Will Jr
JF-Expert Member
- Jul 21, 2018
- 4,897
- 7,074
Viongozi wa Yanga inabidi waelewe tatizo la Yanga si wachezaji, tatizo letu ni benchi la ufundi. Shida kubwa ninayoiona Yanga ni miundo ya timu (structures). Tunapounda mashambulizi muundo haueleweki na ikitokea tunacheza dhidi ya timu bora zinazozuia nafasi inaleta shida sana kutengeneza nafasi.
Unaweza kufanya rejea ya mechi zote dhidi ya Simba ya Pablo (0-0) au mechi zote za kimataifa tulizocheza chini ya kocha Nabi. Kwa mara ya kwanza niliona hili tatizo ilikuwa Yanga dhidi ya Ruvu shooting (3-1) msimu uliyopita. Hii mechi nakumbuka Ruvu walipata kadi nyekundu ikawa rahisi kwa upande wetu.
Timu ikiwa haina mpira muundo haueleweki pia, tuna press kwenye umbo lipi? Nimemsikiliza Mwinyi Zahera ameongelea kuhusu nafasi za wachezaji hazikuwa sahihi kipindi Yanga inaruhusu goli kule Sudan na kaongelea pia uwiano wa timu inatukosesha uhimili wa mchezo, na yupo sahihi, mfumo wetu hauko compact kabisa.
Hakuna ufahamu kwa wachezaji kwamba mpira upo wapi, adui yupo wapi, mwenzangu yupo wapi, na mimi nikae wapi, wachezaji wanakosa elimu ya msingi kimbinu. Benchi la ufundi ilibidi kufanyia kazi madhaifu haya, ni mambo ya msingi kuliko zile pasi tunazocheza. Nini maana ya pasi nyingi kama timu inapata shida kutengeneza nafasi?
Mwinyi Zahera anasema "Nakuachia mpira ila najua kabisa nitakufunga." [emoji16] Tunasifika kwa kucheza mpira wa kumiliki (possession football) na wachezaji wazuri kiufundi tunao wengi.
Hitimisho;
Ni vizuri mkurugenzi wa ufundi kushiriki kwenye mambo ya ufundi, asikae kama kivuli, anaonekana kuwa na suluhisho ya baadhi ya matatizo yetu.
Ikitokea anatafutwa kocha mpya basi kigezo cha kuangalia CV au historia yake ya nyuma sio lazima, uelewa wake kwa mpira wa kisasa ni muhimu, kigezo kikuu kikiwa winning probability hasa kwenye tough games.