'Nimevurugwa', Video Ya Snura Yapigwa Marufuku, BASATA Washindwa Kustahimili Mauno

'Nimevurugwa', Video Ya Snura Yapigwa Marufuku, BASATA Washindwa Kustahimili Mauno

Ibrahim300

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2010
Posts
390
Reaction score
68
Staa wa nyimbo za kibongo ambaye pia anatamaniwa na waume wengi, Snura a.k.a Mamaa Majanga amewaudhi Baraza la Sanaa la Taifa kwa video yake ya Nimevurugwa, jambo ambalo limewafanya kupiga marufuku nyimbo hiyo kutochezwa katika runinga za Tanzania.

Kisa na sababu ni kuwa video hiyo imekosa maadili na vigezo katika jamii.

Akizungumza hivi karibuni, Snura alisema hajui ni sababu gani iliyofanya kazi yake kufungiwa kupigwa katika vituo vya televisheni.
"Nilipigiwa simu na rafiki zangu na kuambiwa hivyo, lakini mpaka sasa sijui ni kwa sababu gani maana sioni kama nimefanya kitu cha ajabu katika video hiyo na cha kushangaza hata sijaulizwa na yeyote, ila ndiyo hivyo," alisema Snura kwa mishangao.

Snura aliongezea kuwa wakati alipofanya nyimbo ya Majanga alipoteza mashabiki wengi kwa kuwa hakucheza soo wakati huu alipocheza katika video yake ya Nimevurugwa kumbe ilikuwa kama kujikolea makaa ya moto.

Stori imedondoshwa kutoka bkuHABARI Blog
 
Kwa style hii tutegemee hata nje ya boks ya joh makini na yenyewe piakufungiwa
 
Wanafanya hivi kwa nyimbo za kibongo tu au mpaka za nje??😕

Waangalie upya kuna Nyimbo nyingi sana zinatakiwa zisichezwe..

Hata wanaume kuvaa hereni..Mlegezo..Ni nje ya maadili..Fungiaaaa..

Wanawake kuvaa nusu uchi... Fungiaaa...
 
Wabongo wanajifanyaga wanaishi peponi,wakati "ukwu" wanaangalia na yale manyimbo mengine ya Nigeria

Tuache watu wafanye mziki na sio kuwakalia kooni wasanii.

Mbona nyimbo ya Ride ya Ciara haikufungiwa kwenye nchi nyingine zaidi ya kupangiwa muda wa kupigwa kwenye vituo vya television
 
kiukweli haikua na maadili kabisa, af alinikera na idea ya kuweka wanafunzi mle ndani
 
Saafiiii....wanatukatia mauno mpk unaona aibu kuangalia na wazee wako...ya ulaya ya ulaya...msituharibie watoto na njaa zenu
 
Anakatika mno style za chumbani,anaemfungiaa na apigweeee
 
SNURA na SHILOLE
.
Naomba wote wafungiwe pleaz
.
 
kuvurugwa ni majanga matupu....me nashangaa snura akikata tamaa watu hawaongei ila akikata mauno ..ni hataree tupu ni shiidaah..
 
Kalewa sifa za mashbika hadi kasahau maadili.

Fungia tu.
 
Back
Top Bottom