Enzi za machifu (Mfumwa) wakipare ulitokea ugomvi.
Ndugu kafa, mdogo wake karithi mke. Amezaa na mke mtoto mmoja wa kike.
Mahari ya mtoto wa kike ilipototewa mrithi wa mjane anataka kuichukua akatumie wakati watoto wakubwa wa marehemu walitegemea dada yao akiolewa watatumia mahari ile kuolea.
Kilichotokea watoto wa marehemu walifungua shauri kwa chifu/mfumwa kudai kuwa ile mahari ni halali yao.
Kawaida ndoa ya kipare kimila ni mbuzi dume mmoja kwa jina wanaita "mpingirwa". Hata bibi kizee akiachwa ili itambulike kaachwa wakwe lazima wamrudishe yule mbuzi wa ndoa.
Hukumu ilikuwa hivi;
Chifu alimuuliza mrithi " hivi kaka yako alipokufa mbuzi wa ndoa 'mpingirwa' alirudishwa nawe ukatoa wako upya"? Mdogo wa marehemu akajibu "hapana".
Akaambiwa mtoto huyo huna haki naye, wewe ni sawa na beberu aliyetoka kwenye kundi lake akaenda kwenye kundi la jirani akawatia mimba mitamba ya mbuzi wa jirani, watoto watakaozaliwa wanakuwa wa mwenye kundi, mwenye beberu hawezi kuwadai.
Hivyo kwa mfano huu wewe ni beberu umetia mimba mtamba wa jirani mtoto ni wa jirani si wako.
Sent using
Jamii Forums mobile app