Nimeyakanyaga mwezenu nimekutana na mke wa mtu katika harakati za kutaka kutogoza mumeo kasikia yote!

Shida vijana mnajikuta vichwa vidogo vina macho kila unachoona unatamani 🤣🤣Tuambie kabisa msiba wako utakua wapi tuje kufinya mpunga
 
Si upige Simu kwa mwenyekiti wa CCM alimalize hili unakwama wapi ndugu yangu
 
Kiingereza unaiandikaje hii Madam Hannah ?

Nakumiss 😃😃😃
Wewe ile siku niliomba unifundishe ile kitu namna ya kutumia ukaniambia niiulize google sio….. Likewise Manyanza.

Hahahah haya asante kwa kunimiss😂
 
Niliharibikiwa na gari tokea mchana Kijiji kimoja karibu na Makambako huku Nyanda za juu Kusini.

Sasa ndugu zangu, eneo nililopata hiyo breakdown lipo Duka kubwa na mara ya kwanza nilipoenda kununua kinywaji nikahudumiwa na binti mmoja mkali! Kama kawaida ya sisi wa ki-ume, nikameza mate ndugu yenu.

Kisa; nimerejea kwa mara ya pili kununua super glue na ndipo nilipomuuliza kama yupo huru ili nigombee Jimbo. Binti kajibu yupo kwenye mahusiano japokuwa siyo ki vilee.

Bwana bwana, kumbe binti yule ni mke wa jamaa mwenye hilo Duka na wakati ana nijibu hilo swali, Mwamba kumbe alikuwa Store na alisikia. Hatari!

Ghafla nikaona mtu anamfuata yule binti kwa ghadhabu iliyo kuu na kuanza kumpiga makofi ya nguvu. Nami nikachoropoka mle ndani.

Sasa, gari imeharibika jirani na Duka, na jamaa namuona tokea muda akiranda-randa na anatambua mimi ndiye mwenye hiyo gari.

Nifanyeje ndugu zanguni?!
Kitu umekosa ni akili.
 
Wewe ile siku niliomba unifundishe ile kitu namna ya kutumia ukaniambia niiulize google sio….. Likewise Manyanza.

Hahahah haya asante kwa kunimiss😂
Jamani ulivyo mkaleee hivi unashindwa kutumia kweli ? 🤣🤣🤣

Wengine tulisoma shule Kiingereza kilikuwa hakuna nisaidie basi hiyo sentence uliyoandika kwa Kiingereza 😃😃😃
 
Usiog
Niliharibikiwa na gari tokea mchana Kijiji kimoja karibu na Makambako huku Nyanda za juu Kusini.

Sasa ndugu zangu, eneo nililopata hiyo breakdown lipo Duka kubwa na mara ya kwanza nilipoenda kununua kinywaji nikahudumiwa na binti mmoja mkali! Kama kawaida ya sisi wa ki-ume, nikameza mate ndugu yenu.

Kisa; nimerejea kwa mara ya pili kununua super glue na ndipo nilipomuuliza kama yupo huru ili nigombee Jimbo. Binti kajibu yupo kwenye mahusiano japokuwa siyo ki vilee.

Bwana bwana, kumbe binti yule ni mke wa jamaa mwenye hilo Duka na wakati ana nijibu hilo swali, Mwamba kumbe alikuwa Store na alisikia. Hatari!

Ghafla nikaona mtu anamfuata yule binti kwa ghadhabu iliyo kuu na kuanza kumpiga makofi ya nguvu. Nami nikachoropoka mle ndani.

Sasa, gari imeharibika jirani na Duka, na jamaa namuona tokea muda akiranda-randa na anatambua mimi ndiye mwenye hiyo gari.

Nifanyeje ndugu zanguni?!
Usiogope mkabili kwani vipi bhana demu si kasema mahusiano hayako kivile ASA uogope nn Mkuu nenda shughulikia gari ila uwe tyr kwa lolote
 
Back
Top Bottom