Nimeumwa na Kichwa Baada ya Kuisoma Definition ya Serikali ya J/Muungano kwenye Rasimu ya 2

''Jamuhuri ya muungano wa Tanzania ni nchi na shirikisho lenye mamlaka kamili ambalo limetokana na Muungano wa nchi 2 za jamuhuli ya Tanganyika na Zanzibar ambazo kabla ya hati ya makubaliano ya Mungano wa mwaka 1964, zilikuwa nchi huru.,''

My Take: Kama Jamuhuli ya Muungano ni NCHI ya shirikisho lenye mamlaka hizi nchi nyengine Tanganyika na Zanzibar zitakuwa na nini?

Kwa mtazamo wangu wa haraka haraka hapa ni kwamba Nchi moja kubwa ambayo ni ya Muungano itakuwa na mamlaka kuizimeza nchi 2 ndogo, na si dhani kama hizi nchi nyengine zitakuwa nchi kweli hapa kwa wale ndugu zetu kule visiwa vya kalafuu Zanzibar watakuwa wamepigwa changa la macho,

Ningeshauli waendelee na mfumo uliopo kwa kadhia hii itakayokuja kuwapata ndugu zetu kule Zanzibara ambao walipindua na kupata uhulu wao.

Ivi muunago wa shirikisho umewahi kuwa ni nchi duniani? kuna nchi duniani yaitwa muungano?

Kibaya Zaidi lasimu pia imeeleza mipaka ya JMT itakuwa yote ya Tanganyika na Zanzibar: ndugu hapa hakuna mabadiliko ni kumezwa zaidi.

kwenu wanajamvi..

Rudi darasani ukajifunze kuhusu matumizi sahihi ya r NA l
 
Aisee mi ndio maana nilipendekeza serikali MOJA TU.! Nikasema neno Zanzibar lifutike kama Tanganyika lilivyofutika ili tuwe na mkoa wa unguja na wa pemba. Sherehe za uhuru na mapinduzi zisiwepo badala yake iwepo ya Muungano tu.
 
siyo ww ni njaa yako tu iyo samuel 6 anakugaia elf4 kwa siku., muda unao bado mshawishi warioba na JK waifaye nchi 1

Ndo matatizo yenu! Kila anayetoa maoni yake anatumwa kwa kupewa pesa. Mkuu mkate wangu naupata kwa kutumia vyetu safi kabisa bila kumnyenyekea mtu ndo maana nipo huru kutoa maoni yangu!
 
Mimi nilipendekeza kuwe na tanganyika na zanzibar ambazo zinaongozwa na mawaziri wakuu wanaochaguliwa na wawe wakuu wa serikali zao. Kwenye muungano kuwe na rais na makamu wake ambaye atakuwa ndio mtendaji mkuu, huku hakuna waziri mkuu. Rais atakuwa amiri jeshi mkuu na kiongozi wa nchi. Hawa watasimamia mambo ya muungano tu. Mambo ya tanganyika yanakuwa ya watanganyika na zanzibar yanakuwa ya wao. Sio mambo ya sasa mzanzibari anapewa wizara ya watanganyika aafu watu wamekaa kimya!
 
Umeongea pumba ivi nchi iliyopoteza roho za ngugu zao kwa kuikomboa nchi yao leo iongozwe na Waziri Mkuu?? Me nashangaa sn ivi kwani nani anataka huu muungano? kwanini watanganyika leo wanawatafutia wazanzibar kila rai ilmradi wawe kwenye Muungano maana yk ni nini? kama si kutawaliwa na sultani mweusi??
 
Kinacho changanya ni hilo shirikisho kuitwa Nchi katika tafsiri yake., badala ya kuitwa shirikisho tu., ili nchi zibaki kuwa zile zile 2 ya Zanzibar na Tanganyika na ndivyo miungano yote inavyokuwa duniani., ilikuwa iitwe ivi ''shirikisho la muungano wa nchi za Tanzania''

Tulienda kivyetu miaka 50, tulikuwa na muungano usiofahamika na ili kuendeleza fikira za waanzilishi wetu tutaendelea kuchonga muungano kivyetu usitafute reference ya muungano wetu hutoikuta ulimwengu huu!
 
Mifano ya tawala(nchi) zilizoungana na kuunda shirikisho la nchi (Federal state) ni kama United States of America ni muungano wa tawala (nchi) huru 50 ambazo zimeunda hiyo inayoitwa USA. Pamoja na USA kuwa na katiba ya Federal Lakini hizo states kila moja ina katiba yake na uongozi wake chini ya Gavana. Uingereza(United Kingdoms)ni muungano wa tawala huru za Kifalme. Muungano wetu wa Tanganyika na Zanzibar (JMT) iwe na kiongozi mmoja atakaye tambulika kama Rais na mamlaka kamili juu ya nchi shiriki. Hivyo basi tunacho takiwa ni kila nchi(State) kuwa na kiongozi wa State atakaye tambulika kama Gavana au Waziri Mkuu, badala ya yeye naye kutambulika kama Rais. Hivyo katiba yetu ya Muungano inabidi pia itamke kiongozi wa Tanganyika na Zanzibar watambulike kwa title gani! Gavana au waziri Mkuu lakini siyo Rais. Tuwe na Rais mmoja tu wa Muungano.
 
Halafu kuna watu watapiga kura kukubali rasimu ya Katiba hii bila kujua wanakubali kitu kisichokuwepo! Huwezi kupigia kura kuukbali "shirikisho la nchi mbili" wakati moja haina hata serikali...
 
mzee mwanakijji yatosha elimu hyo, hakuna kupiga kura hadi tujue maslahi ya Tanganyika vinginevo ni kuwapa ccm ulaji tu
 
Mifano ya tawala(nchi) zilizoungana na kuunda shirikisho la nchi (Federal state) ni kama United States of America ni muungano wa tawala (nchi) huru 50 ambazo zimeunda hiyo inayoitwa USA. Pamoja na USA kuwa na katiba ya Federal Lakini hizo states kila moja ina katiba yake na uongozi wake chini ya Gavana. Uingereza(United Kingdoms)ni muungano wa tawala huru za Kifalme. Muungano wetu wa Tanganyika na Zanzibar (JMT) iwe na kiongozi mmoja atakaye tambulika kama Rais na mamlaka kamili juu ya nchi shiriki. Hivyo basi tunacho takiwa ni kila nchi(State) kuwa na kiongozi wa State atakaye tambulika kama Gavana au Waziri Mkuu, badala ya yeye naye kutambulika kama Rais. Hivyo katiba yetu ya Muungano inabidi pia itamke kiongozi wa Tanganyika na Zanzibar watambulike kwa title gani! Gavana au waziri Mkuu lakini siyo Rais. Tuwe na Rais mmoja tu wa Muungano.

Unalotaka wewe ndilo walilokataa Zanzibar. Hawataki kukosa kuwa na Rais, unachokitaka wewe ni sawa lakini kama tukiwa na shirikisho la mikoa ya Wachaga, wanyakyusa, wasukuma, wahehe .....waunguja na wapemba, Wazenj hawataki. Anachotaka Waryoba na Kikwete siyo Shirikisho, ni Jamhuri huku kiuhalisia siyo Jamhuri. Tatizo la nchi hii ni ulaji, ukisema sana wanakuita "Meli iliyozama" na matusi kibao. Waacheni waTzBara waende huko tunakoenda sasa. Tutakutana kujadili kero baadaye.
 
Tulienda kivyetu miaka 50, tulikuwa na muungano usiofahamika na ili kuendeleza fikira za waanzilishi wetu tutaendelea kuchonga muungano kivyetu usitafute reference ya muungano wetu hutoikuta ulimwengu huu!

Sasa hivi kuna washambenga huko ulaya wanatuita:Tanzania, United Republic of Zanzibar Urban! Upo hapo?
 
Yule Mzee haambiliki (Nyerere) aliwabeza wenziwe kwa kusema kiongozi regerege huzaa serikali regerege akasahau kuwa kiongozi controversial huzaa muungano controversial!
 
Duh! Mkuu! Ni kama ulizaliwa naye yule Mzee kwa falsafa zako!

Na ukisikia alikuwa haambiliki ni kweli. Siku moja wakati wakitoka Tabora School kwenda likizo walipewa chakula cha njiani. Walipofika Mwanza Wasukuma wote ikawabidi kuteremka. Julius akasema "Msiteremke mpaka tule wote hiki chakula" Wakurya wakapinga wakihofia kucheleweshwa safari ya kwenda Butiama na Musoma. Julius alicharuka nusura azipige, " Kwa nini chakula cha wasukuma na wakurya kwa pamoja kikaliwe na wakurya tu?" Alikuwa kweli haambiliki na walikila hapo hapo Mwanza mpaka kikaisha.

Angekuwepo sasa hivi, Mkuu mambo yangenyoka. Lakini ndiyo basi tena!
 
''Jamuhuri ya muungano wa Tanzania ni nchi na shirikisho lenye mamlaka kamili ambalo limetokana na Muungano wa nchi 2 za jamuhuli ya Tanganyika na Zanzibar ambazo kabla ya hati ya makubaliano ya Mungano wa mwaka 1964, zilikuwa nchi huru.,''

My Take: Kama Jamuhuli ya Muungano ni NCHI ya shirikisho lenye mamlaka hizi nchi nyengine Tanganyika na Zanzibar zitakuwa na nini?

Kwa mtazamo wangu wa haraka haraka hapa ni kwamba Nchi moja kubwa ambayo ni ya Muungano itakuwa na mamlaka kuizimeza nchi 2 ndogo, na si dhani kama hizi nchi nyengine zitakuwa nchi kweli hapa kwa wale ndugu zetu kule visiwa vya kalafuu Zanzibar watakuwa wamepigwa changa la macho,

Ningeshauli waendelee na mfumo uliopo kwa kadhia hii itakayokuja kuwapata ndugu zetu kule Zanzibara ambao walipindua na kupata uhulu wao.

Ivi muunago wa shirikisho umewahi kuwa ni nchi duniani? kuna nchi duniani yaitwa muungano?

Kibaya Zaidi lasimu pia imeeleza mipaka ya JMT itakuwa yote ya Tanganyika na Zanzibar: ndugu hapa hakuna mabadiliko ni kumezwa zaidi.

kwenu wanajamvi..

Hizi shule za kata zimeleta shida...
Yaani hata kuandika kwa ufasaha kwa kiswahili napo shida!

Any ways...ndoho tahabhuuu...
 
Back
Top Bottom