Nimsaidiaje mhitimu wa kidato cha 4 alayepata Division Zero(0)?

Mkuu..Kuna wengine hawana Akili TU za shule...Hata ungempeleka Feza..(Japo wasingemkubali)
 
Sawa ila nadhani kwa upande wa kurudia, itakua ngumu kwa sababu hata mwenendo wake ulikua wa kusua sua tangu madarasa ya chini.
Kama hili unalijua, mfanyie cancelling asijiskie vibaya tena mwambie kuna namna nyingi za kutusua kimaisha. Mungu ameweka kitu ndani yake na hilo halijatokea bahati mbaya. Kuna sababu hakutaka apitie njia ile ya kufanikiwa but for the mean time akajifunze ujuzi utakaomsaidia Veta. Kisha atajipanga zaidi mbeleni akishakuwa na kitu cha kufanya.

Au kama uko vizuri mfungulie uwakala wa mitandao ya simu na banks pia akikaa sehem nzuri ataweza jipatia riziki yake na kusonga mbele na maisha. Uzuri wa watu ambao wako weak shuleni wana maarifa mengi sana ukiwa expose mtaani. Anaweza buni vitu mpaka ukamshangaa.
 
Sawa ila nadhani kwa upande wa kurudia, itakua ngumu kwa sababu hata mwenendo wake ulikua wa kusua sua tangu madarasa ya chini.
kama ni hivyo kaa naye mjadili yeye anapenda kufanya nini na anataka kuwa nani angekuwa dodoma ningetamani kuongea naye huwenda angekuwa wazi kwangu kuliko kwako.
usimlazimishe kujiunga na vyuo vya veta kwa kile ukionacho wewe bali yeye awe chanzo cha nini kinaweza kuwa msaada kwake.
 
Ila kweli unakaaje na mtoto halafu anapata zero.

Na wewe mzazi au mlezi ni kilaza mwanzo mwisho.

Nyie ndo mnachelewesha uchumi wa juu.
 
Huyo ni sawa na mtoto wa sister wangu. Alijifanya mwamba kila tukimwambia asome ili tusijelaumiana alituona sisi wazushi.

Sasa hapa namsikilizia tu kwanza, akili ikimkaa sawa ndio nitajua tunafanyaje. Si unajua kitaa tena.
 
Achana naye kwanza. Mpe hata miaka mitatu akue kiakili. Ajue maisha sio lele mama. Atambue akipata msaada asiufanyie mzaha. Atambue ni ninianakitaka maishani. Atafanya fanya kazi kuna moja ataipenda. Akikua kiakili ndio umsaidie
Hii ndio misimamo yangu ,atakua amejifunza kidogo
 
Ukali unasaidia.

Ila hawa watoto wa Sisi Wazazi tuokuwa tunakula Ada wanaweza kukushangaza. Utakuta kijana anaona akifeli ni Wewe Mzazi umefeli. Yeye haoni kama inamu athiri!
 
Huyo ni sawa na mtoto wa sister wangu. Alijifanya mwamba kila tukimwambia asome ili tusijelaumiana alituona sisi wazushi.

Sasa hapa namsikilizia tu kwanza, akili ikimkaa sawa ndio nitajua tunafanyaje. Si unajua kitaa tena.
Kwa hiyo mkuu unanishauri nimuache kwanza angalau miaka mitatu mtaani ili apate msoto sio?
 
Ukali unasaidia.

Ila hawa watoto wa Sisi Wazazi tuokuwa tunakula Ada wanaweza kukushangaza. Utakuta kijana anaona akifeli ni Wewe Mzazi umefeli. Yeye haoni kama inamu athiri!
Ni ukweli mkuu, sijui ni kwa sababu huwa hawajapevuka kiakili
 
Sawa mkuu
 
Kwa hiyo mkuu unanishauri nimuache kwanza angalau miaka mitatu mtaani ili apate msoto sio?
Inategemea mkuu. Usikopie kaka utafeli!

Mimi namuacha kidogo coz tulikuwa tunamkanya sana sana sana juu ya kusoma ila alituona mafamba. Sasa ili tumsaidie ni lazima yale ambayo tukimwambie kwa mdomo ayaone uhalisia wake otherwise tutampeleka "vyeta" sasa hivi halafu ataona agghhhh walikuwa wananiambia life tight mbona kama kawa tu.

Kwahiyo inategemea unamuonaje huyo mdogo wako?? Kafeli bahati mbaya au aliyataka?? Anazo heshima kidogo kwako?? Anastahili second chance now?? Au aipate baada ya msoto kidogo??
 
Usisikilize hadithi za Abunuasi. Angalia kipaji chake kimeelekea upande gani, au mapendezi yake ni nini, maana ni dhahiri uwezo wake darasani ni mdogo sana.
Mfano:
1. Mpeleke akasomee umeme wa magari, atapata pesa sana.
Vijana wengi wa kisasa akinunua gari yeye anajua kuwasha na kuweka gia tu, hata kucheki oil hajui!!
2. nk, nk, nk
 
Ushauri mzuri,
Lakini akishakaa mtaani anawezq kubadilika na kujiunga na makundi hapo ni habari yake inaisha,huwezi kumpeleka chuo kijana ambae ashazoea kushika viela
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…