Nina rafiki ambae nilisoma nae primary mpaka secondary miaka ya nyuma, Nilibahatika kuonana nae town miaka 2 ilopita, akani introduce kwa mkewe.
Jamaa alikua anapenda kuja kwangu, hua tunaenda kuangalia mpira, na mara nyingine kwa mambo ya ki business. Mara nyingi huwa namwambia arudi home mapema ili shemeji asiudhike. Jamaa alikua akilalamika kua mke wake ana wivu sana na mkorofi. Nilimjibu kua huyo ni mke mzuri na anampenda ndo maana yuko hivyo na nilimu heshimu sana shemeji.
Siku 1 mkewe alinipigia simu akinishutumu kua mimi namuharibu mumewe kwa kumpeleka kwa wanawake na toka amejuana na mimi amebadilika na akanitukana sana.
Nikaongea na jamaa kuwaa tusiwe tunawasiliana na mara nyingi, akinifata nilijaribu sana kumkwepa. Pamoja na jitihada zangu zote, mkewe kila siku alikua akinitumia meseji za kunitukana, nikaona isiwe taabu kwa kuwa jamaa alikua ni mtu wa kunisikiliza sana nikampeleka sehemu kumkutanisha na mtoto wa kitanga.
Jamaa baada ya kupewa mambo kanogewa, hivi sasa kampangishia nyumba Mikocheni na ana process harusi. Nikamshauri aachane na huyo mke mkorofi na kweli amempa talaka na kumrudisha kwao, na huko wana maisha magumu anapata shida namuonea huruma lakini ndo hivyo amejitakia
Fundisho kwa walioolewa:
Msiwe mnawafikiria vibaya marafiki wa waume zenu. Waheshimuni.