Basi bila shaka umenielewa. Asante
TEHAMA = ICT
Ha ha ha ha aiseeee. Kuna haja ya kufuatilia sana watu wanapataje ajira serikalini, sasa kama mtu anashindwa kutofautisha neno taarifa na Habari, tunachangamoto sana.
Habari ni aina ya taarifa iliyo kamilika na yenye chanzo na tamati kuhusu tukio fulani.
Kila habari ni taarifa ila sio kila taarifa ni habari. Neno taarifa ni mkusanyiko wa chembe au elementi za ufahamu kuhusu tukio lolote.
Daktari anapokupima kipindi ukiumwa, anachukua sampo ya damu yako ikiwa ni mojawapo ya kiambishi fizikia chenye chembe zitazobeba taarifa kuhusu hali yako kiafya. Akisha peleka maabara na kupima damu akajua kisababishi cha wewe kuumwa kutokana na taarifa iliyobebwa na damu yako then ataandaa habari kukupasha unasumbuliwa nini na tiba yako nini.
Huyo mtu m'moja kutokana na ufahamu wake mdogo juu ya matumizi ya misamiati sahihi ya lugha ya kiswahili katika kutafasiri neno la kiingereza information, amewamislead watumiaji wa haya maneno bila kujua au kwa makusudi.
Neno tehama linaweza kuwa sahihi kama matumizi yake ambayo yamekusudiwa na taasisi husika. Ila haimaanishi kuwa ni definition au Abbreviation ya neno ICT.
So, neno Taarifa kwa English ni Information. Neno habari unaweza tumia neno News labda.