Nimevumilia muda mrefu sasa nakaribia kuuteka mtaa hamasa kwa wanaoanza biashara

Hongera mkuu na hayo ni matokeo ya kuamini kile unachokifanya bila kukata tamaa. Focus yako kwenye mipango yako inakulipa sasa, ungekubali kuyumbishwa na wayasemayo leo hii ingekuwa majuto.
 
Hongera sana Mkuu, naamin ukiachana na ofisi yako bado unaendelea zaid kujitanua (kuongeza assets)
Hapana mkuu kwa sasa focus yangu ni kuweza kuwa accommodate wateja nilionao ifike kipindi nisikose hata muamala kisa eti sina cash au float nikishafika level hiyo ndio nitafikilia kuongeza kitengo kingine
 
Hongera mkuu na hayo ni matokeo ya kuamini kile unachokifanya bila kukata tamaa. Focus yako kwenye mipango yako inakulipa sasa, ungekubali kuyumbishwa na wayasemayo leo hii ingekuwa majuto.
Ahsante mkuu, hakika biashara inahitaji uvumilivu wa hali ya juu na kutokukata tamaa kwani upepo muda wowote unaweza badilika ukaanza kupata matumaini

Tupambane tusikate tamaa siku moja tutatoboa tu
 
sahihi kabisa
 
Na hayo ndio malengo yangu, ila nataka nitafute capital ya kutosha kwa income yangu sitaki kuingia chocho za depts najua safari itakuwa ndefu sana ila nitaifikia inshallah
Nieleweshe kuhusu super agent Mkuu
 
Wanaitwa mawakala wakuu ambao wakala wa kawaida anaenda kuweka au kutoa float kwake
Hivi mawakala wakuu profit ratio yao ktk kamisheni kwa muamala mmoja inalingana na mawakala wa kawaida? na je super agent pia anaweza akafanya na miamala ya kawaida?
 
Hapana mkuu kwa sasa focus yangu ni kuweza kuwa accommodate wateja nilionao ifike kipindi nisikose hata muamala kisa eti sina cash au float nikishafika level hiyo ndio nitafikilia kuongeza kitengo kingine
Ni vizuri lakini kuna kanuni moja inasema usiweke mayai yote kwenye kapu moja.

Siku nikitulia nitaeleza kisa changu chote mpak kufikia level nilizopo sasa hivi... Binadamu ni watu wabaya sana wenye roho za kichawi na husda hasa ukifanikiwa mbele ya macho yao.
 
Ushauri mzuri nasubiri kisa nipate kujifunza
 
Tupe mkuu hicho kisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…