Nimewekeza kwenye mitiki inalipa, karibu tuwekeze

Hongera sana kwamoyo huo wa ukarimu , ni jambo jema kumsaidia mtu bila kujali unamfahamu au humfahamu....
Siku kila mmoja atakapoweka avatar ya picha yake ya kweli kutakuwa na vioja, manake wengi humu mitandaoni "wanakula ugali kwa picha ya samaki"
Kuna wengine visu zaidi ya avatari zenyewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilisikia hii habari ya mitiki sikujua kama ni kweli hebu fafanua mkuu faida ikojekwa mfano ukiwa na eka 5 baadaya miaka kumi ni sh ngapi waeza earn?

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Maeneo ya Bagamoyo unaweza kupanda hii miti?
 
Ila nikuulize swali mkuu unalimia wapi hii kitu, na hujaweka mchanganuo wa Gharama hata heka 1 tuu

Sent using Jamii Forums mobile app
Shamba langu lipo morogoro,
Ekari moja unapanda miche 529 kwa maana ya 3x3
Hivyo itagharimu sh. 159000/=
Hiyo ikiwa ni gharama za miche pekee, upandaji unategemeana na watu utakaokubaliana nao, lakini watu wetu wanapanda kwa sh 200/mche kwahyo itakua sh.106000/=

Kwahyo jumla upandaji na gharama ya miche inakua sh. 265000 kwa ekari moja.

NB. Gharama za miche zinajumuisha na usafirishaji kwa mikoa ya dar pwan na morogoro, had kufika kwenye vituo vikubwa na sio shambani
 
Reactions: PYD
Nilisikia hii habari ya mitiki sikujua kama ni kweli hebu fafanua mkuu faida ikojekwa mfano ukiwa na eka 5 baadaya miaka kumi ni sh ngapi waeza earn?

Sent using Jamii Forums mobile app
Hii itategemea na aina ya soko unalolikusudia, nitakuelekeza soko la nje ambalo ndio zuri na utapata faida kubwa.

Mti wa miaka 15-20 unakua ni bora na una thamani zaid sokoni.
1cubic metre inafika hadi usd 1500 ukifika sokon kwa soko la india, hivyo kama utatoa gharama za usafirishaji na vibali ili upate ni kiasi gani utabaki nacho,

Shamba la ekari moja baada ya kupunguza miti unaweza kuvuna hadi miti 300,
 
Mashamba yake unaweza kupanda mikoa gan broo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inahitaji maji ya kutosha, kama mikoa ya morogoro, pwani, tanga, kilimanjaro pia, lindi na mtwara pamoja na maeneo jiran na hayo yenye mvua za kutosha,.. sina uhakika na maeneo mengine lakini watu wanima maeneo mengi lakini inaweza kuwa na changamoto kwenye ukuaji.
 
Sasa kinacholipa hapa ni mitiki au alizeti na asali?
 
Umelima kama eka ngapi na kutokana na eka ulizoanza nazo ulianza na mtaji kiasi gani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu mi nataka kujua hii miti inakubali maeneo ya kanda ya nyanda za juu kusini, kwa maana ya Mbeya, Rukwa, Songwe na Katavi.

Pia nahitaji kujua gharama ya kuhudumia miti (pruning, usafi n.k) kwa heka, pia inaweza kuchukua mpaka miaka mingapi.?
 
Mkuu mi nataka kujua hii miti inakubali maeneo ya kanda ya nyanda za juu kusini, kwa maana ya Mbeya, Rukwa, Songwe na Katavi.

Pia nahitaji kujua gharama ya kuhudumia miti (pruning, usafi n.k) kwa heka, pia inaweza kuchukua mpaka miaka mingapi.?
Kuvuna ni miaka 15-20.
Prooning inafanywa mara nyingi ili mti uweze kunyooka vizuri na mbao zisiwe na vidonda. ( hivyo siwezi kukuambia gharama halisi ).
Pia kuna thinning hii ni kupunguza idadi ya miti shambani ili iweze kunenepa.
Thinning inafanya kulingana na mahitaji (miti inayopunguzwa hutumika kama mirunda). Unashauriwa kufanyq thinning miti ikiwa na miaka 3-5.
Kwa maeneo ya nyanda za juu kusini sijawahi kufanyia kazi
 
Shukran sana Bro

Ipo siku nitakutafuta kwa ushauri zaidi in sha Allah
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…