Mbigirikavu
Senior Member
- Aug 19, 2022
- 101
- 118
Pamoja na droo ya 1-1 Singida Big Stars dhidi ya Simba FC, na Yanga kuwapiga Waarabu waoga wa Tunisia, ukweli ni kwamba matokeo ya Mamelody Sundown Ladies 1-0 Simba Queens yameniumiza mara mia ya yote yaliyotokea jana. Yaani natamani mechi irudiwe.
Hata kama Refa kapendelea Mamelody, hakuna cha maana kitakachofanyika cha kuinufaisha Simba Queen. Pongezi kwa Simba yote, namaanisha yote, hakuna wa kulaumiwa.
Mabinti wamefanya kila wawezalo na tumeona walivyopambana kwa jasho na damu, na hapa ndipo panaponiumiza zaidi. Sina cha kulaumu kuanzia uongozi, benchi la ufundi, wachezaji na mashabiki.
Labda ushauri wangu kwa kile nilichokiona ni kwamba, Mamelody walikuwa na nguvu kubwa, na Simba waliingia na mtindo wao wa kasi na nguvu ambapo kipindi cha pili walionekana kuzidiwa kidogo.
Labda wangeanza na mchezo wa kutunza nguvu kwa kupiga pasi fupi eneo la katikati badala ya pasi ndefu ambazo zilikuwa na 'rebounds' nyingi na mipira kurudi haraka kwa mabeki.
Lakini yote kwa yote nimehuzunika kutolewa. Nawaombea ushindi kwenye mechi yao ya mwisho ya kutafuta mshindi wa tatu.