Yericko Nyerere
Platinum Member
- Dec 22, 2010
- 17,027
- 20,519
Nimeumia sana, imenichukua masaa kadhaa kusema chochote baada ya uamuzi huu mgumu wa waliokuwa viongozi wakuu wa Chama changu Chadema Naibu Katibu Mkuu Bara Mh Kigaila, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Mh Salumu Mwalimu na Waliokuwa wajumbe wa Sekretaieti yote ya Chama kujivua uanachama wa Chadema.
Nimeumia kwasababu tatizo hili uongozi mpya umeshindwa kulitibu tangu uchaguzi ulipomalizika, Tulishauri uongozi mpya uwaunganishe wanachama waliogawanyika baada ya Uchaguzi, Lakini walioshinda wakakomaza mafuvu na kutupuuza, wakatuita tuna madonda ya uchaguzi hayajapona kisha tukaitwa wasaliti na mwisho tukaitwa maccm. Haya ndio yametufikisha hapa.
Katika siasa lolote linatokea, huu ndio utofauti wa siasa na harakati, Mwanasiasa anafikiria kushika madaraka ili afanye mageuzi ya sheria na mifumo mbali mbalimbali ya kijamii. Wakati huo Mwanaharakati anafikiria kuhimiza mageuzi ya sheria na mifumo mbalimbali ya kijamii, Yaani mwanaharakati hafikirii kuitoa ccm madarakani bali kuishinikiza ccm ifanye mageuzi ya sheria na mifumo ya kijamii tu, Kwamba ccm ikitekeleza madai hayo, basi mwanasiasa huyo anaweza kuhamia tu katika madai mengine mfano haki ya wanafunzi wa kike kupewa taulo za kike, Haki ya wanaume kupata unyumba kwa wake zao, nk. Hii ndio tofauti kuu.
Ninawapongeza viongozi hawa kwa uamuzi wao ili wakatimize ndoto zao katika majukwaa mengine kwakuwa jukwa lako walilolijenga kwa maisha yao likawa jukwaa pendwa kwa umma limeharibiwa na wanaona linaenda shimoni. Vyama vya siasa ni vyama vya hiyari, ukiona hapa wenzio hawakutaki basi unatafuta jukwaa lingine.
Niwatakie mapambano mema huko waendako, Mimi nitapambana ndani ya Chadema ili kujaribu kukirejesha chama kwenye misngi yake na kuhakikisha chama kinafuata katiba na miongozo yake, Na kurejesha umoja na mshikamano uliojengwa kwa miaka mingi.
Nimeumia sana chama changu kuvunjika na kuparaganyika siku 70+ tu za uongozi mpya!😭😭😭😭
WE SHALL WIN!
Na Yericko Nyerere