Ibrahim300
JF-Expert Member
- Nov 29, 2010
- 390
- 68
Staa wa nyimbo za kibongo ambaye pia anatamaniwa na waume wengi, Snura a.k.a Mamaa Majanga amewaudhi Baraza la Sanaa la Taifa kwa video yake ya Nimevurugwa, jambo ambalo limewafanya kupiga marufuku nyimbo hiyo kutochezwa katika runinga za Tanzania.
Kisa na sababu ni kuwa video hiyo imekosa maadili na vigezo katika jamii.
Akizungumza hivi karibuni, Snura alisema hajui ni sababu gani iliyofanya kazi yake kufungiwa kupigwa katika vituo vya televisheni.
"Nilipigiwa simu na rafiki zangu na kuambiwa hivyo, lakini mpaka sasa sijui ni kwa sababu gani maana sioni kama nimefanya kitu cha ajabu katika video hiyo na cha kushangaza hata sijaulizwa na yeyote, ila ndiyo hivyo," alisema Snura kwa mishangao.
Snura aliongezea kuwa wakati alipofanya nyimbo ya Majanga alipoteza mashabiki wengi kwa kuwa hakucheza soo wakati huu alipocheza katika video yake ya Nimevurugwa kumbe ilikuwa kama kujikolea makaa ya moto.
Stori imedondoshwa kutoka bkuHABARI Blog