Nimewaza Ujinga: Kwanini magari yasigome kuwaka mpaka dereva atakapochomeka leseni yake na funguo kwa pamoja?

Nimewaza Ujinga: Kwanini magari yasigome kuwaka mpaka dereva atakapochomeka leseni yake na funguo kwa pamoja?

Hilo linawezekana ila tu jua Kila project lazima tuangalie kwanza economic view point kabla haijawa implemented yani safety then Economic sasa upande wa Safety iko ok ila tu hapo kwenye economic ndio pamekwamisha japo sijafanya feasibility study juu ya wazo lako ila kwa maono yangu tu ili Gari iwasiliane na server za polisi sijui wapi inahitaji INTERNET, Swali je coverage ya internet nchini imetapakaa kote?
 
Asante sana kaka mkubwa. Ungetoa ufafanuzi kidogo ili wadau wengine wa hapa JF wafahamu pia hizo hasara.
Faida.
1. Kila gari itaendeshwa na mwenye leseni.
2. TRA watakusanya mapato on time kwa 100%
3. Rahisi kufuatilia matukio kama wizi na history ya gari katika kuendeshwa kwake.

Hasara.
1. Sehemu isiyokuwa na network lazima gari litazima na hakuna tena kuondoka.
2. Gharama kubwa itatumika endapo utaamua kuwa katika mfumo huo.
3. Running Cost ni kubwa sana katika kufuatilia magari nchi nzima.
4. Gari zote lazima zifungwe mfumo huo.
5. Kitengo cha customer service kiongezewe watu.
6. Nk
 
We waza tu hivyo halafu siku unashida ama unamgonjwa ushindwe kumpeleka kisa leseni!! Hizo gari zitakuwa na limitation ya ajabu!.. Bora ibaki funguo tu kuwa ndo lock ya gari kuliko na mileseni yakikupata ya kukupata ndo utaelewa.
 
Mbona kuna baadhi ya gari zinafungwa mpaka GPS? Hii inakuwa ni sehemu ya gharama ya registration ya chombo cha usafiri.
Naona unalizimisha sana wazo lako tulikubali.

Hata hivyo unapoleta wazo kama mradi lazima utuelezee faida na hasara zake. Wewe umeelezea faida tu. Sasa naomba ueleze hasara zake.
 
Kuna sehemu niliwahi fanya kazi nikakuta gari zao ili ziwake lazima ubadge kwanza kisha ndiyo uweke funguo.

Monitoring system yao watakuwa wanafahamu ni nani anayeitumia gari muda huo au orodha kamili ya walioitumia hiyo gari.

Na kwenye issue ya usalama inasaidia kiasi kwani kwa wizi wasio na ufahamu mpana watashindwa kuiba hiyo gari (wale wezi wa kufunja ignition switch na kuunganisha nyaya kisha kusepa na gari) ila kwa wezi watabe hawatasumbuka hata kidogo mfano mzuri ni hizi gari zenye funguo ulio na transponder (immobilizer system) hapa wezi walichemka kiasi baadae wakaanza kuziiba tu kama kawaida.
 
Hata hivyo unapoleta wazo kama mradi lazima utuelezee faida na hasara zake. Wewe umeelezea faida tu. Sasa naomba ueleze hasara zake.
Changamoto labda ni network coverage kwa sehemu za vijijini.
 
Back
Top Bottom