Nimshauri vipi?

Joseph

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2007
Posts
3,518
Reaction score
1,089
Nina rafiki yangu na alikuwa katika mahusiano na dada mmoja ambaye wakati huo alikuwa na boyfriend wake ila bado walikuwa hawafikia kuwa wachumba,pia rafiki yangu huyu nae ana mwanamke wake ambaye wamedumu kwa muda mpaka sasa.
Tatizo ni kwamba huyu dada anaolewa mwisho wa wiki hii huku akiwa na mimba ya rafiki yangu wakati muoaji hajui kinachoendelea,na bibie bado kadata kwa rafiki yangu na anasema anaolewa tu kwa kuwa ni heshima kwake na kwa wazazi wake.
Je mtoto akizaliwa jamaa atakuwa na haki ya kuwa na mtoto wake kama akitaka?
 
hapo hakuna ushauri! ni kumwambia huyo bibi harusi aache utovu wa adabu!

reason behind.
1) atafungaje ndoa na mtu mwengine halaf chakula ya ndoa akampe njemba nyingine (iko wazi kwamba atafanya infidelity after ndoa)
2)atambebeshaje jamaa mimba ambayo sio ya kwake
3) atampotezeaje bwanaharusi wakati wake na interest zake.
4)hivi ni kwanini anajiforce na fake love.
5) anatunza heshima gani wakati heshima kubwa ni kuthamini anaekuthamini?
6).................................
7)................................
etc

nyambafff! hii post imenipotezea apetaiti yangu ya ugali.
 
ooh my god nimekosa hata la kusema hapa..hivi huyu dada kama anampenda mwanamme mwingine kwa nini amekubali kuolewa na huyo jamaa .?hatari...
 
ooh my god nimekosa hata la kusema hapa..hivi huyu dada kama anampenda mwanamme mwingine kwa nini amekubali kuolewa na huyo jamaa .?hatari...
kuna watu wengine wamekuja kuongeza idadi ya wazembe tu ulimwenguni including huyu biharusi. huyu hataki ushauri anataka bakora tu.
 
huyu dada ni selfish kupita maelezo!

anajali heshima yake na wazazi wake tu? what about her kid? what about mwanamme anaemuoa?
 



Jamaa anayeoa kwanini hajui kama mke wake mtarajiwa anamimba?
 
i got the right to remain silent....:tape:
 
hakuna ushauri hapo. sidhani kama kuna mapenzi ya kweli kwa hao wanaocheat. huyo kaka angekuwa anampenda kweli huyo dada na hivi anajua ana mimba yake asingekubali aolewe na mwanaume mwingine. na huyo dada anamdanganya tu huyo kaka kuwa anampenda, hana lolote. waache kama ilivyo na pia waache kudanganyana
 
Arrghh ndio maana wengine hatutoacha maisha ya pizza na bia..Upupu tu...
 
kweli kuna watanzania milioni moja na nusu wenye matatizo ya akili....

kabisa kabisa.....ni kweli.....
 
Haya ndo tunayaita makosa ya kiufundi. Nitarudi na kaushauri zaidi
 
Je mtoto akizaliwa jamaa atakuwa na haki ya kuwa na mtoto wake kama akitaka?
Waliochangia wote mbona mnakwepa swali hili? maana dhumuni la mtoa mada ni kupata jibu la swali hili !!! hayo mengine ni blaablaa tuwaachie wenyewe!!
 
ooh my god nimekosa hata la kusema hapa..hivi huyu dada kama anampenda mwanamme mwingine kwa nini amekubali kuolewa na huyo jamaa .?hatari...

Ni kwa sababu akili zake zinamtosha yeye tu..hana tofauti na walioko wodi za vichaa sema hawajamshtukia tu..
 
Depending on hiyo mimba ni muda gani, huyo dada naona badala ya kupata hiyo heshima anayoitaka kwa kuolewa huenda akapata aibu ya mwaka kwake na kwa wazazi wake. Kwanza akiolewa sidhani kama atatulia kwa mme, na mme akijashtuka mimba si yake, au hata bada ya kujifungua akishtukia mtoto si wake itakula kwa huyo shemeji yako!
 
Jamaa anayeoa kwanini hajui kama mke wake mtarajiwa anamimba?
Jamaa anajua kuwa mimba ni yake ila asichojua ni miezi mingapi kutokana na yeye kuwa ni mtu wa kusafiri mara kwa mara.
 
Wadau kwa taarifa rasmi ni kuwa leo ni send off ya huyo bi dada
 
Wadau kwa taarifa rasmi ni kuwa leo ni send off ya huyo bi dada

Inafungiwa wapi hiyo ndoa nikaweke pingamizi la haki?

Hivi Joseph hebu geuza picha iwe rafikiyo ndo nafanyiwa haya; achana na hiyo iwe ndio wewe ama mdogo wako ama kaka yako ama yeyote anayekuhusu!

Piga picha halafu uone unyama unaoshiriki kumfanyia binadamu mwenzio haki yanai LAANA na iko juu yenu nyote hata kama itawachukua 50 yrs am telling you MUNGU HAJARIBIWI hivyo hata siku moja!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…