Kazanazo
JF-Expert Member
- Aug 16, 2023
- 2,582
- 4,554
Kwemah wakuu,,,tunapeana tu motisha na kuongeza mapambano ya kila siku hasa kwa wadundulizaji kama mimi
Iko hivi, nilipomaliza chuo niliingia zangu kitaa na idea ya kuuza vifaa vya simu na tigo pesa ambayo nilikuwa naifanya toka nikiwa chuoni hasa tukifunga chuo au nikiwa mwanzoni mwa semester hiyo ilikuwa 2019
Wakati naanza kazi ilikuwa ngumu sana kwa siku wateja hawazidi kumi na wakija wanakuja wale walioshindwa na madoni wa mtaa yaani wanataka kutuma au kutoa mpunga mkubwa ambao sikua nao na biashara ya accessories ilikuwa haisogei kabisa
Changamoto kubwa ilikuwa majungu ya wateja na maneno yao ya kukatisha tamaa mara wakwambie kama huna si ufunge mara wakuchane live kuwa hapa hutoboi fulani ndio kila kitu na ukizingatia sikuwa na mtaji wa maana lakini niliendelea kupambana kwani sikuwa na idea ya biashara nyingine hata kama kamisheni ilikuwa ndogo sana kipindi kile bado niliendelea kupambana
Hadi kufika muda huu ni takriban miaka 5 nashukuru Mungu kijiwe kimechangamka wakati mwingine unashindwa kupata hata muda wa kula kwa ubize, cha kushangaza ni kuwa walewale waliokuwa wakinikatisha tamaa ndio marafiki zangu na wateja wangu wakubwa
Huwa wakija watapiga stori za mawakala wengine na kukupa umbea mwingi na uongo sijui wamefirisika, walikuwa na pesa za mkopo n.k lakini kwakuwa naijua biashara huwa siwasapoti kiviile zaidi ya kuwaitikia na kutabasam kama vile nawasapoti ilimradi kazi inaenda safi
Mwisho, kwa experience yangu ndogo ya miaka mitano nimegundua biashara yoyote changa inapitia hatua nyingi sana hadi kuimarika kabisa inaweza chukua miaka hadi 10 au 20 kuwa doni wa mtaa kwa hiyo vijana tusikate tamaa hasa kama umeamua kuwa upande wa biashara wakati wetu uwaja
Ahsanteni