Nimewekeza kwenye mitiki inalipa, karibu tuwekeze

Dah, am so lucky. Ntakupigia ili unisaidie ujuzi wa kulima miti hiyo. Nina kama heka kumi hivi ziko Mang'ula. Nataka nianze na moja ili nipate uzoefu. Kwa sasa shamba hili nalima Mpunga tu.
Karibu sana mkuu
Kama shamba linatumika kwa sasa, kwa mazingira ya huko baada ya kilimo cha mpunga hua ni kiangazi.. hivyo sio rahisi miti kuota labda uwe na chanzo cha umwagiliaji maana mitiki inahitaji maji ya kutosha..
Kama hakuna chanzo cha maji tofauti na mvua, ningekushauri upande kwenye mvua za vuli za November.

Karibu
 
Jambo zuri sana hili
vp kwa tuliopo mikoani unaweza kunitumia mbegu?
 
noted
 
Kazi nzuri. Je, inachukua miaka mingapi kuvunwa Mbao? Je, maeneo ya milimani inaweza ikasktawi? Soko lake likoje ?
 
Kazi nzuri. Je, inachukua miaka mingapi kuvunwa Mbao? Je, maeneo ya milimani inaweza ikasktawi? Soko lake likoje ?
Kuvunwa ni miaka 15-20, kutegemeana na eneo kwa maeneo mengine hata zaidi ya hapo,...
Maeneo ya miliman yakiwa na maji ya kutosha inastawi vizur sana..
Mitiki inahitajika sana sokoni na ni miti yenye thamani kubwa sana kutokana na matumizi yake kuwa mengi.. ukiwa na shamba kubwa unaweza kuunganisha ukauza nje ndiko kwenye bei nzuri zaid
 
Dah, am so lucky. Ntakupigia ili unisaidie ujuzi wa kulima miti hiyo. Nina kama heka kumi hivi ziko Mang'ula. Nataka nianze na moja ili nipate uzoefu. Kwa sasa shamba hili nalima Mpunga tu.
mI NAHITAJI SHAMBA HUKO MANG'ULA
 
de pedezyee mimi nimelima mitiki kwa ajili ya kulinda shamba langu, kilimo cha kila mwaka kilikuwa kinaniumiza kichwa tu hivyo ili kulinda shamba kwa kizazi kijacho nikaamua kupanda hii miti. Ila ki ukweli sijui thamani yake zaidi ya kuambiwa maneno ya mtaani tu kuwa ina thamani kubwa.

Mwenye figure za thamani hasa ya hii miti anasaidie au wapi naweza kupata taarifa sahihi. Miti ina miaka miwili, ukubwa wa shamba ni 10 eka.
 
Bei zinatofautiana kulingana na aina ya soko.. nikimaanisha kuna soko la ndani na soko la nje, mara nyingi mkulima anakua hapati faida kubwa kutokana na kuruhusu watu wa kati (madalali) kwenye biashara. Hiyo inapelekea dalali kupata pesa nyingi kuliko hata mkulima aliyeangaika nayo,

Nitarudi kukupa mchanganuo wa bei za mitiki kwa kiwango cha juu na kiwango cha chini, lakini pia namna ya kufanya ili uuze kwa bei sahihi
 
de pedezyee nitashukuru ndugu, unaweza kuwa na mali ila hata thamani yake halisi hatujui. Ukirudi tena ni tag au ni quote ili nipate notification ya post yako.
 
Mitiki unavuna baada ya muda gani... kuna maeneo mazuri ya kununua uko ili kuuilima... bei inaendaje kwa heka.. Faida baada ya kuitunza kwa heka unaeza pata shilingi ngapi...? asante boss
 
de pedezyee nitashukuru ndugu, unaweza kuwa na mali ila hata thamani yake halisi hatujui. Ukirudi tena ni tag au ni quote ili nipate notification ya post yako.
Kwenye soko la mitiki hakuna bodi ya kucontrol bei, hivyo bei inakua ni makubaliano ya muuzaji na mnunuzi kwa kipindi kilichopo,

Kwa sasa kama una shamba lenye miti iliyokomaa kwa kuuzwa unaweza kutumia namba zangu hapo juu nikakuinganisha na wanunuzi moja kwa moja
 
Mitiki unavuna baada ya muda gani... kuna maeneo mazuri ya kununua uko ili kuuilima... bei inaendaje kwa heka.. Faida baada ya kuitunza kwa heka unaeza pata shilingi ngapi...? asante boss
Inavunwa baada ya miaka 15 had 20, mchanganuo wa bei pitia post za juu kwenye uzi huu
 
Maeneo sina uhakika sana, kwa sababu ni mashamba ya muda mrefu, unaweza kuangalia maeneo mengine yenye ardhi mpya ni mazur zaidi maana unaweza kupata kwa gharama nafuu
 
Ndugu hakuna usiri wala aibu ya kuweka bei wazi hapa kama una connection, mbona bei ya miche umeweka hapa, kama unajua bei ya soko pia weka kusaidia wengi zaidi.
 
Ndugu hakuna usiri wala aibu ya kuweka bei wazi hapa kama una connection, mbona bei ya miche umeweka hapa, kama unajua bei ya soko pia weka kusaidia wengi zaidi.
Hapana mkuu mimi ninahusika na miche tu, sio mnunuzi wa mitiki, ila baada ya kuulizwa na watu wengi ikabidi nifatilie..

Sijabahatika kujua exactly figure, ila baadhi ya wanunuzi wameniambia wapo interested sana na watu wanaotaka kuuza miti kwa sasa huku bei wakisema ni makubaliano yao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…