Nimeumwa na Kichwa Baada ya Kuisoma Definition ya Serikali ya J/Muungano kwenye Rasimu ya 2


Rudi darasani ukajifunze kuhusu matumizi sahihi ya r NA l
 
Aisee mi ndio maana nilipendekeza serikali MOJA TU.! Nikasema neno Zanzibar lifutike kama Tanganyika lilivyofutika ili tuwe na mkoa wa unguja na wa pemba. Sherehe za uhuru na mapinduzi zisiwepo badala yake iwepo ya Muungano tu.
 
siyo ww ni njaa yako tu iyo samuel 6 anakugaia elf4 kwa siku., muda unao bado mshawishi warioba na JK waifaye nchi 1

Ndo matatizo yenu! Kila anayetoa maoni yake anatumwa kwa kupewa pesa. Mkuu mkate wangu naupata kwa kutumia vyetu safi kabisa bila kumnyenyekea mtu ndo maana nipo huru kutoa maoni yangu!
 
Mimi nilipendekeza kuwe na tanganyika na zanzibar ambazo zinaongozwa na mawaziri wakuu wanaochaguliwa na wawe wakuu wa serikali zao. Kwenye muungano kuwe na rais na makamu wake ambaye atakuwa ndio mtendaji mkuu, huku hakuna waziri mkuu. Rais atakuwa amiri jeshi mkuu na kiongozi wa nchi. Hawa watasimamia mambo ya muungano tu. Mambo ya tanganyika yanakuwa ya watanganyika na zanzibar yanakuwa ya wao. Sio mambo ya sasa mzanzibari anapewa wizara ya watanganyika aafu watu wamekaa kimya!
 

Umeongea pumba ivi nchi iliyopoteza roho za ngugu zao kwa kuikomboa nchi yao leo iongozwe na Waziri Mkuu?? Me nashangaa sn ivi kwani nani anataka huu muungano? kwanini watanganyika leo wanawatafutia wazanzibar kila rai ilmradi wawe kwenye Muungano maana yk ni nini? kama si kutawaliwa na sultani mweusi??
 

Tulienda kivyetu miaka 50, tulikuwa na muungano usiofahamika na ili kuendeleza fikira za waanzilishi wetu tutaendelea kuchonga muungano kivyetu usitafute reference ya muungano wetu hutoikuta ulimwengu huu!
 
Mifano ya tawala(nchi) zilizoungana na kuunda shirikisho la nchi (Federal state) ni kama United States of America ni muungano wa tawala (nchi) huru 50 ambazo zimeunda hiyo inayoitwa USA. Pamoja na USA kuwa na katiba ya Federal Lakini hizo states kila moja ina katiba yake na uongozi wake chini ya Gavana. Uingereza(United Kingdoms)ni muungano wa tawala huru za Kifalme. Muungano wetu wa Tanganyika na Zanzibar (JMT) iwe na kiongozi mmoja atakaye tambulika kama Rais na mamlaka kamili juu ya nchi shiriki. Hivyo basi tunacho takiwa ni kila nchi(State) kuwa na kiongozi wa State atakaye tambulika kama Gavana au Waziri Mkuu, badala ya yeye naye kutambulika kama Rais. Hivyo katiba yetu ya Muungano inabidi pia itamke kiongozi wa Tanganyika na Zanzibar watambulike kwa title gani! Gavana au waziri Mkuu lakini siyo Rais. Tuwe na Rais mmoja tu wa Muungano.
 
Halafu kuna watu watapiga kura kukubali rasimu ya Katiba hii bila kujua wanakubali kitu kisichokuwepo! Huwezi kupigia kura kuukbali "shirikisho la nchi mbili" wakati moja haina hata serikali...
 
mzee mwanakijji yatosha elimu hyo, hakuna kupiga kura hadi tujue maslahi ya Tanganyika vinginevo ni kuwapa ccm ulaji tu
 

Unalotaka wewe ndilo walilokataa Zanzibar. Hawataki kukosa kuwa na Rais, unachokitaka wewe ni sawa lakini kama tukiwa na shirikisho la mikoa ya Wachaga, wanyakyusa, wasukuma, wahehe .....waunguja na wapemba, Wazenj hawataki. Anachotaka Waryoba na Kikwete siyo Shirikisho, ni Jamhuri huku kiuhalisia siyo Jamhuri. Tatizo la nchi hii ni ulaji, ukisema sana wanakuita "Meli iliyozama" na matusi kibao. Waacheni waTzBara waende huko tunakoenda sasa. Tutakutana kujadili kero baadaye.
 
Tulienda kivyetu miaka 50, tulikuwa na muungano usiofahamika na ili kuendeleza fikira za waanzilishi wetu tutaendelea kuchonga muungano kivyetu usitafute reference ya muungano wetu hutoikuta ulimwengu huu!

Sasa hivi kuna washambenga huko ulaya wanatuita:Tanzania, United Republic of Zanzibar Urban! Upo hapo?
 
Sasa hivi kuna washambenga huko ulaya wanatuita:Tanzania, United Republic of Zanzibar Urban! Upo hapo?
Yule Mzee haambiliki (Nyerere) aliwabeza wenziwe kwa kusema kiongozi regerege huzaa serikali regerege akasahau kuwa kiongozi controversial huzaa muungano controversial!
 
Yule Mzee haambiliki (Nyerere) aliwabeza wenziwe kwa kusema kiongozi regerege huzaa serikali regerege akasahau kuwa kiongozi controversial huzaa muungano controversial!

Duh! Mkuu! Ni kama ulizaliwa naye yule Mzee kwa falsafa zako!

Na ukisikia alikuwa haambiliki ni kweli. Siku moja wakati wakitoka Tabora School kwenda likizo walipewa chakula cha njiani. Walipofika Mwanza Wasukuma wote ikawabidi kuteremka. Julius akasema "Msiteremke mpaka tule wote hiki chakula" Wakurya wakapinga wakihofia kucheleweshwa safari ya kwenda Butiama na Musoma. Julius alicharuka nusura azipige, " Kwa nini chakula cha wasukuma na wakurya kwa pamoja kikaliwe na wakurya tu?" Alikuwa kweli haambiliki na walikila hapo hapo Mwanza mpaka kikaisha.

Angekuwepo sasa hivi, Mkuu mambo yangenyoka. Lakini ndiyo basi tena!
 


Hizi shule za kata zimeleta shida...
Yaani hata kuandika kwa ufasaha kwa kiswahili napo shida!

Any ways...ndoho tahabhuuu...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…