Nimevamiwa kwenye plot yangu

Obama wa Bongo

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2012
Posts
5,431
Reaction score
4,925
Habari zenu wana JF
naombeni mnisaidie jambo hili ambalo linanitatiza sana,ili nipate pakuanzia kwani uelewa wangu wa sheria ni mdogo
mwaka 2007 nilinunua kiwanja cha serikali mbweni dsm,pale wizara ya ardhi,wakati huo sikuwa na fedha ya kutosha kwa ajili ya ujenzi.ila nilikuwa na natembelea almost kila mwaka maana niliamini hakuna haja ya mlinzi kwa kuwa nina hati za serikali na kila mwaka ninalipia kodi
sasa mwaka huu nimedunduliza vihela plus mikopo bank nataka kuanza ujenzi(18 months project),nakuta kuna watu 5 pia wameuziwa same plots na watu wasiofahamika ila wote watano hawana hati za kumiliki za serikali kama mimi.yaani wameandikishana tu kwa wanasheria au mahakamani
natayari malumbano yameshaanza ila mm nimewaambia muda wowote naanza ujenzi maana ni na hati wao watajijua,naomba mnisaidie yafuatayo
  1. ninawenza anza ujenzi haraka bila building permit?
  2. je wanaweza kwenda kunizuia kwenye baraza la ardhi?maana nahofia hela zangu nilizokopa zataisha bila kufanya ujenzi
  3. je kama akitokea mtu mwingine na hati kama mimi itakuwaje?
  4. je mimi naweza kuwahi mahakani kuwa zuia?
kuna kampuni maarufu ya udalali nimesikia imehusika katika hayo mauzo ya mmoja ya wamiliki feki almost 70 millions deal!je naweza kuishitaki hiyo kampuni?

wasalaam nawasilisha wana jukwaa.
 
...wewe huna tofauti na Kijana ambaye ana mchumba wake, amekaa anamtizamaaaa, hatangazi tarehe ya kuoa, siku akipata wa kukamilisha ndoto yake na kumtangazia nia, ndo unaanza tapa tapaaaaaa

1. Ukianza kujenga ndo fujo zitaanza (kazungushie uzio wa ukuta, usijenge weka bango lenye maelezo)
2. Toa taarifa serikali ya mtaa/kijiji halafu... polisi..nenda manispaa/wizarani then mahakamani
3. Kiuhalisia hautakaa HAPO kwa amani kutokana na kila mmoja anayekidai ana lake moyoni....tafuta eneo jingine jenga....utakaposhinda kesi...uza
 
sheria za ardhi mbona ziko wazi jamani.... ukimiliki ardhi kwa mda mrefu bila development yoyote serekali ina locus yakukunyanganya ardhi hio.........je kuna maendeleo yoyote ambayo ulifanya?namaanisha hata kuweka b con?au kuweka jiwe lolote la msingi?kumbuka ardhi hapa tanzania ni ya raisi wa jamuhuri anauwezo wakukunyanganya mda wowote akiwa na public intrest na ardhi hio......
 

mkuu kiwanja kimepimwa na kina hati miliki ya jina langu!bcon na pin zote zipo squarea metre 2200 low density.then asilimia kubwa ya viwanja havijaendelezwa eneo hilo mm ndio nataka kuendeleza.
leo mchana nimepitia wizarani bado inaonyesha mimi ndio mmiliki halali
 

Kama wizarani jina ni lako....basi tambua wewe uko salama kwani pale ndio mwisho wa mambo yote. Ila kama ulivyoshauriwa usifikirie kupajenga kwanza kwani zikianza kesi hapa usishangae kikapita kipindi kirefu bila kupewa ruhusa ya kufanya chochote na pengine hata material ya ujenzi kuzuiwa hapo.
 

Asikutishe wao (Ardhi) waliouza hivyo viwanja hawakuweka miundo mbinu km umeme hivyo wewe una haki ya kusubiri kuendeleza hii ndiyo iwe hoja yako kwani tulipouziwa walisema wataweka barabara za lami, maji na umeme ambavyo maeneo mengi havipo. Hao waliouziwa wameliwa kwani ilibidi waende Wizara ya Ardhi kuhakiki, na kama rais angetwaa kiwanja chako basi ilibidi itangazwe ktk gazeti la Serikali. Mimi nakushauri endelea na ujenzi kwani ukuwatapeli wewe hakuna haja ya kusumbua kichwa.
 
Wewe kweli ni Nyati huogopi kitu... Sasa hapo hayo maelezo yako ni sheria ipi unakuwa umetumia?
 
sawa wakuu ila bado nahitaji sana mawazo yenu zaidi
 
zungusha uzio,weka bango ,mtambulishe mkit mtaa, kafanye search 1st floor ardhi then kama jina ni lako kwenye search weka caveat, endelea na ujenzi simultenously na kuomba permit. Openly kiwanja ni chako wahi kabla hakijajengwa itakuwa complicated.
 
Unanafasi kubwa ya kushinda kesi,milki yako haiwezi kubatilishwa kiholela tu utaratibu wa kubatilisha miliki ni mrefu na mgumu mno,ukiona unaendelea kusumbuliwa fungua shauri katika baraza la ardhi la wilaya yako,na kwa ushauri zaid wasilina na wanasheria uaiswe na hofu tunza hati yako kama moyo wako.
 
Tayari huo ni mgogoro wa ardhi. Wafahamu wavamizi wako na ufungue kesi baraza la ardhi na nyumba wilaya. Usijenge utauawa bule na wavamizi. Mtafute mwanasheria akuandikie application na uipeleke kwa pilato. Itachukua muda mrefu shauri kuisha ila utashinda kaka.
 
Ushauri mzuri, tafuta kiwanja kingine ujenge kwani kwa vyovyote vile mgogôro utatumia muda kwani parties tayari ni wengi. Tumia pesa uliyokopa kujenga pengine kesi îkiisha na hakika utashinda maana ulimilikishwa kihalali na mtu haruhisiwi kumnyang'anya mtu hati miliki labda rais na kwa tangazo la serikali. Suala la kufanya developments within 36 months ni agizo la kisheria (kama condition ya kumilikishwa) ila usiogope kwani Tanzania no one cares.
 
zungusha uzio,weka bango ,mtambulishe mkit mtaa, kafanye search 1st floor ardhi then kama jina ni lako kwenye search weka caveat, endelea na ujenzi simultenously na kuomba permit. Openly kiwanja ni chako wahi kabla hakijajengwa itakuwa complicated.

thanx mkuu nilishafanya searching ya mmliki halali last friday pale ardhi bado mm ni miliki halali!niko kwenye process ya kutafuta building permit
 
yawezekana ni kweli ukawa mmiliki halali wa hiyo plot lakini umekuwa ukihold kwa muda gani? na unaimiliki kwa kutumia sheria ipi kati ya deemed right of occupancy na grant right of occunancy..? maana unaweza kuwa na plot ambayo unamiliki kihalali lakini ukashindwa kuindeleza kwa muda mrefu bado serikali na locus ya kuichukua lakinin pia ni vema nikijua kama ulitumiwa notice ya kunyang'anywa hiyo plot..?
 
kwa msada zaidi nitafte mm napatikana open university no yangu ni 0717205888
 
pamoja na kuwa wewe ni mmiliki halali lakini usisahau hapo kuna mtu keshatoa 70m na wengine sijui wametoa kiasi gani. Kumbuka akili ya mtu anayeshawishika kutoa 70m bila kujua kuwa kuna kitu kama kwenda wizarani kuhakiki lazima ni ya chini sana na anaweza kufanya lolote akiangalia mwenye kiwanja (maana anaona ndiye kakichukua) bila kujua kuwa mbaya ni aliyemtapeli. Tumia busara kuchukua tahadhari katika hilo.
Hili ni tatizo lingine kuishi kwenye nchi ya watu tusiopenda kuwajibika na kufikiri.
 
mkuu JERRYone serikali hawajalichuakua ila matapeli ndio wanamefanya hivyo! nimekuwa mmliki tangu 2007 na kuna vitu vingi vilinifanya nishindwe kuanza ujenzi mfano hapakuwa na miundombinu mizuri ya mtui kuishi eneo hilo pia usalama ulikuwa mdogo sana!
 
Last edited by a moderator:
asante mkuu nimechukua taadhari kubwa maana baadhi yao walitaka tukutane nikawaambia kupitia simu kuwa kwanza twende baraza la ardhi kila mtu akiwa na legal document za kumiliki kiwanja cha serikali,sasa hawa wenzangu wanazo hati za kimila walizoandikishana kwa wanasheria wao. so mm nimekataa kuonana nao maana wanaweza kunidhuru wakinipigia simu unaona kabisa hawa watu wamepanic wamegundua wameshatapeliwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…