Nimewagomea Wanafamilia tusichangie Harusi ya Kaka bali tuchangie mdogo wetu masomo na Nyumba tumalizie. Wamefura nimelikoroga

Nimewagomea Wanafamilia tusichangie Harusi ya Kaka bali tuchangie mdogo wetu masomo na Nyumba tumalizie. Wamefura nimelikoroga

Bush Dokta

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2023
Posts
24,831
Reaction score
45,154
Kama mnavyojua ndugu zangu sisi ni wanyong mpaka pale sisiemu itakapotoka madarakani.

Hivyo maisha yetu ni ya kuunga unga na kusaidian ili siku zisonge.

Na mtu pekee wa kukuinua ni mwanafamilia mwenzako Dada au Kaka.

Mimi nilimaliza masomo baada ya kuhangaikiwa sana na Dada yangu na Kaka Yangu waliokuwa wanafanya kazi za Ndani.

Hatimaye nikayakwaa majiwe kadhaa ya Elimu.

Baada ya kuyakwaa majiwe ikabidi na mimi nianze sasa kuinua waliobaki nyuma. Ila sasa maji yamezidi Unga. Nahitaji msada. Hivi kwa Tanzania hii unaweza kusomesha watu watano kwa mpigo vyuoni?

Basi tukasonga mbele kama familia hatimaye tukainuka, sasa watu kadhaa wana vipato vizuri tu. Alhamdullilah.

Tuna kesi tatu kwa pamoja.
1. Dogo yuko chuo anasoma.

2. Nyumba imejwngwa bado finishing.

3. Kaka anafunga ndoa.

Mimi kwenye kikao cha wanafamilia nimewambia hizi fedha badala ya kuchangia harusi tuchange kwa ajili ya Dogo masomoni na Tumalizie nyumba ya familia (Family house kwa maana ya family house).

Wamefura.

Hii imenishangaza ni sawa na washkaji zangu unakuta anachangia harudi laki tatu huku Mama yake kijijini anaumwa anamtumia elfu 20.
Wafrika tubadilike. Maendeleo ni sisi wenyewe.
 
Hahahaha

1000012500.gif
 
Mi Niko upande wako sana tuu ila.

Changamoto ni pale mnapoitwa Kwa Agenda ya Harusi harafu wewe unaongelea mambo ya ada ya dogo.

Mentality ya waafrica wengi huchukulia Harusi kuwa ni jambo la siku Moja halitarudia hivyo hulisheherekea Kwa mkazo wake.

Binafsi nakushauri fanikisheni ndoa ya kaka aoe isije wajengea mgawanyiko wa kifamilia... Hayo mengine pia yafanyike.

With 🙏; mtwa mkulu
 
Mwambie aache kusumbua watu aandae tsh M3 siku ya harusi mkitoka kanisani mnaenda familia na watu wa karibu wachache kupata chakula cha jioni heavy hotel flan cool na picha za hapa na pale kama kumbukumbu.

Maisha yanasonga mambo ya kuomba omba mchango na kutaka sherehe yako waje watu hata usio wajua binafsi siifagilii sana....
 
Mi Niko upande wako sana tuu ila....
Changamoto ni pale mnapoitwa Kwa Agenda ya Harusi harafu wewe unaongelea mambo ya ada ya dogo.
Mentality ya waafrica wengi huchukulia Harusi kuwa ni jambo la siku Moja halitarudia hivyo hulisheherekea Kwa mkazo wake.
Binafsi nakushauri fanikisheni ndoa ya kaka aoe isije wajengea mgawanyiko wa kifamilia... Hayo mengine pia yafanyike.
With 🙏; mtwa mkulu
Sawa mkuu umeshauri vizuri.
Kumbuka huyu bro huwa hachangii mambo ya familia kwa nini sisi tupoteze kwa ajili yake?
 
Mwambie aache kusumbua watu aandae tsh M3 siku ya harusi mkitoka kanisani mnaenda familia na watu wa karibu wachache kupata chakula cha jioni heavy hotel flan cool na picha za hapa na pale kama kumbukumbu .....maisha yanasonga mambo ya kuomba omba mchango na kutaka sherehe yako waje watu hata usio wajua binafsi siifagilii sana....
Well. Watu wabadilike kwa kweli.

Tuwachie masherekhe makubwa watu wa middle income na Wale wanaokula kwa urefu wa kamba zao. Sisi tusitake maajabu
 
Inaonekana familia Yako inapenda sana sherehee kuliko maendeleo ya kifamilia kiujumlaa..

Sasa ww nenda wanavyotaka na baada ya hapo kausha watujua watapata wapi ada ya dogo
 
Inaonekana familia Yako inapenda sana sherehee kuliko maendeleo ya kifamilia kiujumlaa..

Sasa ww nenda wanavyotaka na baada ya hapo kausha watujua watapata wapi ada ya dogo
Sawa ila mimi nimewaeleza kwa uzuri tu bila ugomvi. Wasije wakasema mbona hukusema
 
Back
Top Bottom