Nimsaidiaje mhitimu wa kidato cha 4 alayepata Division Zero(0)?

Nimsaidiaje mhitimu wa kidato cha 4 alayepata Division Zero(0)?

Haya Matoto pasua kichwa kweli kweli! Mimi hapa nilijidai kuleta toto la dada lililoshindwa shule nikasema liende veta, tukaliuliza vizuri kabisa kwamba lingependa fani gani? Likachagua ufundi ujenzi, tukalilipia kila kitu kwenda chuo lilipokuta kuna kuingia darasani si likaanza utoro wa kijinga kijinga tu! Mara leo liende, kesho lisiende pumbavu kabisa! Wife kwa vile alikuwa ametoa hela yake kulilipia ada akaliwashia moto, khaaa, si likatoroka nyumbani eti shangazi mkali, pumbavu kabisa nikaliambia kwangu lisirudi tena!!
Mkuu ni kweli kabisa vijana wengi wanachelewa kujitambua
 
jinsia gani
Yes waseme; maana mimi nataka kuajiri mabinti wawili waliomaliza kidato cha nne hapa home kuwasaidia wanangu h/w...maana mama yao kasafiri masomoni na mimi muda mwingi nachelewa kurudi home majukumu ya kazi.

Mshahara ni 120,000.
 
Shida mie naona hata ujuzi unaopatikana huko Veta upo outdated, maana nina rafiki yangu ni mwalimu wa veta yeye pia ni koroma, hata msg akiandika mtihani yaan hajui kuandika vzr lkn ndio mwalimu
Sasa imagine anazalisha wahitimu wa aina gani

Yes waseme; maana mimi nataka kuajiri mabinti wawili waliomaliza kidato cha nne hapa home kuwasaidia wanangu h/w...maana mama yao kasafiri masomoni na mimi muda mwingi nachelewa kurudi home majukumu ya kazi.

Mshahara ni 120,000.
Mkuu ni jinsia ya Kiume
 
Ajifunze financial literacy skills Aanze biasharaa awe na mindset ya kujiajiri na kuweza kujifunza fursa mbali mbali yan Aishi kidigitaliii then Aishii maisha halis ajifunze namna ya kuinvest kweny real estate .
 
Ajifunze financial literacy skills Aanze biasharaa awe na mindset ya kujiajiri na kuweza kujifunza fursa mbali mbali yan Aishi kidigitaliii then Aishii maisha halis ajifunze namna ya kuinvest kweny real estate .
Ahsante, ushauri mzuri
 
Ongea naye baada ya kumtoa out kama Upo Mza mpeleke malaika beach resort kama Upo dar viwanja utavijua bana kama Upo Arusha mpeleke sijui Grand melia.
Akishakula baya zote dunia hata kama 50k muweke dogo awe na furaha sana.
Kama anapenda Dada Poa mchukulie mmoja na zana avae apige kama Viwili atoe stress kabisa kichwani.
Afu muulize moyoni mwake kuwa ile sauti ya ndani inamwambiaaje kuwa ni yeye ni nani anapenda kuja kuwa kama nani.
Ndoto yake ama anajiona kwa nani
Mfano Mke Nilikuwa Najiona kwa bamdogo alikuwa akileta Magari yake ya mizigk ya dukani. Scania na tela zake kabila hazijaja semi.
So nilijiambiaga moyoni mwangu kuwa nikija kuwa mkubwa ni lazima nije niwe naleta mzigo Wa Fulani kama huyu mzee.
Sauti ya ndani INA mamlaka makubwa sana tena sana.
Nimesoma ila shule haimo moyoni mwangu mpaka muda huu naifanyia ndoto yangu kazi mana ndo furaha yangu.
Kuna muda Ulifika nikaresechi kutoa semi kama 5 tokea tanga cement mpaka Mza ni bei gani mana ni napenda nikaagiza mzigo hakuna ushindani wowote ule.
Nilipofikia uwezo huo nilijiona kama nimepumua kuwa nimemaliza safari yangu niliyokuwa naiwaza tokea nikiwa mdogo.
Yaani huwa nafurahi sana nikijona nikijaza mzigo hapo semi ama Fuso tandem naupeleka mahali Fulani nafurahi sana.
Hayo ni baada ya kuvumilia kufanya kazi ambazo hazipo moyoni mwangu.
Yaani ile kazi za ofisini unapangiwa namna ya kuvaa Mara uchomekee uvae tai.
Huwa Nakuona kama Niko utumwani.
Asubuhi yabidi uwahi kazi za watu whether or not.
So mie huwa najionaga kama ni utumwa mana ni kama Uko jeshini ambayo hata ukienda kukojoa yabidi uage unakuwa kama Mke Wa MTU ama MTT Wa shule. Andikeni majina mnaotaka kwenda shuleni.

Nb in your mind nimetoa case yangu iwe pia kama fundisho sana kwa vizazi sana na sio kujisifia jamani mana najua humu kuna kila aina ya akili.
Yaani nimesoma kisa Nina uwezo Wa kusoma na kufaulu ila shule haikuwepo kwenye ndoto zangu hata siku moja.
Lasita bro alikuwa ananifukuza niende shule ivyo ivyo ikatokea nikaizoea nikaipiga mana nikiwa nafanya kitu huwa sirembi nafanya kwa moyo mmoja to maximum ultimate power.
 
Heshima kwenu wakuu.

Kama kichwa hapo juu kinavyojieleza. Nina mdogo wangu alifanya pepa ya form 4 mwaka jana (2020) lakini matokeo yametoka amepata Division Zero(0)

Nawezaje kumsaidia huyu mdogo wangu.

Ahsanteni.
Mtafutie kitu cha kufanya anachokiweza maana masomo kwa elimu ya kikoloni ni wazi sio fungu lake!
 
Nasoma coment nacheka sanaa almost wote mnaomshauri hamjawahi kupitia hiyo situation ndo maana kila mtu ana shauri lake labda niwambie kitu hakuna kitu kibaya kama kujiona au wewe mwenyewe kujiona umechelewa ktk maisha hakuna kuchelewa wala kuwahi katika maisha wakati wakupambania maisha yako binafsi mda wote ni sawa tu ili mradi uwe na afya njema tu.

Mimi ni mhanga mwa wahitimu ambao sikufanya vizuri o level unajua kwanini hata mimi sijui kwanini ? Nachojua nilisoma kwa juhudi na maarifa lakini mwisho nikaambulia cr 2 tu na masifuri kibao ni katupwa 4 ya mwisho kabisa so advance nisingeweza kwenda kabisa niende wapi sasa? Hata nilipomwambia mzee wangu hakukata wala hakukubali swala la kurudia au kutafuta taaluma nyingine unajua why? Aliniachia uwanja mpana nichague mwenyewe pakwenda na chakufanya . Nikawaza nikawazua lakini bado nikajiona sinachakufanya zaidi ya kukaa nyumbani sawa kukaa nyumbani hadi lini ?

Nikajiwazia bora nikasomee ufundi wa umeme hicho ndo nilikiona na kipenda lakini sikuwa na uhakika kama nakiweza nikamwambia wazo langu mzee hakupinga akaniuliza tu kuna mkakati mwingine siku za mbeleni au ndo ukitoka huko kwenye umeme ndo umemaliza nikamwambia bado ntakuwa na angalia uwezekana wakurudia pepa la 4 akasema powa akalipa ada nikawa nasoma pale cha ng'ombe Veta ..(electrical installation) trust me veta ni chuo kikubwa cha kukufamya ukue kiakili nimakutana na eatu wazima walionizidi miaka kibao darasa moja wako very serous nikaanza kuaddapt tabia zao za kuwa serous na maisha ni kila kitu unachokifanya watu wanafamilia zao wapo darasani duu! Hapo ni full maushauri tu ya kiutu uzima .

Kwa umri wa wale jamaa nikajiona bado sanaa mimi kusongesha kitabu nikachapa miaka miwili pale nikaondoka na grade 2 yangu safi kwa jinsi umeme ulivyo mgumu kwa theory masoma ya o level yakasome

Hapo ndo nikaona ngoja ni text kurudia pepa .mzee akasema poaa nikaanza twiti mwenge nikachukua masoma yote nilifali isipokuwa hesabu nikarudia kama PC nikasoma kwa fujo huku nafanya ishu zangi za umeme kumbuka kwanza na vihela vya kula kutokana vikazi vyangu vya mtaani si huduma ndogo ma kuomba omba hakupa nikapiga kitabu mwisho pepar nmatokeo nikapa cR mbili tena na mi f kibao kumbuka sikurudia yale masoma nilifauli so jamaa tukamasishana tupige advance sasa cr si ninazo nne tukaanza twiti tena ya nguvu kuja kutoboa nina 2 safii nikajiunga na chuo kwa pesa yangu 3yrs nikatoboa nikarudi kwenye ishu zangu za umeme hadi nilipopata ajira 2011 ndo kiaachana na shughuri za umeme nikaendelea na taaluma yangu ya chuo .hii ni story yangu ya kweli kabisa .nilichojifunza nikwamba baba aliniacha niamuwe mwenyewe kuhusu maisha yangu nami nikafanya kweli .asante baba asante marafiki wote tulistuggle pamoja kwa kupeana moyo.
 
Nimpeleke akachukue ujuzi gani mkuu? Mnaweza nishauri na hapo.
Sasa yeye ndo aseme upi ujuz anautaka???? Sis htuwez sem mpeleke ujuz flan n sio fani ake. We kaa nae chin muhuliz nn kipo moyoni mwake. Mwambie awe huru chchte aseme.

Bcz anaweza kuwa anapenda ushonaji nguo akaogop kkuambia kisa utamuon boya aksema fundi umeme akaenda veta akfeli tena. Ko ushaur wangu we muhulize kirfiki n awe muaz apo ndo utopoteza ada ila ukimchgulia apo 90% ADA inaenda potea
 
Kuna maisha besides shule akiwa serious na kilimo na ufundi mdogomdogo (hasa wa kiume) utanishukuru ila akiwa wa kike ajirembe sana anaweza kuolewa
 
Back
Top Bottom