, Desmond aliitumia nafasi hiyo kuingia chumbani kwa Noela ili aitafute ile Bahasha maana alijuwa tu inaweza kuwa na taarifa mbaya dhidi yake

Alipekua kila mahali hadi alichoka lakini hakufanikiwa kuiyona ile bahasha, aliamini Bahasha ilikuwa mlemle ndani, alizidi kuitafuta bila mafanikio, alitumia muda mrefu kufikiria na kuitafuta Bahasha bila kuipata maana aliiweka kwenye shefu ambayo aliificha mahali, jasho lilimtoka Desmond huku akizidi kutafakari itakuwa ipo sehemu gani.

Baadaye alisikia mlio wa gari ya Noela, alipochungulia dirisha alimuona Noela akishuka kwenye gari, haraka alijuwa akikutwa hapo ndani bila taarifa atashtukiwa, aliangalia kama kuna kitu ambacho hakikukaa sawa, haraka alikirudisha kisha alitoka chumbani, alifuta jasho akaketi sebleni, uzuri ni kuwa Mama yake Noela muda wote alikuwa jikoni hivyo hakufanikiwa kujuwa kama Desmond aliingia Chumbani kwa Noela.

Alipoingia Sebleni alishangaa kumuona Desmond ambaye alikuwa akimfahamu kama Joshua

“Eeeh Baby umekuja saa ngapi?” Aliuliza Noela akiwa mwenye furaha na mshangao juu tena akiwa anaweka chini mizigo aliyokuja nayo, kisha alimrudia Desmond

“Nimekuja muda mrefu sana, nimekaa hapa kwa muda mrefu kukusubiria uje” Alijibu Desmond kama siyo yeye vile aliyekuwa akipekuwa chumbani kwa Noela kuitafuta ile Bahasha.

“Ndiyo amekuja muda mrefu nikawa naandaa Chakula” Ilisikika sauti ya Mama yake Noela ( Mlami ) kisha naye alisogea karibu

“Chakula tayari Baba” Mama Noela alimwambia Desmond

“Ah Mama asante sana” Alisema Desmond kisha alienda kupata chakula wakati huo Noela akiwa amepumzika kwenye sofa akionekana kuchoka, wakiwa mbali mbali Desmond alimtupia Noela swali

“Unaoneakana umechoka sana vipi ulifanikiwa?” Aliuliza kwasababu Noela alienda kuangalia gauni la kuvaa siku ya kuvishwa pete

“Ndiyo nimefanikiwa lipo kwenye mfuko” Alijibu noela, Desmond aliendelea kula hadi alipomaliza akaaga akaondoka zake bila kufanikiwa kuipata ile baasha ambayo ilikuwa ikimpa wasiwasi, baadaye Noela aliingia chumbani lakini aliona kama kuna baadhi ya vitu vyake vimekaa tofauti siyo kama alivyoviacha, alipata shahuku ya kuzidi kukagua aliona ishara ile ile akahisi moja kwa moja chumba chake kilipekuliwa, alirudi sebleni kwa Mama yake akamuuliza

“Mama Nani amepekua chumbani kwangu?” Alihoji Noela akiwa mwenye kushangaa

“Kupekua? Mmh mbona hakuna aliyeingia huko…” alijibu Mama Noela sababu hakunuona Desmond akiwa ameingia huko

“Ina maana kumejipekua kwenyewe eti Mama? Vitu nilivyoacha siyo nilivyokuta ndiyo maana nimekuuliza, Mlami utasemaje hujui wakati upo nyumbani muda wote?”

“Aaah au Joshua aliingia huko? Lakini hapana mbona aliketi hapa muda wote”

“aaah” Aligugumia Noela kisha alirudi chumbani, alichukua simu akampigia Desmond akamuuliza kama aliingia chumbani kwake, Desmond alimkatalia kuwa hakuingia huko, basi simu ilikatika huku ikimuacha na maswali mengi Noela kuwa ni Nani aliingia huko na alienda kufanya nini.

Ndani ya Hospitali kubwa, Desmond alienda kumuangalia Mke wake ambaye ni adui mkubwa kwake, kilichomshangaza ni kuzuiliwa kuingia kwenye chumba ambacho Mke wake Mandy alikuwa amewekwa kwa ajili ya matibabu, yalikuwa ni maombi ya Nesi Lucia kwa daktari mkuu wa Hospitali.

Alilalamika Desmond

“Nazuiliwa vipi kumuona Mke wangu wa ndoa? Kwanini anapelekwa kwenye wodi nyingine bila kunitaarifu Mimi?” Alihoji akiwa mbele ya nesi mmoja, Nesi Lucia alikuwa amejibanza mahali akimfuatilia Desmond, alikuwa na mashaka sana na Desmond tokea ile siku ambayo Desmond alienda na Mwanasheria pale Hospitalini na kumsainisha Mandy kwa alama ya kidole.

Desmond alichanganikiwa kwa jambo moja, kama Mke wake ataamka atasema Nani alimuuwa Mama yake Kitu ambacho Desmond alipambana kuhakikisha hakuna siri inayotoka.

“Ni maagizo kutoka kwa Dokta Mkuu wa Hospitali nasi tunayafuata” Alisema Nesi huyo wa kiume, Desmond hakutaka kusema tena baada ya kusikia kuwa maagizo ya kuzuiliwa yaliyoka kwa Dakatri Mkuu wa Hospitali hiyo. Alitembea kisha aliketi kwenye Kiti akakumbuka jambo

Alikumbuka siku moja mvua kubwa ilikuwa ikinyesha, mvua hiyo iliambatana na radi za hapa na pale, alikuwa akiendesha gari huku akionekana kuwa mwenye kutafakari jambo zito kichwani, nyuma yake kulikuwa na gari nyeusi iliyokuwa ikimfuata taratibu, Desmond hakuiyona.

Gari hiyo nyeusi iliyo nyuma yake ndani kulikuwa na Mama Mtu mzima, Mama huyo alikuwa ni Mama yake Mandy, Mama Mandy alipata taarifa kuwa Desmond amepanga kukutana na Mwanasheria wa Mandy kisha wabadilishe hati za mali za Mandy.

Mama Mandy alizidi kumfuatilia Desmond Usiku huo ambao uliambatana na mvua na upepo, safari hiyo ilikita nje ya Mji huo waliokuwa wakiishi tena katika ghofu moja ambalo Mwanasheria wa Mandy aliyeitwa Joel alikuwa akimsubiria Desmond.

Mama Mandy alionekana kuwa makini sana kumfuatilia Desmond, alikuwa peke yake, hakujuwa kuwa Desmond alikuwa ameshashtuka kuwa kuna gari iliyokuwa ikimfuatilia kwa nyuma, Mama Mandy alipoona gari ya Desmond imesimama naye alisimamisha gari kwa mbali kidogo kisha alishuka akawa anatembea kwenye mvua taratibu huku akiwa makini mno, alisogea taratibu sana hadi kwenye gari ya Desmond lakini hakumuona Desmond, Usiku huo ulijaa giza kiasi.

Alipoangalia vizuri mbele aliona ghofu, alipata wazo kuwa huenda Desmond atakuwa ameingia humo, basi alisogea hadi ndani ya Ghofu hilo ambalo lilionekana kuwa kimya sana, hakukuwa na Mtu yeyote yule kitu ambacho kilizidi kumshangaza.

Akachukua simu yake ili ampigie Mandy amueleze mahali alipo pia amwambie Binti yake juu ya Mchezo mchafu aliokuwa akiufanya Desmond, kabla hata hajapiga simu alisikia hatua nyuma yake alipogeuka alimuona Desmond akiwa amesimama nyuma yake, alipoangalia mikono ya Desmond haraka aliona amevalia Gloves.

“Desmond! Unataka kufanya nini?” Aliuliza Mama yake Mandy akiwa anavujwa na maji kwenye mwili kutokana na ile mvua iliyompiga kule nje

“Uchafu unaoufanya umefika mwisho Joshua, kila siku nilikuwa nikimwambia Mandy kuwa wewe huna mapenzi naye bali unahitaji mali za Mtoto wangu, Mwanasheria Joel yupo wapi?” Aliuliza Mama Mandy, Desmond alihema kidogo kisha Joel alijitokeza

“Hadi wewe Joel? Unajuwa ni kiasi gani familia inakuamini Joel? Unashiriki uchafu mkubwa kama Huu, hili siwezi kulifumbia macho, nyote mnaingia kwenye mikono ya sheria” Alisema Mama Mandy kisha alionekana kutaka kupiga Simu lakini haraka Desmond alimuwahi, akampora simu akaona alikuwa anataka kumpigia Mandy

“Unataka kufanya nini Mama? Unataka nifungwe? Unataka niwe Masikini au unataka Mtoto wako aniache? Hii ni siri ambayo hukupaswa kuifuatilia Mama…..” Alisema Desmond huku akijikaza lakini alikuwa akiumia sana ndani ya Moyo wake

“Mandy ni lazima atajuwa kuwa wewe si Mtu mzuri na nina ushahidi wa video na picha ambazo nimetumiwa, umekuwa ukikutana na Joel kila siku Jioni na kupanga mipango yenu michafu..” Alisema Mama yake Mandy

“Pole Mama kwasababu hutoweza kufanya hivyo” alisema Desmond haraka alikata waya uliokuwa ukining’inia kisha akamnyonga Mama yake Mandy hadi alipofanikiwa kummaliza, Mwanasheria Joel alikunja uso wake kuashiria kuwa jambo hilo halikuwa la kawaida.

“Joel Mimi na wewe tumeuwa hapa sawa? Tunapaswa kuondoka na kukaa kimya, nipe hizo nyaraka” Alisema Desmond, haraka alipewa nyaraka kisha Joel alisema

“Bado saini ya Mtu mmoja tu, Mkeo Mandy”

“Nitajuwa nini cha kufanya” Alisema Desmond kisha haraka walianza kutoka lakini Desmond aligeuka kuutazama mwili wa Mama Mandy, alikuwa amevalia cheni ya Dhahabu yenye thamani kubwa sana, alirudi akamvua kisha akaiweka kwenye koti la suti yake, alafu alisema

“Sisi ni Watoto wa kimasikini sana”

Kumbukumbu ya Desmond iliishia hapo, alitikisa kichwa chake kisha alielekea ofisini kwa Daktari wa Hospitali, Daktari alipomuona Desmond alijuwa nini kimemleta, Desmond alianza kumshambulia Daktari huyo kwa maneno

“Umeagiza Mke wangu apelekwe Wodi nyingine alafu Mimi nizuiliwe kumuona si ndiyo? Hivi unajuwa ulichokifanya?” Alisema Desmond kwa hasira

“Desmond hebu kaa kwanza tuongee, hili jambo siyo la kulichukulia jazba, tulichofanya ni kupandisha daraja matibabu ya Mkeo ili aweze kuamka haraka ” Alisema Daktari huyo kwa upole sana
 
SEHEMU YA SABA

“Kuamka haraka? Unajipa kazi ya Mungu si ndiyo? Unafikiri Mimi sitaki Mke wangu aamke haraka? Nataka ila mlipaswa kunishirikisha na sio sahihi kunizuia mimi kumuona Mke wangu…Nitamuhamisha kwenye Hospitali hii haraka sana” Alisema Desmond

“Desmond naomba unielewe, Mkeo utamuona lakini siyo kama zamani kutokana na aina ya matibabu ya sasa pia wodi aliyopelekwa, nakuomba uwe mpole. Muhimu Ni afya ya Mkeo Desmond” Alisema Daktari lakini Desmond alizidi kuwa juu

“Natoa siku mbili Mke wangu awe amerudishwa kwenye wodi yake aliyokuwa akikaa, vinginevyo nitamuhamisha hapa” Alisistiza Desmond kisha aliondoka zake, lakini Daktari aliwaza sana ikiwa Desmond anampenda mke wake kwanini akatae asipatiwe matibabu kwenye wodi mpya? Kama gharama mbona wao ni Mabilionea wakubwa tu

Alipata wazo la kumtafuta Lucia ambaye alitoa wazo la Mke wa Desmond kuhamishwa Wodi na kupewa huduma za daraja la juuu zaidi, alimpigia simu akamwambia wakutane nyuma ya Hospitali hiyo mahali ambapo palikuwa na Bustani.

Mara moja walikutana huko, Daktari akataka kujuwa nini ambacho kilikuwa kikiendelea na kwanini Lucia alitoa wazo lile, ilionekana kuwa ni swali gumu sana kwa Lucia kumjibu Daktari huyo akamwambia

“Ni kwasababu ni Mgonjwa wangu ndiyo maana nilitaka apewe matibabu ya haraka ili kumuamsha mapema” Alijibu akiwa anatazama chini lakini akili ya uzee ya Dakatari Mkuu ilimwambia kuwa Lucia alikuwa na jambo lingine kabisa

“Unajuwa fika kuwa unaniongopea Lucia…Niambie ukweli, Lucia wewe ni kama Binti yangu wa kumzaa tena hata Mjukuu wangu, sura yako inaonesha dhahiri kuwa unnificha jambo…nyuma ya pazia kuna nini?” Aliuliza tena Daktari huyo, alimpa nafasi Lucia afikirie nini cha kufanya, mwishowe aliona ni bora amfungukie daktari huyo, alimwambia

“Nina mashaka Desmond akawa siyo Mtu mzuri kwa Mke wake Mandy, juzi alikuja na mwasheria akamsainisha Mgonjwa kwa alama za vidole, nilipouliza nilijibiwa kuwa sipaswi kuingilia masuala ya kifamilia” Alieleza Luicia

“Una uhakika?”

“Nina uhakika na ndiyo sababu ya kukuonba Mkuu mgonjwa ahamishwe daraja”

“Lakini inafikirisha sana sijui kuna nini nyuma yake. Ndiyo maana nilikuja kukuuliza sababu Desmond aliwaka sana baada ya kujuwa kuwa hawezi kumuona Mke wake. Hapo ndipo wasiwasi wangu ulipoanza….Kaendelee na kazi Luicia tutaongea baadaye” Alisema Mkuu huyo kisha alimtazama Lucia akitokomea eneo hilo akiwa ndani ya mavazi ya kihudumu

Baada ya kupita masaa kadhaa, Desmond alimuarika Mwanasheri Joel kwenye moja ya Baa zenye hadhi, alihitaji kumueleza kuhusiana na jinsi mambo yalivyokuwa

“Kesi hii tukienda kichwa kichwa tunaweza jikuta tunafia jela…” alisema Desmond akiwa anagida unywaji, joel akauliza

“Kuna jambo jipya?”

“Kuhusu gari yangu niliyomuulia Sanga kutokukutwa Eneo la tukio badala yake kukutwa gari nyingine kabisa ikiwa na mwili wa Sanga, tafsiri yake kuna Mtu wa tatu ambaye anaijuwa hii inshu, pili ni kuhamishwa kwa Mke wangu na kupelekwa kwenye wodi nyingine bila Mimi kupewa taarifa kisha nikazuiliwa kwenda kumuona, ni ishara kuwa kuna bomu linaenda kulipuka” Alisema Desmond akiwa anamtazama Mwanasheria Joel

“Uuuupss!! Hata mimi taarifa ya gari imenivuruga sana, huyo Mtu wa tatu ni nani hasa? Na kwanini hadi leo hajapiga simu wala kutoa taarifa polisi?” Aliuliza Joel

“Nashindwa kuelewa, kila ninapoliwaza jambo hili naishia kukosa majibu ya kueleweka japo namtilia sana mashaka nesi anayemuuguza Mke wangu, kuna bahasha amempa Mpenzi wangu sijui kuna nini ndani yake napata ukichaa” Alisema Desmond

“Desmond hii ni vita kubwa sana na mwisho wake hautokuwa mzuri kama tunavyofikiria ni lazima tuwekeze nguvu na pesa ili tumalize mizizi yote” Alisema Joel

“Kesho kutwa ni siku ya kumvisha pete Noela, kama yule nesi atakuja kwenye shughuli basi kila kitu kitaharibika, ni lazima tumzuie asije” Alisema Desmond

“Hiyo kazi niachie Mimi nitahakikisha hafiki kwenye shughuli lakini wewe unatakiwa kuhakikisha unamtafuta Mtu wa tatu aliyeona ukiwa unamuuwa Sanga Baharini, huyo ni Mtu hatari sana na huwenda anajuwa kuhusu kifo cha Mama Mandy kuwa mimi na wewe ndiyo wauwaji” Alisema Joel kisha alinyanyuka, akachukua mkoba wake akapiga funda moja ya kinywaji akaiweka glasi kwa nguvu juu ya meza kisha akaondoka zake pale.

Jioni Lucia alimpigia simu Noela wakati huo akiwa anarejea nyumbani kwake akamuuliza kuhusu ile bahasha kama ameanza kuifanyia kazi lakini Noela alizidi kumsistizia kuwa ni lazima shughuli ya kuveshana pete ipite kwanza ndipo aifanyie kazi, basi Lucia alikata simu akaelekea nyumbani kwao, akiwa anaingia ndani aliiyona gari nyeusi ikiwa imesimama nje ya nyumba yao, aliitazama lakini hakutia shaka kabisa, ndani ya gari hiyo alikuwemo Mwanasheria Joel na kilichomleta pale kilikuwa ni kuanza kazi ya kuhakikisha Lucia aendi kwenye hiyo shughuli, baada ya kufahamu anapoishi Lucia, Mwanasheria Joel aliondoka zake.

Alimkuta Mama yake akiwa amelala, alikuwa mgonjwa hivyo jukumu kubwa la Lucia lilikuwa ji kuhakikisha kuwa Mama yake anakuwa salama, Maisha yao yalikuwa duni na yeye ndiye tegemezi, alipitia huko chumbani na kumkuta Mama yake akiwa amelala, alimfunika shuka kisha alitoka akaenda kuketi sebleni.

Alitafakari mambo mengi sana ikiwemo alichozungumza na Daktari Mkuu kisha alikumbuka alichokiweka kwenye bahasha aliyompa Noela, aliweka picha ya Desmond na Mwanasheria Joel kisha aliambatanisha na maelezo ya alichotaka Noela akifanye, alivuta pumzi zake kisha alijilaza kidogo pale pale Sebleni.

Usiku ulipoingia, nyumbani kwa akina Noela na Mama yake kulikuwa na shamra shamra sababu tukio la kuvishana pete lilikuwa limekaribia, baadhi ya ndugu walikuwa wamefika pale, sura ya Noela ilizidi kunawiri kwa tabasamu bila kujuwa kuwa kulikuwa na vita kubwa iliyokuwa inapiganwa chini kwa chini, Upande wa kule Hospitali matibabu yaliendelea kwa Mandy, kukawa na tumaini kidogo lakini Desmond hakuambiwa chochote kile sababu Tayari daktari Mkuu na Nesi Lucia walikuwa na ajenda ya siri kuhusu uhai wa Mke wa Desmond aliyeitwa Mandy.

Siku iliyofuata baada ya muda wa kazi kuisha, Lucia alimuomba Noela waonane mara moja, walionana mgahawani majira ya Mchana, ombi la Lucia likawa lile lile lakini Noela alimsistizia kuwa hadi Shughuli ipite.

“Lucia ni kesho kutwa tu navishwa pete, kama nilivyokwambia sitawekeza fokasi kubwa kwenye kazi yako sababu nina shughuli iache ipite kisha nitarudi kazidi na nitaanza na kazi yako” Alisema Noela

“Sawa Noela lakini ni muhimu sana ukafungua ile Bahasha” Alisitiza sana Lucia

“Sawa nitafanya hivyo kwa ajili yako, nitahakikisha unafaulu katika hilo jambo unalonipa kulifanya” Alisema Noela

“Umesema ni kesho kutwa ndiyo unavishwa pete, nitajitahidi ili nimuone shemeji yangu….kama sikosei ulisema anaitwa Joshua”

“Una kumbukumbu kama zamani, ndiyo anaitwa Joshua. Uje Lucia, ni muhimu sana” Alisema Noela, waliachana baada ya kuwa wamezungumza vya kutosha. Aliporudi nyumbani Noela aliketi akajiuliza ni kwanini Lucia anasistiza sana afungue hiyo Bahasha.

Basi alielekea kwenye kisanduku chake cha kuhifahdia nyaraka mbalimbali za kazi, ndimo alimohifadhi ile Bahasha inayotafutwa na Desmond, aliitoa kisha aliishikilia akiwa ameketi chini kando ya sanduku hilo

“Mmh kuna nini humu mbona Lucia anasistiza sana nifungue?” Alijisemea Noela ndani ya moyo wake, mwisho aliona ni bora aifungue ili kuondoa ile lawama aliyokuwa akipewa na Lucia kuwa anapuuzia kazi yake

Alichana kwa juu kisha karatasi zikawa zinaonekana kwa juu, akavuta karatasi moja lakini wakati anaivuta akaidondosha picha ya Desmond Mwanaume ambaye anamjuwa kama Joshua na ndiye Mtu anayetakiwa amfwatilie na kujuwa ukweli wa mambo yaliyojificha na ndiye Mwanaume anayeenda kuvishana naye pete, bahati nzuri picha iliangukia kwa kujifunika, nyuma hakukuwa na maandishi yoyote yale.

Aliiokota picha hiyo ikiwa imejifunika vile vile, moyo ulianza kumdunda hata kabla hajaona picha hiyo, alijishangaa sana lakini kabla hajaigeuza Mama yake aliingia chumbani akamuona Binti yake akiwa katika hali ile ya waiswasi.

Alimpokonya ile bahasha na picha kisha akavirudisha kwenye ile Bahasha bila hata kuiangalia picha hiyo ya Desmond, akaweka Bahasha kwenye sanduku hilo alilokuwa ameliacha wazi kisha alilifunga.

“Noela huu siyo wakati wa wewe kufanya kazi, mara nyingi kazi zako zinakuumiza kichwa na kukufanya ukose raha. Huna haja ya kuwa katika hali hiyo cha Msingi ni kuweka akili kwenye tukio la kesho kutwa la kuvishwa pete na Mwanaume unayempenda”

Alisema Mama Noela kisha alimnyanyua Mtoto wake

“Unaenda kuwa Mke wa Joshua, ni jambo ulilolipigania kwa muda mrefu hebu lipe kipaumbele, kazi zako utaendelea nazo baada ya shughuli kupita sawa?”

“Sawa Mama” alijibu Noela kisha alitoa tabasamu, laiti kama angelikuwa ameiyona ile picha basi mambo yote yangelikuwa yameharibika maana angesoma kilichoandikwa na Lucia, angekuta siri ya jina la Desmond kisha tuhuma nzito.

“Haya twende” Alisema Mama Noela kisha alitoka na Binti yake lakini akili ya Noela ilijikuta ikianza kuwaza ile Bahasha ya Lucia.

Naaam!! Desmond hakupotea Hospitalini sababu alijuwa fika kuwa kwa huduma anazopewa Mke wake anaweza akaamka muda wowote hivyo alihitaji kummaliza japo alizuiliwa kumuona, alimtafuta Nesi Lucia akamwambia anahitaji kumuona Mke wake.

“Lucia mnanitendea vibaya sana kwa kutoniruhusu nimuone Mke wangu, wewe unajuwa ni jinsi gani nampenda Mke wangu na nimekuwa hapa kila siku kuhakikisha afya ya Mke wangu inakaa sawa” Alisema Desmond wakiwa wamesimama, hakujuwa kama Lucia tayari alimuhisi vibaya

“Sasa kipi bora Desmond, umuone Mke wako kila siku akiwa katika hali ileile au usimuone ili afya yake ikae sawa ndani ya muda mfupi? kumbuka Mkeo amekuwa hapa kwa zaidi ya miezi mitano, hadhi ya maisha yenu hakupaswa kuwa kwenye ile wodi wewe hukulioma hilo?” Alisema Lucia huku kila mmoja wao akipigana vita ndani kwa ndani, Desmond alipokuwa akimtazama Lucia alikuwa akijiambia kuwa lucia ndiye Mtu wa tatu anayejuwa kila kitu huku Lucia akijisemea ndani ya moyo wake kuwa ukweli utajulikana Desmond

“Hilo ni sawa lakini kwanini maamuzi haya yamekuja ghafla tu tena bila kunishirikisha Mimi? Hamjui ni kiasi gani nimeumia mimi Lucia, nampenda Mke wangu Mandy” alisema Desmond akiwa anatokwa na mchozi

“Huna sababu ya kulia Desmond, ungekuwa unampenda Mke wako usingemsainisha hati ya Makabidhiano ya Mali ukiwa na Mwanasheria” Alisema Lucia, Desmond akashtuka sasa kuwa Lucia ndiye aliyetoa hilo wazo la kuhamishwa kwa Mke wake baada ya ile siku kumsainisha Mandy mbele yake

“Anhaaa kwahiyo wewe ndiye uliyetoa wazo la Mke wangu kuhamishwa?” aliuliza Desmond akiwa anafuta chozi kisha aliweka tabasamu la kikatili, ile hali ya majonzi aliiondoa baada ya kugundua kuwa anaongea na Mtu ambaye alikuwa ameushtukia mchezo mzima.

“Lucia hukupaswa kujiingiza huku kabisa kwasababu hujui ilianzaje wala inaenda kuishaje, umefanya kosa kubwa litakalo

kugharimu. Mama yako ni Mgonjwa, ni bora uweke Mawazo yote kwa Mama yako kuliko kuweka kwa Mtu ambaye atakuja kukugharimu” Alisema Desmond kwa sauti iliyokaza yenye kumaanisha, Lucia alicheka chini chini kisha akamwambia Desmond

“Mwanzo nilikuwa nikikupenda sababu niliamini una mapenzi mazito sana kwa Mke wako lakini baadaye nilikuchukia baada ya kugundua kuwa wewe ni miongoni mwa waliosababisha yeye akawa pale, nakuhakikishia Desmond, igizo unalofanya ukweli utajulikana Mkeo akiamka” Alisema Lucia kisha alianza kuondoka lakini Desmond alimshika mkono akamwambia

“Una masaa 24 ya kutoka katika hili Lucia, Uwe na siku njema” Alisema Desmond kisha kila mmoja alielekea alipopakusudia, lakini Maneno aliyoyazungumza Lucia yalimtia ukichaa sana Desmond akiwa kwenye gari aliwasiliana na Joel akamwambia Wamuuwe Lucia kabla ya tukio la kuvishwa pete kwa Noela.

Siku hiyo Lucia alizidi kuchanganikiwa sana, aliporudi nyumbani kwao alichukua simu yake ambayo wakati anaongea na Desmond alimrekodi ili aweze kuongeza ushahidi wa kumpa Noela, alimtumia sauti hiyo ya mazungumzo Noela kisha akampigia simu ili amuelekeze lakini Noela hakupokea simu, maandalizi ya Tukio la kuvishwa pete yalikuwa yamepamba moto sana hivyo hakuwa na muda wa kukaa na simu.

Siku hiyo iliisha, siku iliyofuata ndiyo ilikuwa siku ya kuvishwa pete kwa Noela, maandalizi yote yalifanyika pale pale nyumbani kwao sababu hawakutaka Watu wengi, gharama zote alizifanya Desmond. Usiku wa tukio Lucia alijiandaa, akamuaga Mama yake akamwambia

“Mama naenda kwenye sherehe ya rafiki yangu, sitochelewa kurudi. Nakupenda sana Mama yangu” Alisema

“Nakupenda pia Binti yangu, usijali nenda Mama nitakuwa salama. ” alisema Mama yake Lucia, waliagana hapo kisha Lucia alitoka. Alisimama Nje akimsubiria Mtu wa Pikipiki aliyewasiliana naye kuwa aende kumchukua hapo na kumpeleka nyumbani kwa akina Noela, alisimama kwa muda mrefu nje, alipoona muda unazidi kwenda alianza kutembea taratibu ili kama atakutana na Pikipiki aitumie, Ulikuwa ni usiku wa saa mbili, baadaye likaja gari moja na kusimama mbele yake, Lucia alijiuliza ni nani aliyesimama mbele yake.

Kioo kilishushwa akaonekana Mwanaume mmoja

“Samahani Dada unaenda wapi?” Aliuliza huyo Mwanaume

“Naenda mahali kwani vipi?” aliuliza Lucia maana alikuwa amechukia kwasababu bodaboda wake alikuwa amendanganya kuwa hayupo mbali kumbe yupo mbali

“Sio vema Mtoto wa kike akatembea kwa mguu usiku huu, naelekea barabara ya sita sijui wewe” Alisema Mwanaume huyo, Lucia alifikiria akaona ajishushe tu kwa huyo Mwanaume maana yeye alikuwa akielekea Barabara ya nne.

“Naelekea Barabara ya Nne” Alijibu Lucia

“Basi twende nikusindikize” Alisema Mwanaume huyo, Lucia aliingia kwenye gari, safari ilianza kuelekea nyumbani kwao Noela, wakiwa Barabarani mwanaume huyo alionekana kumtongoza Lucia lakini Lucia hakuonekana kumkubali kisha alimwambia

“Kama umenipa msaada ili unitongoze naomba unishushe Mimi siyo Mwanamke wa hivyo” Alisema Lucia akionekana kuchukizwa..
 
SEHEMU YA NANE

“Aaah usijali samahani kwa hilo, tunapita kushoto ili tuwahi kufika” Alisema Mwanaume huyo kisha alikata kushoto lakini Lucia alimuuliza

“Huko barabara imefungwa kuna ujenzi utapita vipi alafu kuna pori kubwa huko” Alisema Lucia jamaa alizidi kuongeza gia kisha alicheka, ndipo Lucia alipomkumbuka Desmond na kauli yake, basi Lucia akaanza kuhangaika ili ashuke maana alijuwa hapo ni lazima atafanyiwa kitu kibaya, kumbuka Tayari maagizo ya kuuawa kwa Lucia yalikuwa yametolewa na Desmond, katika pirikapirika gari hiyo ikajikuta ikipoteza uelekeo na kugonga Mti.

Hali zao zilikuwa mbaya mno, Lucia alijitahidi kufungua mlango akiwa hoi damu zikiwa zinamtoka, Mwanaume huyo naye alikuwa akitokwa na Damu usoni, naye alifungua mlango akaanza kumfukuza Lucia aliyekimbilia porini eneo ambalo lilikuwa na mlima hivi. Akiwa anazidi kukimbia Lucia alimpigia sana simu Noela lakini simu haikupokelewa, katika kukimbia akajikuta ameindondosha simu yake.

Mwanaume huyo aliiokota simu ya Lucia kisha aliendelea kumfukuza, bahati mbaya Lucia alijikwaa akaanguka chini, mara moja Mwanaume huyo akiwa ana vuja damu alimfikia.

“Wewe ni Nani na unataka nini?” aliuliza Lucia akiwa katika hali ya hofu sana huku akiwa amechoka.

“Unataka kujua mimi ni nani na Nataka nini kwako si ndiyo? Mimi ni muuwaji nimekuja kuchukua roho yako Lucia” Alisema Mwanaume huyo akionekana kumfahamu vizuri sana Lucia

“Uniuwe kwa kosa gani mbona sikufahamu?” aliuliza Lucia akiwa katika hali ya hofu huku maumivu ya Mguu yakizidi kumtafuna.

“Kosa lako ni Moja tu, kujifanya mjuwaji. Umeonywa mara ngapi kuhusu Mandy wewe?” aliuliza Mwanaume huyo na kumfanya Lucia sasa ajuwe kuwa Desmond alishatuma Mtu ili auawe.

“Ina maana umetumwa na Desmond si ndiyo? unafikiri ukiniuwa itakuwa mwisho wa kila kitu? nakuhakikishia kifo changu hakitofanya siri yenu isitoke, tena itatoka kwa kishindo kikubwa sana” Alisema Lucia katika hali ya kujiamini sana baada ya kujuwa kuwa alitakiwa kufa kwa maagizo ya Desmond

Yule Mwanaume alimbana vizuri Lucia pale chini akahakikisha anakosa hewa kwa zaidi ya dakika moja kabla ya kunyonga shingo ya Lucia, baada ya hapo alipiga simu mahali akasema

“Kazi imeisha” Alisema kisha aliubeba mwili wa Lucia akaenda kuuweka kando ya Barabara hiyo ambayo ilikuwa na giza sana kisha akaliwasha gari lake lililobamiza kwenye Mti kisha aliondoka eneo hilo.

Shughuli ilikuwa imepamba moto, Noela hakumuona Lucia akienda hapo licha ya kuarikwa, hakujuwa kuwa Lucia alikuwa ameuawa porini. Desmond alimuuliza Noela alikuwa akifikiria nini baada ya kumuona akiwa kama Mtu mwenye kutafakari jambo

“Rafiki yangu Lucia, alisema anakuja hadi sasa hivi, nampigia simu hapatikani” Alisema Noela

“Atakuja tu, Watu wengine ndio kwanza wanaingia hivyo naye ataingia tu” Alisema Desmond huku akijuwa fika kuwa Lucia alikuwa ameuawa.

Muda ulienda bila Lucia kutokea eneo hilo, shughuli ilifanyika kwa bashasha zote. Desmond akawa mchumba rasmi wa Noela, ilikuwa ni siku yenye furaha sana Kwa Noela na Mama yake sababu jambo hilo lilisubiriwa kwa muda mrefu, basi zikapigwa picha za kutosha, Watu walikula hadi kusaza, Furaha ilitawala usiku huo. Baada ya kuisha tukio hilo, Desmond aliaga ili aondoke lakini alimuona Mtu mmoja aliyemfananisha akiwa ameketi mahali anazungumza na Mwanume mmoja.

Desmond alimtazama sana Mwanaume huyo huku akijiuliza alimuona wapi, akakumbuka alimuona siku ambayo aliliona gari lake likiwa maegesho ofisini wakati gari hilo alilitumbukiza baharini, alikuwa hamfahamu Mtu huyo na wala hakumuarika, ila hakutaka kulipa uzito jambo hilo maana kama hakuarikwa na yeye basi atakuwa amearikwa na Mpenzi wake Noela.

Akaendelea kuaga Watu kwa ajili ya kuondoka eneo hilo, ghafla aliguswa begani na Msichana mmoja ambaye alikuwa akihudumia Watu vinywaji, msichana huyo alimpa Desmond ujumbe wa karatsi, Desmond akamuuliza Msichana huyo

“Ametoa Nani?”

“Mkaka yule…” Msichana huyo alipoonyesha alipokaa Mtu aliyetoa ujumbe huo hakuwepo hapo, akaanza kumtafuta kwa macho lakini hakumuona ila Desmond alimuona mwanzo Mtu aliyekaa hapo, alikuwa ni yule Mwanaume aliyemuona ofisini kwake

“Haya sawa asante” Alisema Desmond, kisha alisogea pembeni akafungua ujumbe huo akakuta maneno yaliyosomeka

“LUCIA AMEKUFA LAKINI SIYO MWISHO, TUKUTANE JUMATATU KATIKA HOTELI YA HAVANA SAA 7 MCHANA!! CHUMBA NAMBA 43, NINA USHAHIDI WA ULIYOYAFANYA”

Desmond alishtuka sana, alimtafuta Mwanaume huyo bila mafanikio, alitoka nje kabisa lakini hakufanikiwa hata kumuona Mtu huyo alijikuta akichoka mwili na akili, Mtu wa tatu bado aliendelea kumtesa lakini bahati nzuri aliifahamu sura yake, alimuita Mwanasheria Joel kisha waliondoka hapo kwa ajili ya kujadili ni jinsi gani watamkabili Mtu huyo.

Noela alilala fofo baada ya kunywa pombe vya kutosha, aliamka siku iliyofuata ambayo ilikuwa ni Jumatatu, akili yake ikamwambia kuwa siku hiyo hawezi kufanya chochote zaidi ya kupumzika tu, lakini baadaye alifikiria kuhusu Lucia, alijaribu tena kupiga simu ya Lucia lakini haikuita kabisa.

Alianza kupata mashaka pengine amepata tatizo ila hakuwa na Mtu wa kumuuliza, aliwasha Tv ili aangalie habari za hapa na pale, ndipo alipokutana na taarifa ya kifo cha nesi Lucia aliyeuawa kwa kunyongwa shingo hadi kufa, Roho ilimripuka sana Noela

Alishtuka sana kusikia taarifa hiyo na kibaya zaidi ni kuwa aliacha Mama ambaye ni mgonjwa sana, mara moja Noela alivalia nguo zake akamuaga Mama yake kisha akaelekea mahali ambapo maiti ya Lucia ilikuwa imehifadhiwa, ni katika ile ile Hospitali ambayo Lucia alikuwa akifanyia kazi, alikutana na Daktari Mkuu wa hiyo Hospitali akawa anazungumza naye.

Mkuu huyo alimuelezea Lucia kwa jinsi alivyoweza mbele ya Noela, kikubwa zaidi Noela alikufa akiwa masikini, pili alikuwa na ndoto za kuja kuwa Nesi bora zaidi katika Hospitali hiyo na tatu aliacha Mgonjwa aliye katika hali mbaya sana.

“Mgonjwa aliye katika hali mbaya?” Alihoji Noela

“Ndiyo! alikuwa akimuhudumia kwa kipindi chote, alikuwa na ndoto ya kumuona Mgonjwa huyo anakuwa mzima tena lakini ndoto ya Lucia imezimika ghafla kama Mshumaa” Alieleza kisha chozi lilimtoka akalifuta, Noela alipelekwa hadi kwenye chumba ambacho Mgonjwa wa Lucia alikuwa amelazwa, hakuwa mwingine bali ni Mandy Mke wa Desmond.

Alimtazama Mandy kisha alisema

“Hakika Lucia amekufa na ndoto zake” Alisema Noela huku akifuta chozi lake, alikumbuka mara ya mwisho alipewa kazi na Lucia, haraka alitoka wodini ili alekee nyumbani kwake kuangalia zile nyaraka alizopewa na Lucia.

Wakati anatoka Desmond alikuwa akiingia Hospitalini hapo, wawili hao hawakuonana. Haraka akiwa na gari yake Noela alifika nyumbani kwao, alimkuta Mama yake akiwa ameketi sebleni, alitaka kumpita ila Mama yake alisema

“Amekuja Mtu uliyemuagiza amechukua sanduku” Alisema Mama Noela na kumfanya Noela ashangae ni Nani alikuja kuchukua Sanduku

“Mama unasemaje, sanduku la chumbani kwangu?”

“Ndiyo kwani hukumtuma Mwanaume mweusi hivi?” aliuliza Mama Noela

“Mamaaaaaaa!!” aligumia Noela kisha alielekea chumbani kwake haraka, kweli Sanduku liliondolewa chumbani hapo

Haraka alirudi Sebleni akamuuliza Mama yake

“Mtu huyo amekuja saa ngapi?”

“muda siyo mrefu sana alikuja na gari akasema umemuagiza na alikuwa akijuwa hadi lilipokaa nikamiami, ina maana hukumtuna Mtu?” aliuliza Mama Noela kwa mshangao, Noela hakujibu alitoka akapanda gari kisha akaanza kumtafuta huyo Mtu, alipita mitaa mbali mbali bila mafanikio yoyote yale hadi alichoka.

Aliamuwa kurudi nyumbani, ndipo alipogundua huwenda kulikuwa na jambo zito lilifanya Lucia auawe, akafikiria atapata vipi kujuwa alichokuwa anatakiwa kufanya.
 
SEHEMU YA TISA

Alitafakari kwa muda mrefu sana kisha akafungua Whatssap yake akakumbuka kuna jumbe alizokuwa ametumiwa na marehemu Lucia ila alikuwa hajazifungua.

Alikutana na Ujumbe wa sauti, alifikiria kusikiliza ujumbe huo ila moyo wake ulijawa na woga akahofia kuijuwa hiyo siri iliyopelekea kifo cha Lucia, basi akajipa moyo akakaza roho yake. Alishtuka sana aliposikia sauti ya Desmond akizungumza na Lucia tena wakionekana kujuwana kabisa. Alisikia maongezi hayo yakisema

“Lucia mnanitendea vibaya sana kwa kutoniruhusu nimuone Mke wangu, wewe unajuwa ni jinsi gani nampenda Mke wangu na ninekuwa hapa kila siku kuhakikisha afya ya Mke wangu inakaa sawa” Alisema Desmond

“Sasa kipi bora Desmond, umuone Mke wako kila siku akiwa katika hali ileile au usimuone ili afya yake ikae sawa ndani ya muda mfupi? kumbuka Mkeo amekuwa hapa kwa zaidi ya miezi mitano, hadhi ya maisha yenu hakupaswa kuwa kwenye ile wodi wewe hukulioma hilo?” Alisema Lucia

“Hilo ni sawa lakini kwanini maamuzi haya yamekuja ghafla tu tena bila kunishirikisha Mimi? Hamjui ni kiasi gani nimeumia mimi Lucia, nampenda Mke wangu Mandy” alisema Desmond kwa sauti ya kilio

“Huna sababu ya kulia Desmond, ungekuwa unampenda Mke wako usingemsainisha hati ya Makabidhiano ya Mali ukiwa na Mwanasheria” Alisema Lucia,

“Anhaaa kwahiyo wewe ndiye uliyetoa wazo la Mke wangu kuhamishwa?” aliuliza Desmond

“Lucia hukupaswa kujiingiza huku kabisa kwasababu hujui ilianzaje wala inaenda kuishaje, umefanya kosa kubwa litakalo kugharimu. Mama yako ni Mgonjwa, ni bora uweke Mawazo yote kwa Mama yako kuliko kuweka kwa Mtu ambaye atakuja kukugharimu” Alisema Desmond kwa sauti iliyokaza yenye kumaanisha, Lucia alicheka chini chini kisha akamwambia Desmond

“Mwanzo nilikuwa nikikupenda sababu niliamini una mapenzi mazito sana kwa Mke wako lakini baadaye nilikuchukia baada ya kugundua kuwa wewe ni miongoni mwa waliosababisha yeye akawa pale, nakuhakikishia Desmond, igizo unalofanya ukweli utajulikana Mkeo akiamka” Alisema Lucia

“Una masaa 24 ya kutoka katika hili Lucia, Uwe na siku njema” Alisema Desmond

Yalikuwa ndiyo maneno yaliyosikika, Lucia alichoka mwili na akili alijikuta akikaa chini kama mzigo

“Joshua wewe ni Desmond? Umemuuwa Lucia? Una Mke Joshua?” Alisema kwa suati ya chini iliyojaa mihemo ya kuchanganikiwa, Ni mwanaume aliyetoka kumvisha pete siku iliyopita tu lakini leo anagundua siri nzito za Mauwaji

Chozi lilimbubujika Noela, aliangalia kidole chake kilicho na pete,

“Joshua…..Desmond…Una Mke ee!!” alisema kwa kuchanganikiwa Noela

“Kwanini sikukusikiliza mapema Lucia, nisingefikia uamuzi huu mbaya zaidi katika Maisha yangu” Alisema Noela, alijikaza sababu ni Mpelelezi na mwanasheria Mkubwa tu Nchini, aliwaza kisomi zaidi nini afanye

Akasikiliza tena huku moyo ukimuuma na chozi likimvuja, kisha akakumbuka alipoenda kuangalia mwili wa Marehemu Lucia alipelekwa pia kwa Mgonjwa wa Lucia, aliunganisha maelezo akapata picha kamili huwenda mgonjwa wa Lucia ndiye Mke wa Desmond…PATAMU HAPO!!

Alifuta chozi lake akaivaa elimu yake ya kipelelezi japo bado moyo ulimuuma sana Noela, alitoka chumbani akakutana na Mama yake, hakutaka Mama yake ajuwe chochote kile ila Mama Noela alihisi Mwanaye alikuwa akilia>>>>>>>>>>>>>>

“Ulikuwa unalia?” alihoji Mama Noela

“Mama kuna rafiki yangu amefariki” Alisema Noela “Mmh! masikini pole sana, unaenda msibani?”

“Ndiyo Mama” Basi waliachana hapo, Noela aliingia kwenye gari kwa ajili ya kuelekea Hospitalini.

Hakutaka kupokea simu za Desmond sababu alijisikia vibaya sana kutokana na alichokisikia hivyo alihitaji zaidi kupata uhakika wa mambo, moja kwa moja alienda hadi kwa Mkuu wa Hospitali hiyo. Alimuuliza kuhusu Mgonjwa wa Lucia

“Mgonjwa hali yake bado haijakaa sawa lakini tunajitahidi kuhakikisha anaamka, yapo mambo ambayo Lucia alikuwa akiyafuatilia kuhusu Mgonjwa..” alisema Dktari

“Mgonjwa anaitwa Nani?” aliuliza maana kwenye ile sauti alisikia kuwa anaitwa Mandy

“Mgonjwa anaitwa Mandy Desmond”

“Huyo Desmond ni Mume wake?” alihoji Noela kwa kujikaza sana alitamani alie

“Ndiyo ni Mume wake wa ndoa”

Noela alimuonesha Daktari picha ya Desmond kwa kutumia simu “Ndiyo huyu Mume wake vipi unamjuwa?” alihoji Daktari “Hapana naifanya kazi yangu tu”

“Ooh! alafu kama sikosei yupo wodini, twende ukazungumze naye huwenda ana la kukwambia” Alisema Daktari huyo akionekana wazi kuwa alifahamu baadhi ya Mambo ila hakutaka kujiingiza matatizoni baada ya kifo cha Lucia

Noela na Daktari waliongozana hadi wodini lakini bahati mbaya Desmond alikuwa ameondoka wodini hapo muda mchache uliopita, Noela alifanikiwa kuujuwa ukweli, pale pale aliingia yule Polisi aliyekuwa akifuatilia hali ya Mandy, Alifahamiana na Daktari wakasalimiana lakini pia alifahamiana na Noela sababu alikuwa mpelelezi mzuri sana.

“Oooh Noela uko hapa, salam yako” Alisema Polisi huyo

“Hapana shaka unapeleleza juu ya kifo cha nesi wa mgonjwa” Alisema polisi huyo

“Ndiyo! wewe umekuja kufanya nini hapa?” aliuliza Noela

“Huyu Mgonjwa ni Mtu ninayesubiria aamke ili anipe siri ya kifo cha Mama yake” Alisema Polisi, Noela alishtuka sana

“Kuna kifo tena katika ugonjwa wake?”

“Ndiyo! kabla ya kukutwa na kilichomkuta alikuwa akiijuwa siri ya kifo cha Mama yake, hivyo kuamka kwake kutafungua kesi upya japo ni kesi ngumu sana” alisema polisi huyo na kumuacha Noela akiwa njia panda, hakujuwa ashike lipi aache

lipi kila alilolisikia lilimpa stori mpya kichwani pake akajiuliza haraka

“Kama Noela ameuawa na Mume wa Mandy maana yake ameuawa kwasababu kuna jambo lilipaswa kufichwa, ina maana Desmond alimuuwa Mama yake Mandy! mbona nachoka” Alijisemea kisha aliangusha tabasamu lenye maumivu makali sana ambayo si rahisi mwingine akafahamu.

“Haya sawa” alijibu Noela kisha alitoka hapo, alienda nyuma ya Hospitali alilia sana, aligundua Mwanaume aliyempenda alikwua Muuwaji na Muongo, alijipa moyo na tumaini kuwa atashinda kila jambo

Tuachane na kule Hospitalini, Mchana ulikuwa umeingia, Desmond hakuwa na hili wa lile kuwa Noela alikuwa amesha fahamu siri zake, alijaribu tena kumpigia Noela huku akiwa na Mwanasheria wake wakiwa ndani ya gari wakijiandaa kuelekea Hotelini.

Simu hiyo haikupokelewa kabisa

“Au amepata taarifa ya kifo cha rafiki yake imemchanganya?” alihoji Mwanasheria Joel

“Sina hata ninalolifikiria kwasasa Joel, naona mambo yanazidi kuwa magumu” Desmond aliwasha gari wakiwa na kitabu cha Hundi ya fedha ambacho waliambiwa na Yule Mwanaume waende nacho Hotelini

“Vipi umejaribu kumpigia Mtu wa tatu?” alihoji Desmond

“Naambiwa Namba haipo, huwenda anatumia simu kwa nyakati anazohitaji yeye mwenyewe. Desmond alikanyaga Mafuta kuelekea Hotelini wakiwa na tumaini kuwa wanaenda kujisafisha bila kujuwa bomu jipya lilikuwa limelipuka.

Walifika Hotelini kwa muda walioambiwa kisha walielekea Kwenye chumba walichoelekezwa, waliamini watamkuta Mwanaume huyo, walipofungua mlango walikutana na sanduku lililoibwa kwenye chumba cha Noela, sanduku hilo Desmond alikuwa akilijuwa alishtuka sana

“Hili ni sanduku la Noela, limefikaje hapa wakati nililitafuta sana ili kuipata ile bahasha” Aliuliza Desmond, walikagua chumbani humo na kujiridhisha kuwa hakukuwa na Mtu yeyote, walipogusa mlango wa sanduku hilo dogo waliona unafunguka kirahisi, sasa wakakutana na ile bahasha yenye siri nzito sana.

Desmond na Mwanasheria Joel walizisoma nyaraka zilizo ndani ya Bahasha hiyo, Desmond alikaa chini kwa kuchoka mno kisha akamwambia Joel

“Kama Noela atakuwa ameisoma hii Bahasha basi kila kitu kimeharibika Joel”

“Kama angekuwa amesoma angekuuliza, kwanini hasemi chochote hadi sasa?” aliuliza Joel

“Hajasema chochote lakini simu yangu hapokei tokea asubuhi wakati Mimi ni Mume wake mtarajiwa, tumevishana pete jana tu. Hapana shaka Anajuwa kitu fulani” Alisema Desmond kisha alikunbuka kitu akasema

“Ni Nani huyu anayefahamu kila kitu?” aliuliza, kabla hata hajapata jibu kutoka kwa Joel simu ya Desmond iliita, namba iliyopiga ilikuwa ngeni kabisa machoni pake

“Pokea!!” alisema Joel huku akimuonesha kwa ishara Desmond kuwa apokee haraka sana kabla haijakata, Desmond aliipokea

“Hello” Alisema Desmond huku simu ikiwa sikioni

“Desmond, mmeona kila kitu. Bahati iliyo njema ni kuwa Noela hajui chochote hadi hivi sasa, laiti kama atagundua kuwa wewe ni Muuwaji basi tegemea kuharibu kila kitu hata unachokitaka hakiwezi kufanikiwa” Ilisikika sauti nzito ya kiume, sauti hiyo haikuwa ngeni kwake ilikuwa ni sauti ya Mwanaume aliyewaambia waende pale Hotelini

“Wewe ni Nani na unataka nini hasa?” alihoji Desmond

“Mimi ni Mr. Nobody ( Sijulikani ) kila wakati naokoa Maisha yako sababu wewe ni mzembe sana Desmond, Hapana shaka umebeba kitabu cha Hundi?” Alisema Mwanaume huyo aliyejitambulisha kama Mr. Nobody

“Ndiyo lakini kwanini unafanya haya yote, unataka nini?” Aliuliza Desmond

“Fuata nitakayokwambia, andika hundi ya Shilingi Milioni mia tisa haraka sana kisha nitakuelekeza mahali unapopaswa kuipeleka, ukifanya ujanja wowote ule Maisha yako yatakuwa rehani sababu yapo mikononi Mwangu” Alisema Mr. Nobody, Desmond alimtazama Mwanasheria wa Mke wake aliyeitwa Joel, kisha alipewa ishara ya kuandika Hundi hiyo haraka sana ili kuhamisha pesa kutoka kwenye akaunti ya Kampuni ya Mandy na kupeleka kwa Mr. Nobody

Haraka Desmond akawa anaandika ile Hundi ili tu kujiweka salama, lakini kwenye sura ya Mwanasheria kulijaa tabasamu ambalo Desmond hakuliona, alipomtazama Joel alibadilisha sura

yake na kuwa ya hofu kama vile alikuwa akicheza mchezo mchafu kwa Desmond. Baada ya kumaliza kuandika aliweka tena simu sikioni

“Nimeshaandika, natakiwa kuipeleka wapi?” Aliuliza Desmond baada ya kuwa ameshamaliza kuandika hundi hiyo yenye thamani ya Milioni 900.

“Pembeni yako kuna Mwanasheria wa Mke wako mkabidhi hiyo Hundi kisha Mwambie ailete Katika Baa ya Silva, nje ya Baa ataiyona gari nyekundu, aiweke humo. Kumbuka anapaswa kwenda peke yake” Alisema Mr. Nobody kisha alikata simu.

“Amesema nikupatie wewe Joel kisha utaipeleka Silva Baa, utaona gari nyekundu utaiweka humo hii hundi. Nakuomba sana Joel fanya kama alivyotaka” Alisema na kusistiza Desmond

“Amesema niipeleke Mimi? vipi kama akinidhuru huko, Mimi naogopa Desmond” Alisema Joel.

“Sikia Joel acha woga nenda kaipeleke hii hundi, hakuna kitakacho kupata laiti kama angekuwa na lengo la kukudhuru amgekudhuru muda wote.”

“Haya sawa!” aliitikia Joel kisha walitoka hapo, nje alimpa ile Hundi ili aipeleke huko ambako ilipotakiwa kufika, Joel aliingia kwenye gari kisha akaondoka zake pale.

Wakati Joel anaondoka, simu ya Desmond iliita, aliyekuwa akimpigia alikuwa ni Mchumba wake Noela, kwanza aliitafakari hiyo simu kabla ya kuipokea maana alikuwa na hofu kubwa sana juu ya mambo yao kugundulika, baadaye aliipokea

“Hello” Alisema Desmond

“Joshua naomba tuonane kwenye mgahawa muda huu” Alisema Noela kisha alikata simu, Desmond alishusha pumzi zake baada ya kujiridhisha kuwa Noela hajagundua lolote maana kama angedungua asingemuita jina la Joshua bali angemuita Desmond, kumbe Noela alishajuwa kila kitu, alikuwa katika upelelezi wake binafsi

Desmond alipotoka pale Hotelini moja kwa moja alienda kuonana na Mchumba wake Noela kama alivyoambiwa, alimkuta Noela akiwa amejawa na tabasamu na bashasha kitu ambacho kilimfanya Desmond azidi kujiamini kuwa Noela hajafahamu lolote lile, waliagiza chakula huku Noela akizidi kumsoma Desmond, akili ya Desmond haikutulia kabisa sababu alihitaji kufahamu kama Joel alikuwa amefanikiwa kupeleka Hundi ile kwa Mtu wa Tatu
 
SEHEMU YA KUMI

“Nimetoka Hospitali, unamkumbuka yule rafiki yangu uliyewahi kuniona naye hapa?” aliuliza Noela makusudi ili kuzidi kumsoma Desmond

“Eeeh nakumbuka, anaumwa?” alihoji Desmond

“Hapana amekutwa ameuawa huko porini, inasikitisha mno alafu kaacha Mama anayeumwa sana” Alisema Noela huku akiwa makini sana na jicho lake la uchunguzi, Desmond alishtuka mno huku macho yake yakiwa yamemtoka pima kama Mjusi aliyebanwa na mlango

“Ameuawa…..Nani aliyemuuwa?” alihoji Desmond akiwa katika hali ya kuchanganikiwa sana, Noela akagundua kuwa alichokuwa ametumiwa na marehemu Lucia kilikuwa na ukweli mtupu

“Haijajulikana, polisi wanafanya uchunguzi. Inasemekana pia ameacha mgonjwa ambaye yupo mahututi na huyo mgonjwa inawezekana kuwa chanzo cha kifo cha Lucia” Alisema Noela huku jicho lake likiongeza umakini wa kumtambua Desmond

“Mgonjwa!! aaah Noela, naomba tuachane na hizo stori, tumekuja hapa kula Mpenzi” Alisema Desmond kisha alimwambia Noela

“Naenda chooni mara moja” Desmond alinyanyuka akaelekea Chooni bila kujuwa kuwa Noela alikuwa tayari amegundua kuwa yeye ni Muuuwaji

Japo moyo ulimuuma sana Noela ila kilichompata Lucia alijiona ana kila sababu ya kuleta haki, Desmond alipofika chooni alijiinamia kwenye sinki la kunawia maji akiwa amechoka sana, alianza kuhisi ugumu mkubwa sana kwenye Maisha yake, alimpigia simu Joel akamuuliza kama amekutana na huyo Mtu wa Tatu.

Joel akiwa ndani ya gari hilo aliloelekezwa alipokea simu, alionekana kuzungumza kwa kutulia sana huku pembeni yake kukiwa na mwanaume mmoja

“Nimeshampatia” Alisema Joel

“Haya basi tukutane mara moja pale tunapokutanaga….naona mambo magumu, Kifo cha Lucia kimekuja kuharibu kila kitu” Alisema Desmond, baada ya simu ya Desmond kukatwa Joel alimgeukia Mwanaume ambaye yupo ndani ya hiyo gani akamwambia

“Ngoma imeanza kuchezwa, Hii Hundi hakikisha unachukua pesa na kuziweka kwenye akaunti nyeusi, ni lazima tumtumie Desmond kuvuna pesa alafu kila kitu kitamuangukia mwenyewe” Aliagiza Mwanasheria Joel, kumbe mwanasheria Joel ambaye ni mwanasheria wa Mandy ndiye Mtu wa tatu ambaye alikuwa akijifanya kuzunguka kwenye suala lililojificha ili apate pesa kutoka kwa Desmond kwa kujifanya anajuwa siri za Desmond, Mwanaume aliye pembeni yake ndiye yule ambaye Desmond alikuwa akimtilia shaka na ndiye aliyekuwa akifanya michezo mingi michafu na ndiye aliyelitoa lile gari kule Baharini kisha akaliweka gari lingine kisha akawapigia simu polisi

Basi, Baada ya kumaliza kuongea na Joel akifikiria ni Mtu mzuri anayeshirikiana naye alirudi kwa Noela ambaye alijifanya yupo bize akipata chakula, angalau baada ya kutoka Chooni alionekana kuwa sawa japo Noela alikuwa ameshamgundua muda mrefu, walipata chakula ndipo Noela alipomchomekea Desmond

“Nasikia Mgonjwa wa Marehemu Lucia ameamka leo, ingekuwa faraja sana kwa Lucia kumuona mgonjwa aliyemhudumia kwa muda mrefu akiamka” Alisema kwa mtego Mkubwa sana na Desmond akaingia mtegoni, alishtuka akauliza

“Unamaanisha Mandy?” alihoji akiwa ameamka kutoka kitini, ndipo sasa akawa amemdhihirishia wazi Noela kuwa ana Mke pia ni Muuwaji

Noela naye akaamka akijifanya kushangaa

“Heee kumbe unamjuwa?” Alihoji Noela

“Hapana….Hapana simjui, Noela tutaonana baadaye” Alisema Desmond kisha aliondoka mbio kuelelekea Hospitalini bila kujuwa kuwa alikuwa ametegwa, Haraka Noela alimfuata kwa nyuma kisha naye aliingia kwenye gari yake akawa anamfuatilia Desmond kwa nyuma, Safari hii ilifika hadi kwenye Hospitali aliyolazwa Mandy

Akiwa amepaki gari eneo lingine la Hospitali tofauti na alipopaki Desmond, Noela alipokea ujumbe kuwa Mgonjwa Mandy amerudisha fahamu, huu ulikuwa ni ujumbe kutoka kwa Daktari Mkuu wa Hospitali sababu alimuachia maagizo kuwa akiamka Mandy apewe taarifa na pia alipewa agizo moja kubwa sana, Noela akakumbuka alichomwambia Daktari

Alimwambia kuwa anafanya uchunguzi wa kifo cha Lucia na huwenda mgonjwa huyo akawa ndiyo chanzo cha kifo cha Lucia hivyo atakapoamka pengine kuna siri anaifahamu hivyo kitu cha kwanza ahakikishe anamuweka sawa kiakili ili Desmond asishtuke mapema hadi pale watakapopata ushahidi wa kutosha

Akiwa mbio mbio, Desmond alifunga breki miguuni mwa Daktari Mkuu aliyekuwa akitoka wodini kwa Mandy

“Dokta nimesikia Mke wangu ameamka” Alisema Desmond akiwa katika hali ya haraka na hofu mno

“Ndiyo Mkeo ameamka ila bado hana nguvu, unaweza ukamuona ila usimkumbushe chochote” Alisema Dokta, Basi Desmond aliufungua mlango wa wodi hiyo, kweli alimuona Mandy akiangaza huku na kule kama Mtu aliyekuwa akijiuliza yupo wapi

Hofu ilimjaa sana Desmond kisha alimsogelea Mandy taratibu huku akiwa mwenye maswali mazito sana ya kuwa Mandy amemjuwa Desmond kuwa ni Muuwaji wa Mama ake, Mandy alipomuona Desmond alionekana wazi kuwa na maumivu makali moyoni, alimtazama Desmond huku chozi likimbubujika, yule Daktari Mkuu alisimama mlangoni akichungulia tu

Mandy alikumbuka siku ya tukio la yeye kupigizwa ukutani na Desmond, siku hiyo ilikuwa hivi, aliiyona cheni ya Mama yake kwenye koti la suti la Desmond, cheni ambayo Desmond aliivua kwenye shingo ya Mama Mandy baada ya kumuuwa kisha akaiweka kwenye koti lake, Mandy alipoiyona ile cheni ndipo alipogundua kuwa Desmond ni Muuwaji, wakati anapiga Simu Desmond alitokea ndipo vurugu za kufukuzana zilipoanza

Tuendelee, Basi Desmond alisogea na kumshika mikono Mandy akamwambia

“Umeamka Mama?” alihoji Desmond

“Wewe ni Nani?” aliuliza Mandy, Desmond alishtuka sana kisha akajiuliza ina maana Mandy amepoteza kumbukumbu zake, alijikuta akitabasamu maana kama amepoteza kumbukumbu hatoweza kumtaja kama Muuwaji wa Mama yake.

“Pole kwa maumivu sawa Eeh!! Mimi ni Mume wako Desmond” Desmond alijitambulisha pale, Daktari alielekea moja kwa moja kwenye maegesho ya Magari akamwambia Noela kuwa Mandy amefanya kama alivyoagizwa yaani kujifanya amepoteza kumbukumbu.

“Safi sana, Desmond ni mchumba wangu na hii pete amenivisha jana tu” Alisema Noela kisha aliivua pete hiyo

“Sistahili kuwa na pete yake sababu ni Mume wa Mtu pia Muuwaji, kwakuwa ameshajulikana ndiye Muuwaji basi kazi iliyobakia niachie Mimi”

“Sawa!!” Noela aliondoka Hospitalini hapo.

Desmond alibakia Hospitali kwa ajili ya kuangalia kama kuna chochote Mandy anaweza akakumbuka, hii ilimfanya yule Daktari ashindwe kumpa taarifa muhimu Noela.

Jioni ilipoingia ilimkuta Noela akiwa nyumbani kwao akiwa kwenye tafakari nzito kuhusu Desmond ambaye alimdanganya jina kama Joshua, alikumbuka vingi ikiwemo walipotoka, alijikuta akiangusha chozi lenye maumivu makali sana, mapenzi aliyompa Desmond yalikuwa ya dhati sana kwa kipindi chote, kugundua kuwa Desmond alikuwa Muuwaji na Muongo kulimliza sana Noela.

Alijikuta kwenye wakati mgumu sana, ndiyo alimpenda sana Desmond hadi kufikia hatua ya kuvishwa pete lakini angefanya nini wakati Mwanaume huyo alikuwa Muongo na Muuwaji.

Jioni hiyo alitoka akarudi kule Hospitali, Desmond alikuwa wodini kwa kipindi chote akiwa na mawazo kuwa huwenda Mke wake atarudisha kumbukumbu muda wowote ule, ili kumtoa pale Noela alimtumia meseji Desmond akimwambia

“Mpenzi naelekea kwenye pori ambalo Lucia aliuawa, kuna taarifa kuwa alipotoka nyumbani kwao alitoka na kitabu chenye siri pengine nacho kilikuwa ni sababu ya kifo chake, inasemekana kilipotea porini” Alipotuma meseji hiyo alijuwa wazi kuwa Desmond ataenda huko porini ili kuhakikisha alichoambiwa, kweli muda huo huo Desmond alikurupuka kutoka pale wodini akaingia kwenye gari kisha akatoka.

Lakini wakati anatoka Desmond, yule Mwanaume anayetumwa kazi na Mwanasheria Joel alikuwa pale ndani akamuona Desmond akitoka kisha Noela aliingia wodini, yule Mwanaume alimpigia simu Joel haraka sana akamwambia alichokiona, basi haraka Joel alimpigia simu Desmond na kumueleza kuwa kulikuwa na mchezo uliokuwa ukichezwa hapo na kwamba mpenzi wake Noela alikuwa hapo Hospitalini na baada ya yeye kutoka Mpenzi wake huyo aliingia wodini kwa Mke wake Mandy.

Desmond alisitisha safari ya kwenda eneo ambalo Lucia aliuawa baada ya kuambiwa kuwa kuna mchezo mchafu Hospitalini, haraka aligeuza gari akarudi kule Hospitalini, akiwa hoi hai aliingia wodini na kumkuta Mandy akiwa amelala huku chumba hicho kikiwa kimya sana, Desmond alishangaa sana wakati aliambiwa na Joel kuwa mpenzi wake alikuwa hapo, akaamuwa kumpigia simu ili ajihakikishie alichoambiwa, simu ilipopokelewa ilionesha wazi kuwa Noela alikuwa barabarani hivyo alishindwa kuthibitisha alichoambiwa, alimpigia simu Joel na kumwambia alichokiona lakini Joel alimtaka Desmond kuwa makini sana maana Mpenzi wake alikuwa hapo Hospitalini na huwenda anafahamu kuhusu Mandy.

Alienda kukutana na Mwanasheria Joel ambaye alikuwa akimchezea Mchezo mchafu, Joel alimuonesha video Desmond iliyomuonesha Noela akiingia na kutoka pale wodini, ndipo alipopata picha kamili kuwa Noela alikuwa amefanikiwa kumfahamu, Joel alimuuliza

“Huyo ameshajuwa siri kuwa wewe ni Muuwaji, kibaya zaidi huyo ni mpenzi wako alafu mpelelezi utafanya nini?” Desmond alikaa kimya baada ya sekunde kadhaa akamwambia

“Nitajuwa cha kufanya” Desmond alitoka kuonana na Joel, alionekana kuwa mwenye mawazo sana ya nini afanye, alimpigia simu Noela akamuuliza kama alifanikiwa kukipata hicho kitabu, alifanya hivyo makusudi ili kumfanya Noela afahamu kuwa bado Desmond hajajuwa chochote.

Noela alimwambia kuwa hawakufanikiwa kukipata kitabu ila uchunguzi bado unaendelea, Desmond alipata wazo la haraka nalo ni kuondoa uhai wa Noela maana Mke wake hakumbuki chochote hivyo kwa vyovyote Mtu anayeweza kusema ukweli ni Noela.

Alimtunia ujumbe wakutane nyumbani kwake usiku wa siku hiyo, baada ya kuupata ujumbe Noela aliwataarifu polisi aliokuwa akifanya nao kazi maana alihisi huwenda Desmond alishafahamu kuwa anaijuwa ile siri ya Mauwaji. Usiku ulipofika Noela alienda nyumbani kwa Desmond, alimkuta akiwa ameketi mahali anapata bia

Noela aliketi naye akapata chupa ya Bia bila hata kumsemesha Desmond, waligida kidogo kisha Desmond alimuuliza Noela

“Umemuaga Mama?”

“Ndiyo!!” Alijibu Noela

“Siku moja ya uchumba wetu umeshavua pete ya uchumba” Alisema Desmond ndipo Noela aliposhtuka sasa kuwa Desmond alikuwa ameshafahamu.

“Nafikiri ni kitu cha kawaida, inakuwaje kwa Mtu akawa na majina mawili, la uhalisia analificha na kutumia jina feki?” Alisema Noela, hakukuwa na siri tena sababu kila jambo lilikuwa wazi

“Noela umekuwa kikwazo kwangu, ili niwe salama ni lazima nikutangulize” Alisema Desmond kisha alitoa bastola akawa anaifutafuta

“Kwa mpelelezi ambaye amefanya kazi nyingi hawezi kuogopa kufanya kazi hata kama ni hatari kiasi gani au inamgusa ampendaye, Desmond….kumbe una Mke tena ni Mke ambaye ulitaka kuutoa uhai wake kisa pesa, unakumbuka kuhusu Mama Mandy?” aliuliza Noela, Desmond alijawa na hasira akamnyooshea Noela

“Kabla hujaniuwa Desmond, nataka nikwambie kitu kimoja. Pesa haiwezi kukupa kila kitu katika Maisha yako, ila Maisha yanaweza kukupa kila kitu ikiwemo na pesa, waliochagua kuishi walifanikiwa lakini wewe ulichagua pesa ili uishi”

“Ishia hapo hapo Noela” Alisema Desmond kisha alifyatua risasi iliyowashtua polisi aliokuja nao Noela

Haraka waliingia na kumkuta Noela akiwa chini anaugulia maumivu ya bega, bastola ikawa udhibiti kwa Desmond, alikamatwa na wale polisi. Taarifa ya kukamatwa kwa Desmond ilimfikia Joel, akapata wazo la kuikimbia Nchi maana alishajuwa kuwa atatajwa na kukamatwa, Naam!! alitajwa na Desmond, Joel alienda kukamatwa Uwanja wa ndege….

Taarifa ya kukamatwa kwa Joel na Desmond ilimfanya Mandy alie kwa uchungu mkubwa, baada ya kupona kwa Noela, Desmond na Joel walifikishwa Mahakamani kwa makosa ya Mauwaji, Mandy alisimama kama Shahidi namba moja, Hatimaye Desmond na Joel walifungwa kifungo cha Maisha jela, Mandy alimshukuru sana Noela kwa msaada huo hadi kukamatwa kwa Wauwaji

Noela aliishia maisha ya majuto sana sababu aliamini kama angelifanyia kazi mapema bahasha aliyopewa na Lucia basi rafiki yake huyo asingeliuaawa

MWISHO
 
Back
Top Bottom