Uchaguzi 2020 Nimewasikiliza walimu fulani, aisee! CCM haina chake kwao

Superbug

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2018
Posts
13,864
Reaction score
35,079
Jana jioni nilikuwa naongea na walimu fulani aisee CCM imepoteza kwao. Nilijaribu kujifanya Mimi ni mwanaCCM nikaimba ngojera ya stiglaz standadgeji vivuko uchumi wa kati flyova nk.

Majibu yao yalikuwa haya.

Miaka miwili nyuma waliongezwa shilingi (5000-7000) kwenye mishahara yao.sijui ni mwaka gani. Mwaka huu wameongezwa (tsh 30,000-50,000) kwa muda wa miaka mitano wameongezwa wastani wa tsh 30,000 kitu ambacho Ni kinyume na sheria kabisa.

Wakaongeza kuhusu kutolipwa stahiki zao ambazo zilitokana na kupanda madaraja enzi za JK . Waliongezwa madhila wanayoyapata kutokana na makato ya bodi ambapo inawasababisha kwenda kukopa kea wakopeshaji umiza ambao wengi wao ni watu wa musoma.

Walimu wengi wameweka kadi za benk rehani ili wapate mikopo dhalili hii yote kea mujibu wao adui Yao namba moja ni CCM.

Rais mwalimu
Mke wa rais mwalimu
Waziri mkuu mwalimu

Ila hawajawasaidia.

Poleni walimu wangu Mungu atawafuta machozi.
 
Na sio walimu tu, hii awamu imesababisha maumivu kwa makundi mengi kwenye jamii, wajiandae kwenye kampeni watu hawataki story za bombardier wakati hawajui hata kula yao ya siku ikoje kwasababu ya sera zao mbovu za uchumi.
 
Makundi ni mengi sana wakiwemo Wastaafu, vijana wahitimu wasio na ajira, wafanyabiashara, watumishi wengine wa umma nk.
 
Hakuna watu wanao waangusha wapiga kura kama walimu.. Mimi nadhani wamelogwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…