Nimsaidiaje mhitimu wa kidato cha 4 alayepata Division Zero(0)?

Haya Matoto pasua kichwa kweli kweli! Mimi hapa nilijidai kuleta toto la dada lililoshindwa shule nikasema liende veta, tukaliuliza vizuri kabisa kwamba lingependa fani gani? Likachagua ufundi ujenzi, tukalilipia kila kitu kwenda chuo lilipokuta kuna kuingia darasani si likaanza utoro wa kijinga kijinga tu! Mara leo liende, kesho lisiende pumbavu kabisa! Wife kwa vile alikuwa ametoa hela yake kulilipia ada akaliwashia moto, khaaa, si likatoroka nyumbani eti shangazi mkali, pumbavu kabisa nikaliambia kwangu lisirudi tena!!
 
Kama ni wa kike peleka akasome ususi na urembo ,mfungulie saloon afu achana nae mapema sanaaa atasimama kwa miguuu yake

Kama wa kiume peleka akawe hata fundi boda boda then fungua duka LA spear part ,then achana nae
 
Veta ya zamani sio ya leo, siku hizi wanachukua wenye vyeti vya form four, fani mbili ujenz na useremala, ndio la Saba kwa kozi ndefu, kozi fupi yaani short koz fani zote ndio la saba au waliopata sifur, ushaul mwingi sana veta, form four kwa koz ndefu ndio Kama zari lake wanapata Ajira hata serikalini, la saba au sifuri wanajiajiri tu, au kozi fupi.
 
Tanzania hakuna sekta ilio vizuri sana ambapo muhitumu anakua competent.Workshop zenyewe zina vifaa vya kizamani
Mara nyingine ni bora mtu afundishwe na fundi mwingine hata kama analipwa kidogo tu. Shida tena unakuta watu wengine wana roho mbaya na hataki kumfundisha mtu vizuri. Akipata kijana anataka am-abuse tu na sio kumsaidia.
 
Muwahi tu..usimkatishe tamaa. Ana safari ndefu tu bado. Apambane asibweteke. Afunguke akili, asikae ndani.
 
Heshima kwenu wakuu.

Kama kichwa hapo juu kinavyojieleza. Nina mdogo wangu alifanya pepa ya form 4 mwaka jana (2020) lakini matokeo yametoka amepata Division Zero(0)

Nawezaje kumsaidia huyu mdogo wangu.

Ahsanteni.
Mpeleke q.t akasome mwaka mmoja na arudue mtihani
 
Heshima kwenu wakuu.

Kama kichwa hapo juu kinavyojieleza. Nina mdogo wangu alifanya pepa ya form 4 mwaka jana (2020) lakini matokeo yametoka amepata Division Zero(0)

Nawezaje kumsaidia huyu mdogo wangu.

Ahsanteni.
Peleka chuo cha mafunzo Zanzibar

Itamsaidia
 
Hongera mkuu .Ila hata hivyo akili za darasani umelazimisha sana mazee
 
Yanauzi sana mkuu...bora pesa yako ungesave hata kwa manufaa ya familia
 
Mkuu mwenzio anasema dogo ana kichwa cha nazi yaani lile koroma kabisa! Sasa ataenda akasome tena ataweza?
Doo hakuna koroma nakwambia, sema shule zetu tunazowapeleka madogo wetu na jitihada za wazazi kwenye kumpush kunachangia ufaulu na huwezi amini hilo koroma likafanya vzr

Kama yeye anaamini hawezi amtafutie ujuzi wenye tija ,ila kwangu mie veta siiamini kabisa nimeshuhidia baadhi ya wanafunzi wa pale yaan hawana ndoto tena
 
Kushinda mtihani sio be all..., end all...., badala ya kutuuliza sisi umsaidie vipi muulize yeye umsaidie vipi / wapi..., kuna VETA kibao n.k., kama unafanya kazi fulani unaweza kumchukua na yeye ukaenda nae kama apprentice..., in the end afanye unachofanya wewe (after all life is for living..)
 
Kama yeye anaamini hawezi amtafutie ujuzi wenye tija ,ila kwangu mie veta siiamini kabisa nimeshuhidia baadhi ya wanafunzi wa pale yaan hawana ndoto tena
VETA mkuu wako vizuri sana. Mimi kuna mpwa wangu mwingine ambaye naye kichwa ni nazi, lakini kule anaelewa anasoma ufundi umeme, sasa hivi kila akija likizo hapa mtaani ni kama mfalme! Hawa madogo wanaoshindwa ngeli ni kuwatupa huko angalau waokote ujuzi utawasaidia wakija kuwa wakubwa!
 
Shida mie naona hata ujuzi unaopatikana huko Veta upo outdated, maana nina rafiki yangu ni mwalimu wa veta yeye pia ni koroma, hata msg akiandika mtihani yaan hajui kuandika vzr lkn ndio mwalimu
Sasa imagine anazalisha wahitimu wa aina gani
 
Shida mie naona hata ujuzi unaopatikana huko Veta upo outdated, maana nina rafiki yangu ni mwalimu wa veta yeye pia ni koroma, hata msg akiandika mtihani yaan hajui kuandika vzr lkn ndio mwalimu
Sasa imagine anazalisha wahitimu wa aina gani
Kule mkuu asilimia kubwa ni kutenda! Unaweza kulikuta hilo koroma liko vizuri kwenye practical!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…