Li ngunda ngali
JF-Expert Member
- Jun 22, 2023
- 707
- 2,572
Niliharibikiwa na gari tokea mchana Kijiji kimoja karibu na Makambako huku Nyanda za juu Kusini.
Sasa ndugu zangu, eneo nililopata hiyo breakdown lipo Duka kubwa na mara ya kwanza nilipoenda kununua kinywaji nikahudumiwa na binti mmoja mkali! Kama kawaida ya sisi wa ki-ume, nikameza mate ndugu yenu.
Kisa; nimerejea kwa mara ya pili kununua super glue na ndipo nilipomuuliza kama yupo huru ili nigombee Jimbo. Binti kajibu yupo kwenye mahusiano japokuwa siyo ki vilee.
Bwana bwana, kumbe binti yule ni mke wa jamaa mwenye hilo Duka na wakati ana nijibu hilo swali, Mwamba kumbe alikuwa Store na alisikia. Hatari!
Ghafla nikaona mtu anamfuata yule binti kwa ghadhabu iliyo kuu na kuanza kumpiga makofi ya nguvu. Nami nikachoropoka mle ndani.
Sasa, gari imeharibika jirani na Duka, na jamaa namuona tokea muda akiranda-randa na anatambua mimi ndiye mwenye hiyo gari.
Nifanyeje ndugu zanguni?!