Ilitakiwa nifanyeje?[/QUOTE]
Kama nilikufahamu, unaishi pahala palipo na ngozi nyeupe (warabu?, wahindi? wazungu?). Kila moja kati ya watu hawa wana tamaduni tafauti na zetu sisi ngozi nyeusi. Siwezi kusema lolote kuhusu warabu na wahindi lakini kwa kadiri ninavyowaelewa wazungu kidogo ni kuwa, ikiwa bado hamna mazowea ya hali ya juu kabisa kiasi cha kujenga urafiki na uaminifu baina yenu, hawapendi kuulizwa maswali binafsi ya maisha yao (kama hili ulilouliza wewe), imani zao (kama dini), hali zao (kama ndoa) n.k.
Mzungu atakushangaa sana kumwuliza "wewe wa dini gani" "umeoa/umeolewa", hata vitu vidogo sana kama "mbona uko kimya, unawaza nini?". Kwa ngozi nyeusi kama unavyoita wewe ni mambo ya kawaida lakini kwa mzungu haimngii akilini. Unamwuliza dini yake, unataka nini? akiwa tafauti na yako umbague? Unamwuliza kaoa/kaolewa, unataka nini, kumwoa/akuoe wewe?
Kwa ufupi, (t)ungepaswa na (t)unapaswa (t)uwe (m)waangalifu juu ya maswali (t)unayomwuliza mtu hasa ikiwa sio wale ambao
(t)unaaminiana sana.
Nimeweka umojana wingi kwani ni suala linalotuhusu sote.