alovera
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 220
- 173
Habari za siku nyingu wandugu, Mwaka 2010 nilioa mwanamke tuliyedumu naye uchumba takribani miaka 5 tena ndoa ya kanisani lakini huyo Mke aliniacha naye akakimbila USA, baada ya hapo mwaka 2012 nikapata mwanamke ambaye nilimkuta na mtoto mmoja ,na sasa tumeshazaa watoto watatu.
Shida yangu ni kuwa kwao huyu binti upande wa Mama yake ni wachawi sana. Bibi yake alishawahi kumdhuru mwanangu wa kwanza mara mbili tukaponea kwa waganga.
Na toka hapo nikapiga marufuku watoto wangu kukanyaga kwao. Siku za karibuni hasa baada ya kutumia Tiba ya Chumvi kama ilivyoelekezwa na baadhi ya members humu jukwaani,nahisi kama nimezinduka fulani naye ameanza kusema kuwa sina mapenzi naye na kuna kipindi anataka kuondoka (nahisi anatishia kwani haondoki).
Binafsi nina amani sana na wanangu lakini yeye hana amani kabisa na kila siku ni malalamiko tu. Lakini sababu kubwa ya malalamiko ni kuwa nimekata mirija yake mingi ya fedha nilizokuwa nampatia yeye na ndugu zake na pia nimemkataza mawasiliano na ndugu zake ambao nahisi ndio wanaopitisha ushirikina kwaangu,
Hili la mawasiliano limeshindiakana kwani nimekuja kugundua kuwa anawasiliana nao kwa siri,lakini pia ndugu zake ikiwamo mama yake wameanza chuki kubwa kwangu na nahisi nashambuliwa sana kishirikina,hatua nilizochokua kwanza ni kuzidisha ibada na sala,pili natumia tiba ya chumvi.
Ushauri naouomba kwenu wanaJamii Forums,nifanyeje niachane na huyu mwanamke bila kuleta mtafaruku kwenye familia yangu tena mimi ndio nibaki na watoto kwani akienda nao kwao nahisi wanangu watadhurika au nao wataingizwa kwenye uchawi.
Nawasilisha