Nimewagomea Wanafamilia tusichangie Harusi ya Kaka bali tuchangie mdogo wetu masomo na Nyumba tumalizie. Wamefura nimelikoroga

Jamaa alitoka zake Marekani, yeye na mchumba wake (Wabongo).

Kawaletea Wabongo mambo yake ya Kimarekani huko.Alifikiri anawamudu Wabongo.

Basi wee, mwenyewe akajua hajui 😂😂
Hahahaaaa......wanampopoa mpaka anakoma.

Sisi maskini ni hatari sana.kwa mdomo tu hatujambo
 
Hongera mkuu. Most mature decision.
 
Hii imenishangaza ni sawa na washkaji zangu unakuta anachangia harudi laki tatu huku Mama yake kijijini anaumwa anamtumia elfu 20.
Wafrika tubadilike. Maendeleo ni sisi wenyewe.
Sikuhizi wamebadirisha kile kiitikio hawasemi tena "Sisi sio Milima" bali wanasema "Sisi ni Ndugu" tutakutana yaan litakukuta na Wewe watasema hio Pesa ya michango wakajengee kaburi la Babu yenu huko Dumila, Dunia kichaka njoo tuchome nyingine
 
Michango michango mingi ni dalili ya umasikini na kuuendekeza umasikini.
 
Kwasababu umesema mko kadhaa mna kipato kizuri sioni shida inatoka wapi kuchangishana ili mkamilishe yote matatu.
1. Masomo ni on going process
2. Nyumba pia ni long term process.
3. Marriage can be planned.
Changishaneni mtimize yote matatu ili wote muwe na furaha.
 
Huwa inanishangaza mno mno mno.ugonjwa hawatachanga.....masomo kuinuana kimitaji ila waambie harusi...
 
Mwambie afunge kwanza
ndoa af sherehe ya harusi watafanya tu baadae mambo yakijipa au at least mkishapunguza punguza majukumu.

Wanavaa vizuri kanzu safi, Shela ya kukodi kalii, make up haksool na Vipiko piko nini bas hapo mchawi iphone tuu. Mnapiga picha kalii mnapost ushahidi bas shuuli imeisha.
Kwenye msosi sio lazima mpike mavitu mengii. Pilau nyama salad tikiti na soda ni standard kabisa.
Mbona watu wengi tu wanafanya hivo especially waislam kwasab kinachohalalisha tendo ni ndoa mnayofunga pale msikitini/nyumbani kwa binti, sherehe ni mbwembwe tu tena kiuhalisia kabisa huwa ni showoff isokuwa na maana.
 
Mkuu sawa. Lakini mamisha yana mambo mengi. Ndio maana hata matajiri wana pesa nyingi lakini hawawezi kufanya mambo yote kwa pamoja. Lazima Priority one after another.
 
Huwa inanishangaza mno mno mno.ugonjwa hawatachanga.....masomo kuinuana kimitaji ila waambie harusi...
Noma sana.

Mgonjwa hawachangui ila akifa atasafirishwa kutoka Dar kwenda Songea milioni 10. Mgonjwa kafa kwa kukosa milioni mbili.
 
Reactions: Lax
Hapo wanataka kuchoma millions inaelekea hawataki a simple wedding....siyo kwamba hataki ndoa ifanyike but iwe simple tu....
 
Mkuu sawa. Lakini mamisha yana mambo mengi. Ndio maana hata matajiri wana pesa nyingi lakini hawawezi kufanya mambo yote kwa pamoja. Lazima Priority one after another.
Nimeainisha hapo. Shule mtoto hasomi kwa kulipiwa hela yote ni term kwa term kwa miaka yote anayosoma. Pia nyumba inajengwa step by step. Ndoa mnapanga. Yote yanawezekana kufanyikq mkiamua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…