Nimezuiliwa mshahara mwaka sasa

BUMIJA

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2011
Posts
5,950
Reaction score
11,295
Mnamo mwaka 2008nilianza kazi Bagamoyo-Matipwili,nikafanya kazi hadi 2011,nikaomba ruhusa kwenda kusoma,,DEO Alipojua nilzamu yangu kwenda kusoma akanihamisha na mi chuo nilipata,,,,...:na akaniambai hatuwezi kukuruhusu,.::::nikaondoka....Wameziba fedha
 
DEO Alikua na bifu na mimi mana kuna siku nilienda ofisini kwake akafoka na ni kua kosa silijui,,..Kama kuna mwanajf anaweza kunisaidia kutatua tatizo mana nilifanya kazi porini na Headmaster kachangia mana kuna mwanamke alihisi namchukua kumbe la...
 
+255712336687Kwa kweli naomba ushauri mana naonewa na hadi nimekua na chuki na kazi hii ya ualimu,Nikahamishiwa Moreto,...:Ila miaka3nilikaa MATIPWILI.Jirani na hifadhi ya sadani....Simba walikua majirani zetu
 
we acha kuna mshikaji wangu na yeye kazuiliwa mshahara toka October last year ila salary slip zinakuja.... Ma D.E.O ni JANGA wana UBABE wa ajabu kweli wana treat walimu Kama wanafunzi wa kwetu katukataza kuvaa mashati yenye vile vidushu juu Kama ya mapilot eti ni NGuo za kisiasa CDM hili la kuzuia mshahara ni very common Sijui wanafata Sheria gani
 
Na CWT hawatoi msaada wowote! Hebu wasiliana na waziri kivuli wa Elimu au kazi anaweza kukusaidia.. Mimi nilipata tatizo tena kupitia JF marehemu Regia Mtema RIP alinisaidia na nkatatuliwa matatizo yangu, labda na wewe unaweza saidika.. YAANI nikipata mchongo wa kazi kwingine siku naondoka lazima nimpige ngumi afisa elimu
 
Dah poleni sana vijana. Kwani mkiwawashia moto za uso itakuwaje? Kuna kazi ni kipaji, nahisi ningekuwa navaa bukta ofisini niitwe mwalimu ngedere sasa.
 
Sasa itakuaje hapo....Nipate mshahara
 
Duh mkuu hiyo mada umeileta vipande vipande ngoja nikae sawa nikujibu nisije nikaleta majibu vipande vipande...pia
 
Dah poleni sana vijana. Kwani mkiwawashia moto za uso itakuwaje? Kuna kazi ni kipaji, nahisi ningekuwa navaa bukta ofisini niitwe mwalimu ngedere sasa.

mhh wewe na umbo lako sisi wanafunzi tusingesoma...
 
Pole, ila jaribu kuonana na uongozi wa chama cha wafanyakazi, kupeleka malalamiko yako, halafu tuangalie itakuweje!
 
Nitaenda bagamoyo nionane nao
 
mkuu pole sana.wakati unaenda shule ulikuwa umefanya kazi miaka mingapi?ulikuwa na barua ya kuthibitishwa kazini?
 
Kosa kubwa ulilofanya ni kuondoka bila release letter. Kama DEO ana bifu na wewe hapo ndio kabisa lazima akumalize kabisa.Hebu nijibu maswali yangu haya: Lini uliandika barua ya kuomba ruhusa kwenda shule? Ulijibiwa kwa maandishi kwamba hutapewa ruhusa? Ulijaribu kwenda hatua za juu mfano kwa Afisa Utumishi, Mkurugenzi au hata kwa TSD? Chuo ulienda kusoma kozi gani? Baada ya hapo umeandikiwa hati ya mashtaka toka mamlaka ya nidhamu? Umejibu? Umepata barua ya kusimamishwa kazi kwa nusu mshahara? Likizo umejaribu kuitumia ukiwa kituoni kwako? Ukinijibu hayo maswali nitakuwa na kitu cha kusema ila mpaka sasa una hatia ya utoro kazini BUMIJA
 
Last edited by a moderator:
Nitaenda bagamoyo nionane nao
mkuu kuna taratibu za kufanya unapotaka kwenda kujiendeleza,si kila ukipata nafasi lazima uruhusiwe kwenda shule,lazima uwe umetimiza mashart yanayotakiwa!je ulifuata taratibu na masharti husika!!ulikaa kituoni kwa muda gani na ulithibitishwa kazini kabla ya kuondoka na vitu kama hivyo!jaribu kuweka taratibu ulizofuata tuone iwapo una haki au una lazimisha haki iwe upande wako!
 
Ninefanya kazi toka2008-2011,ilikua zamu yangu kwenda kusoma nikahamishwa na wakati chuo nliomba,,...:.Na ruhusa nlikua nayo,,....2015Mungu saidia ifike....::Wabillah Tawfiq
 
Ninefanya kazi toka2008-2011,ilikua zamu yangu kwenda kusoma nikahamishwa na wakati chuo nliomba,,...:.Na ruhusa nlikua nayo,,....2015Mungu saidia ifike....::Wabillah Tawfiq

mkuu,jibu maswali usitafute huruma!
 
DEO Alitamka kua hawezi kutoa ruhusa,..Sina barua yoyote ya kusimamishiwa mshahara,nimethibitishwa kazini,nina TSD NO,Nimdfanya kazi toka2008-2011,nimeenda kwa afisa utumishi anasema niende kwa DEO,Nikiweka appintment simkuti nami nasomea EDUCATION
 
Ulitakiwa uripoti kituo chako kipya cha kazi halafu ungefanya miundo mbinu wizarani ungemgagadua juu kwa juu, ulishajua ni adui yako sasa kwa nini ukampa nafasi ya kukunyonga kiulaini hivyo? Umekaa mwaka mzima ndio unalalamika unafikiri utapataje haki? Kama una hasira kama zangu mpeleke mabwe pande mkamalizane kikubwa!
 
DEO Alikua na bifu na mimi mana kuna siku nilienda ofisini kwake akafoka na ni kua kosa silijui,,..Kama kuna mwanajf anaweza kunisaidia kutatua tatizo mana nilifanya kazi porini na Headmaster kachangia mana kuna mwanamke alihisi namchukua kumbe la...
Kabla sijakushauri chochote naomba nikuulize swali, Je barua ya kuruhusiwa kwenda kusoma na mwajiri unayo? kama unayo hiyo ni defence kubwa kwako, na haki zako zote utapatiwa kwenye vyombo vya sheria, kama huna kuwa mpole tu. maana utachukulika ulitoroka kazi na unaweza kufukuzwa pia.
 
Naomba maoni zaidi +255712336687
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…